UMESIMAMA KWA ZAMU YAKO KATIKA NINI?

Na Mtu wa MUNGU, Mwinjilisti Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Je umesmama kwa zamu yako katika KRISTO au umesimama kwa zamu yako katika shetani?
Au labda wewe umesimama katika zamu yako kwa mambo ya kidunia?
Kila zamu ina malipo yake.
Waliosimama kwa KRISTO kuna uzima wa milele.

1 Petro 1:14-16 ''14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.''

Waliosimama katika mambo ya dunia hao thawabu lao watalipata duniani lakini dhambi zao zitawakosesha uzima wa milele wasipotubu.

1 Kor 6:9-10 '' Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.''


Waliosimama kwa shetani hao wametanguliza kabisa vichwa vyao jehanamu na sasa kiwiliwili tu ndicho kilichobaki kwenda jehanamu.

Zaburi 34:14-16 ''Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie. Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani.''

Ndugu yangu neema bado iko, Wokovu bado uko na maisha matakatifu yanawezekana kuanzia leo.
BWANA YESU anakungoja uamue vyema ili akupe uzima wake.
Yeye Mfalme wa uzima anasema;
''Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Ufunuo 3:20''


Usikubali kuwaiga waliosimama kwa zao zao katika maovu.
Mwanadamu ni wa ajabu sana.
Yuko tayari kupanga mipango mingi sana ya maendeleo ya kimwili na anasahau maendeleo ya kiroho ambayo hutengenezwa na utakatifu katika KRISTO.
Mwanadamu anaweza akawa anafanya mabaya mengi lakini kwa sababu jumapili huenda kanisani basi hujiona yuko sawa. Mwanadamu anadhani ataenda mbinguni kwa sababu jumapili huhudhuria ibada huko siku zingine akiendelea na dhambi. Ibada ni muhimu sana lakini jambo la kujua ni kwamba ibadani tunaenda ili kupata Neno la MUNGU la kutusaidia kuishi vyema.
Sasa mwanadamu alivyo wa ajabu hufanya maovu wiki nzima akitarajia kwenda kutubu jumapili.
Na jumapili kanisani yeye ni mtu wa kusinzia tu ibadani maana shetani alishamkamata zamani.
Ndugu zangu, kifo huwa hakipigi hodi na dhambi zako zinaweza kukupeleka ziwa la moto.




Wagalatia 5:19-21 ''Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa MUNGU.''
 
Unaweza ukadharau sana Neno la MUNGU kwa sababu ndani yako yuko shetani lakini usipotubu na kubadilika hakika jehanamu inakuhusu.

Hujachelewa ndugu ndio maana hata umepata nafasi ya kuusoma Ujumbe Kama  huu wa Neno la MUNGU  hivyo Okoka Leo na anza kuishi maisha matakatifu.
Bwana YESU anaokoa Leo, ukimpokea na kuanza kuishi maisha matakatifu hakika umeokoka.

Yohana 1:12-13 '' Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.'' 
 
Dhambi hazitakufikisha popote ndio maana MUNGU amenituma kwako ili tu nikuambie ugeuke na kuacha uovu wako.
Natamani ufahamu kwanini nakuonya kwa maneno  haya.
Sijui kama unaijua kesho yako.
Sijui kama hao wanaokushangilia kwenye dhambi kama watakushangilia tena siku ukifa.

Ndugu yangu mpendwa sana acha dhambi na jitenge na mambo ya dunia.
Anza kukiishi Neno la MUNGU Leo.

Utakatifu ndio kipimo cha mteule na utakatifu unatokana na kulitii neno la MUNGU

 2 Korintho 6:18 ''Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.''
Andiko hili linatufundisha kwamba MUNGU anatupenda wanadamu wote bila kujali jinsia zetu.
Biblia hapo inaonyesha kwamba kama mwanamke au mwanaume atampa BWANA YESU maisha yake, atakuwa ametengwa mbali na shetani na ataingia katika kundi la watoto wa MUNGU wenye haki sawa mbele zake bila kujali jinsia zao.

Ubarikiwe .
Leo sina mengi sana anza tuombe.


 Tuombe

MUNGU wetu,na Baba wa Bwana wetu YESU KRISTO, tunakushukuru kwa ulinzi wako  leo. Tunakusihi Ee BWANA, wakati huu  uzidi kuonekana kwetu, usituache, wala usiende mbali nasi Ee ngao yetu. Tupiganie dhidi ya adui zetu wanaolenga kutushambulia kupitia ndoto chafu, ugomvi, chuki, kutokulewana kwenye nyumba zetu!Kwa jina la YESU KRISTO.
Tupe amani na kupendana siku zote. Tujalie furaha yako Ee BABA, na shagwe itawale muda wote. Uweza wa ROHO wako Mtakatifu,uwe kiongozi wetu; Kwa Jina la YESU KRISTO.
Tupe maono mapya, tupe kukupenda, tupe Roho ya kukutumikia, tupe ujasiri na uweza wa kuitambua na kuishinda dhambi. Tupe hekima ya kuzijua njia zidanganyazo na ibada za kipepo ili tupate kuweza kuziepuka, Kwa Jina la YESU KRISTO.
Tupe ufunuo mpya juu ya kazi yako,zidi kutukumbusha kulisoma Neno lako na kulitafakari daima, tupe muda wa kukuomba na kukuabudu kama upendavyo Ee MUNGU wetu. Rehema zako na Neema yako, iwe juu yetu; Kwa Jina la YESU KRISTO.
Kwa wingi wa hekima yako, tujalie kadri upendavyo, kupitia ROHO MTAKATIFU, anayetuombea mbele zako daima tena kwa kuugua, hata zaidi tuombavyo. jina lako litukuzwe milele MUNGU wetu uliyetuumba. Asante kwa kujibu maombi haya. Katika jina la YESU KRISTO tumeomba na kupokea.

 Amen Amen.


Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments