KUSUDI LA MUNGU UKIWA NA ROHO MTAKATIFU

Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
Unapoamua kubeba kusudi la KRISTO la injili yake unatakiwa kubadilika kutoka kutii dini na unaanza kumtii KRISTO.
ROHO MTAKATIFU Hutufanya Wateule Wa KRISTO Tujione Wa Thamani Mbele Za MUNGU. 
ROHO MTAKATIFU Ana Kazi Ya Kumfanya Mtumishi Wa MUNGU Ayaseme Yaliyo Ya MUNGU. 
Kila Aliyeokolewa Na KRISTO Ni Mtumishi Wa MUNGU lakini wanaoongozwa na ROHO MTAKATIFU hao ndio wana wa MUNGU.
Warumi 8:14 ''Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

Hakuna ROHO Wa MUNGU Nje Na KRISTO. 
 Yohana 14:15-17  '' Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.''

Kama Kuna Mtu Yuko Nje Ya KRISTO Na Anakuambia Kwamba Ana ROHO Wa MUNGU, Huyo Hana ROHO Wa MUNGU Ila Ana roho Ya miungu. 
Hakuna ROHO MTAKATIFU Nje Na KRISTO. 
ROHO Wa MUNGU Ni Wa Muhimu Sana Ila Hatendi Kazi Nje Na Mpango Wa MUNGU Ambapo Mpango Huo Ni Wokovu Katika KRISTO Pekee. 
ROHO MTAKATIFU Atakaa Na Sisi Wateule Milele Kama Tukidumu Kwenye Wokovu Na Utakatifu.

  1 Kor 2:10 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU.  ''

ROHO MTAKATIFU anajua yote hata mafumbo kwetu yeye anayajua na anaweza kutujulisha tukiomba atujulishe.
 ROHO MTAKATIFU Akiwa Ndani Yetu Hutupatia Picha Ya Yale Tuliyoandaliwa Baada Ya Kumaliza Safari Yetu Ya Maisha Yetu Ya Wokovu Duniani.
ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana kwa kila mteule wa MUNGU.
ROHO MTAKATIFU ndiye huzifundisha roho zetu kutenda mema kayatakayo MUNGU kama tukimtii yeye ROHO MTAKATIFU.
MUNGU Baba anasema ''Geukeni kwa ajili ya maonyo
yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na
kuwajulisheni maneno yangu.
-Mithali 1:23 ''

ROHO MTAKATIFU Humfanye Mteule Kuwa Na Tabia Ya KiMUNGU.
 Warumi 8: 8-9 ''Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza MUNGU. Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye
yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake. ''


ROHO MTAKATIFU anazo karama ambazo yeye huwagawia wateule wa MUNGU. Japokua katika baadhi ya makanisa ya leo kuna tofauti nyingi.
 1 Kor 12:4-11 '' Basi pana tofauti za karama; bali ROHO ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na BWANA ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali MUNGU ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa ROHO kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa ROHO apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo ROHO yeye yule; mwingine imani katika ROHO yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika ROHO yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.''
Kibiblia Huduma za ROHO MTAKATIFU zinatambulishwa na kazi yenyewe na sio majina. 
Katika baadhi ya makanisa hakuna watu wanaoitwa kwa majina ya mitume au nabii lakini inawezekana mitume na manabii wapo wengi tu katika makanisa hayo ila sio manabii wa kujiita majina tu Bali vitendo. Mitume wa kweli wapo sana lakini wakati mwingine Mitume wengi katika kanisa la Leo wanaojiita hivyo hata hawafanani kuwa mitume maana hawafanyi utume. Kazi ndio inatakiwa kumtambulisha mtu na sio kujiita tu jina.
 ROHO MTAKATIFU hakukusudia tu watu wajiite majina Bali watende kazi inayoendana na Huduma aliyowagawia kila mmoja
Leo kuna baadhi ya makanisa Huduma 5 za ROHO MTAKATIFU zimegeuka vyeo, yaani mchungaji akipanda cheo anakuwa mtume na mtume akipanda cheo anaitwa nabii, watu wameona kuwa nabii ndio dili wakati ukweli ni kwamba Huduma 5 za ROHO MTAKATIFU kwa kanisa sio vyeo Bali ni kazi za kufanya kwa ajili ya kulikamilisha kanisa kimafundisho ya KRISTO ya injili ya wokovu.

Kimakosa siku hizi Kuna mpaka manabii wakuu, Yaani wakuu wa manabii. Ila cha kushangaza hakuna jipya waliokuja nalo zaidi ya yale tuliozoea kuyaona, tena yakifanywa na watu wa kawaida sana. Ila kutokana na ulimwengu jinsi ulivopoteza dira katika mambo ya kumwendea MUNGU huku watu wakiwa na hamu ya kupata. Basi hao sasa wanatumia fursa hiyo kujiita majina hayo huku malengo yao haswa yakiwa kujinufaisha.
Karama wakati mwingine zinatumika vibaya na hiyo haifai kabisa.

Ni muhimu pia tukajua kwamba Ili Kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Matunda Tisa Ya ROHO MTAKATIFU Yafanye Kazi Kwenye Kanisa.
Wagalatia 5:22-25 '' Lakini tunda la ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa KRISTO YESU wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.''


Naamini kuna kitu umejifunza.
Maombi yangu kwako ni kwamba MUNGU akupe roho ya maarifa na ufahamu.
Ukiwa na ROHO MTAKATIFU hakika utakuwa na ufahamu wa kujua na kupambanua.
Hebu ona jinsi ROHO wa MUNGU alipokuwa juu ya Kijana Danieli na wenzie. Biblia inasema
Danieli 1:17 "Basi, kwa habari za hao vijana wanne, MUNGU aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto."
MUNGU aliwapa vijana hawa roho ya maarifa na ujuzi katika hekima na elimu.
Ndugu Muombe MUNGU leo na wewe akupe roho ya maarifa na ujuzi ili uvitumie kwa utukufu wa MUNGU.
Omba MUNGU akupe na utapata ila tu jukumu lako ni kumtii MUNGU na kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO.
MUNGU alimpa Daniel roho ya ufahamu wa ndoto na maono.
Hata hilo unaweza ukaomba Leo ili ndoto unazoota uwe unazijua maana yake, kwa MUNGU yote yanawezekana, jukumu lako ni kuomba tu na kuishi maisha matakatifu katika wokovu wa KRISTO YESU Mfalme wa uzima.

MUNGU akupe maarifa mema.
MUNGU akupe ujuzi mzuri katika hekima na elimu.
MUNGU akupe ufahamu katika ndoto na maono.
MUNGU akupe maono na Na ndoto ambazo utazijua maana yake na utajua ndoto hizo zimebeba nini na Jambo hilo litakuwa lini.
Akupe ufahamu wa kujua yote yanayokusudiwa kwenye ulimwengu wa roho ili ujue uombeje kuifuta na kuiharibu mipango ya Giza.
Ni muhimu sana wewe kujua maana ya ndoto unazoota.
Ni muhimu sana wewe kujua maono yako yana maana gani na yamebeba nini na hicho kitakuwa lini.
Kwa MUNGU Baba yote yanawezekana.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda(Yeremia 10:6) hivyo mtegemee MUNGU kwa maombi na utakatifu utashinda.

Yote hayo utayafanikisha ukiwa na ROHO MTAKATIFU.

Yuda 1:20-25 '' Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU, jilindeni katika upendo wa MUNGU, huku mkingojea rehema ya BWANA wetu YESU KRISTO, hata mpate uzima wa milele. Wahurumieni wengine walio na shaka, na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili. Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu; Yeye aliye MUNGU pekee, Mwokozi wetu kwa YESU KRISTO BWANA wetu; utukufu una yeye, na ukuu, na uwezo, na nguvu, tangu milele, na sasa, na hata milele. Amina.''

 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments