NI HERI KUMTEGEMEA MUNGU.


Shalom mteule wa KRISTO.
Karibu tukifunze Neno la MUNGU.
Daniel 1:9-16 "Basi, MUNGU akamjalia Danieli kupendelewa na kuhurumiwa na Ashpenazi, towashi mkuu. Lakini, towashi mkuu akamwambia Danieli, “Nina hofu kwamba bwana wangu mfalme ambaye ametoa maagizo kuhusu chakula na vinywaji unavyopaswa kutumia, ataona kuwa afya yako si nzuri kama ya wenzako wa rika lako. Hivyo maisha yangu yatakuwa hatarini.” Hapo Danieli akamwendea mtumishi aliyewekwa na towashi mkuu kumlinda yeye na wenzake kina Hanania, Mishaeli na Azaria, akamwambia, “Tafadhali utujaribu, sisi watumishi wako kwa muda wa siku kumi kwa kutupa mboga za majani na maji. Kisha, tulinganishe sisi na hao vijana wengine wanaokula chakula cha mfalme, halafu utoe uamuzi wako kulingana na jinsi utakavyoona.” Mlinzi akakubaliana nao, akawajaribu kwa muda wa siku kumi. Baada ya siku hizo kumi, aliwaangalia akaona kuwa wale vijana waliokula mboga za majani walionekana wenye afya na nguvu kuliko wale wengine wote waliolishwa chakula cha kifalme. Basi, yule mlinzi akawaacha waendelee kula mboga za majani badala ya chakula cha fahari na divai."


Danieli alimjua MUNGU ndio maana hakutaka kujinajisi kwa vyakula vya kifalme.
Maneno ya kinywa cha mtumishi wa MUNGU yana mamlaka.
Danieli alimwamini MUNGU hata kwa kupitia mtama na maji tu.
Kwa sababu Danieli na wenzako walimtegemea MUNGU basi baada ya siku kumi hakika MUNGU waliyemtegemea aliwawezesha kuwa na afya njema kuliko waliokula vyakula vizuri vya kifahari .
Kumtegemea MUNGU kuna faida kuliko kuwategemea wanadamu.
Kumtegemea MUNGU kuna faida kuliko kumtegemea vitu.


MUNGU ndiye muumbaji wetu na anaweza kutufanya tuwe na afya hata kwa kupitia mtama na maji tu.
Ukimtegemea MUNGU hata kupitia kitu kinyonge tu anaweza kukuinua, ukimtegemea MUNGU utafanikiwa.
Kumtegemea MUNGU ni kufanikiwa.
Ndugu nakuomba mtegemee MUNGU maana MUNGU wetu hashindwi lolote.
MUNGU wetu hashindwi, iwe ni Leo au kesho bado MUNGU wetu hashindwi.


Jambo muhimu sana ni kumwamini MUNGU na kumtegemea kwa kumtii yeye na neno lake.
Usije ukamlaumu MUNGU hata siku moja maana MUNGU sio chanzo cha matatizo yako.
Chanzo cha mayatizo ni wewe na Kama sio wewe basi matatizo yako chanzo chake ni shetani, lakini Neema ya MUNGU katika KRISTO ipo na MUNGU ukimuomba hakika anaweza kukushindia na matatizo yako yote kuisha.
Ndugu mtegemee MUNGU maana utashinda.
Mtegemee MUNGU kwa maombi na utakatifu katika maisha ya wokovu wa KRISTO.


Huu ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
Kwanini kumtegemea JEHOVAH MUNGU wetu?
Ni kwa sababu
" MUNGU wetu ni MUNGU mwenye kutuokoa; BWANA Mungu pekee ndiye aokoaye katika kifo.-Zaburi 68:20 (BHN)


Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
Kuna sababu kabisa ya kumtegemea MUNGU na kushinda.
MUNGU wetu anajibu maombi.
MUNGU Baba anasema
"Uniite wakati wa taabu, nami nitakuokoa, nawe utaniheshimu.-Zaburi 50:15 (BHN)


Hakuna aliye kama JEHOVAH ndivyo Biblia inavyothibitisha.
Biblia inasema
" Ee Mwenyezi-MUNGU, hakuna aliye kama wewe; wewe ni mkuu na nguvu yako yajulikana.-Yeremia 10:6 (BHN)


Ndugu yangu mtegemee MUNGU Baba hakika utashinda.
Mtarajie Bwana YESU katika ushindi wako.


Ukitenda vyema kwa MUNGU hakika maadui zako kwenye ulimwengu wa roho hakika watamuogopa MUNGU wako maana atakutendea makuuu.
Wachawi watamuogopa MUNGU wako maana kwa maombi yako atawapiga.
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
"Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.-Isaya 59:19"
Ni mwaka wa kumtegemea MUNGU na kushinda.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments