USHUHUDA NA KUSHUHUDIA WENGINE.

Na Mtu wa MUNGU, Mwinjilisti Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Maisha Yetu Wakristo Yanatakiwa Yawe Maisha Ya Ushuhuda Kwa Wengine. Mkristo Mmoja Anaweza Kuwa Sababisho La Watu Wengi Kuokoka, Lakini Pia Mkristo Mmoja Anaweza Kuwa Sababisho La Watu Wengi Kuanguka Dhambini Kama Yeye Mwenyewe Ni Mdhambi. 
 2 Kor 3:2-3 ''Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote;  mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya KRISTO tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa ROHO wa MUNGU aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama.''

Maisha ya mteule wa MUNGU ni barua inayosomwa na watu wote. Watu wanatakiwa waisome barua hiyo kwa mema na sio mabaya.
Mtu yeyote baada tu ya kuokoka tayari anakuwa barua ya KRISTO ambayo watu huisoma.
Ndugu ni vyema jambo moja tu kwamba wewe uwe barua njema na sio barua mbaya.
Mathayo 5:16 ''Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze BABA yenu aliye mbinguni.''

Barua yetu njema inayotakiwa kusomwa na watu wote ni matendo yetu mema na ya haki.
Uhalisia Mzuri Wa Maisha Yako Unaweza Kuwa Ushuhuda Mzuri Katika Maisha Ya Mtu Mwingine. 
Ushuhuda Ni Maisha Ya Mtu Yanayoonekana. 
Maisha Ya Mteule Ni Ushuhuda Tosha Kwa Watu Wanaomzunguka. Ni Muhimu Wewe Kujifunza Kutokana Na Shuhuda Njema Za Watu Wa MUNGU Kwenye Biblia ili ujue jinsi ya kuishi kama barua njema inayosomwa na watu wengine.. 
Ushuhuda Mzuri Zaidi Ni Jinsi Unavyomkiri BWANA YESU Mbele Za Watu.
Sifa ya wana wa MUNGU ni kumkiri YESU mbele za ulimwengu wote.
  "Kila Akiriye Ya Kuwa YESU Ni Mwana Wa MUNGU, MUNGU Hukaa Ndani Yake, Naye Ndani Ya MUNGU- 1 Yohana 4:15.

Ni jambo la lazima sana kumkiri YESU maana usipomkiri ni hatari kwako.
“Basi kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za BABA yangu aliye mbinguni. Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za BABA yangu aliye mbinguni “ Mathayo 10:32-33''

Kinywa chako kinatakiwa kimkiri YESU kama Mwokozi, huo ndio ushuhuda.
Matendo yako yanatakiwa yamkiri YESU.
Maisha yako yanatakiwa yamkiri YESU, huo ndio ushuhuda.
Usipomkiri YESU mbele za watu na yeye hatakukiri mbele za BABA wa Mbinguni.
Ni muhimu sana wewe kuwa unashuhudia wengine ili waje kwa YESU.
Kazi ya kuwaleta wengine kwa YESU sio ya wachungaji tu bali ni ya wateule wa MUNGU wote.
Kazi ya kuleta watu kwa YESU ni ya kwako na ya kwangu, sisi tuliookolewa na Bwana YESU.
Unatakiwa sana uwe mtu wa kushuhudia watu.
Shuhudia injili ya KRISTO iliyokubadilisha wewe, inawezekana hata asingekuokoa YESU ungekuwa umeshakufa.
Shuhudia kwa matendo aliyokutendea.
Kushuhudia kile ambacho MUNGU amekutendea ni kumwaibisha shetani. 
Shuhudia kile alichokutendea MUNGU wako ili hata wanaokuroga wajitambue kabisa kwamba wao wanamawazo mgando pia wao ni vichwa chapati na hawatakupata milele maana uko na YESU milele.
 Unapomkiri YESU Mbele Za Watu Unakuwa Unaukiri Uzima Wa Milele, Na Unapomkana YESU Unakuwa Unaukataa Uzima Wa Milele. 
Ndugu, Mkiri BWANA YESU Siku Zote Za Maisha Yako. Ukimkiri BWANA YESU Unapata Nguvu Zaidi Za Kiroho Za Kuendelea Mbele.
Yohana 3:16-18 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''

Ni Kweli Watu Wanaweza Wakakuthibisha Kwamba Wewe Ni Mtakatifu Katika Maisha Yako Ya Wokovu Wa KRISTO, Lakini Nakuomba Licha Ya Watu Kukuthibitisha Na Wewe Unatakiwa Kujithibitisha Kwamba Ni Kweli Unaishi Maisha Matakatifu. Usilewe Kusifiwa Kwamba Wewe U Mtakatifu Wakati Uhalisia Wa Utakatifu Unaujua Wewe. 
Ndugu, Jithibitishe Mwenyewe Ili Kama Kuna Maigizo Fulani Huwa Unafanya Uyaache. 
Kumbuka, Huwezi Kwenda Uzima Wa Milele Kwa Sababu Watu Wanakuita Mtakatifu Bali Utaingia Uzima Wa Milele Kwa Sababu Wewe Ni Mtakatifu Mbele Za MUNGU. 
Kuna Watu Huonekana Ni Watakatifu Mbele Za Wanadamu Lakini Watu Hao Hao Kwa MUNGU Wasiwe Watakatifu. Utakatifu Unaanzia Kumpokea YESU Kisha Kuishi Maisha Matakatifu Katika Yeye.
1 Petro 1:13-16 '' Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake YESU KRISTO. Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.''

Mara nyingine mteule unaweza ukapitia magumu lakini kwa sababu umeutunza utakatifu katika KRISTO songa mbele maana kuna uzima wa milele.
Wakati mwingine ukiona hakuna mtu wa kukutia moyo hakikisha unajitia moyo mwenyewe huku ukiomba sana.
Lakini kama hakuna mwanadamu wa kukutia moyo hata mmoja kutokana na magumu unayoyapitia; Hakikisha unasoma Biblia maana neno la MUNGU litakutia moyo kuliko watu 7.
Lakini hakikisha unajitia moyo katika mema na sio dhambi.

 Usipoteze tumaini maana aliye upande wako ni mkuu Mno.
Aliyeko upande wako ni YESU KRISTO mwenye mamlaka yote.
Omba tu na dumisha utakatifu na utumishi.


 Ndugu, kama wako wasio na ushuhuda mzuri lakini wanajiita wameokoka usiwafuate hao.
Kuokoka sio kujiita tu kwamba umeokoka bali kuokoka ni kumpokea YESU kama Mwokozi kisha unaanza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu katika yeye Bwana YESU.
Usiwe kama wale ambao hawakubali kujifunza Neno la MUNGU.
Kuna watu baada ya kuokoka husahau kuendelea kumtii Mwokozi wao, husahau kuishi maisha ya ushuhuda, hujitenga na Neno la MUNGU kwa sababu ya tamaa za kidunia.
Ndugu kumbuka pia sio wote wamwitao YESU  kwamba Bwana Bwana watakaoingia uzima wa milele, bali ni wale tu wanaotimiza utakatifu kwa MUNGU.
Maana kama Mtu Hawezi Kukubali Kufundishwa Na Neno La MUNGU Hakika Huyo Lazima Tu Atafundishwa Na Dunia. Mafundisho Ya Neno La MUNGU Ni Uzima Lakini Mafundisho Ya Kidunia Na Uharibifu. 

Ndugu shuhudia injili ya KRISTO inayookoa.
Ni kazi yako kuishuhudia injili kwa watu wote.
Wakati mwingine kama umekabwa na majukumu fulani basi tumia pesa yako kuipeleka injili, injili wakati mwingine ni gharama kubwa kuipeleka lakini ni lazima iende.
Waambie wanadamu waje kwa YESU waokolewe kama kweli wanautaka uzima wa milele.
Waambie '' Baba, Mama, Ndugu Zetu. Twendeni Kwa BWANA. Huku Chini Siko Kwetu . Twendeni Kwa BWANA.''

Ni kazi yako kuwaambia na ni kazi yako pia kuisapoti kwa mali zako injili inayopelekwa na wengine maana kwa njia hiyo utakuwa umehubiri injili pia.
Hakuna namna ni lazima injili ihubiriwe pande zote.
Anayetakiwa kuhubiri ni wewe na mimi.
Marko 16:15-16 ''Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.'

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments