WAKRISTO NA WAKRISTO MAJINA.




Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu ujifunze kitu.
Wakristo ni wale waliompokea Bwana YESU KRISTO kisha wakaanza kuishi maisha mataktifu katika yeye.
Wakristo ni wale wanaomwabudu MUNGU Baba katika roho na kweli.
Biblia inasema hivi.
 Wakolosai 2:6-10 '' Basi kama mlivyompokea KRISTO YESU, BWANA, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya KRISTO. Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa MUNGU, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. ''.
Tena Biblia inasema hivi;
 
Warumi 6:23 '' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.'' 

Tena YESU KRISTO anasema 

 '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.-Ufunuo 22:12-13''

Baada ya hayo naomba ujitathimini katika maisha yako ya Ukristo chini nitakujulisha wakristo jina.
 
ALAMA ZA MKRISTO ALIEKOMAA KIROHO.
 
1. Ana KRISTO ndani yake.
2. Ni Msikilizaji Mzuri wa Neno la MUNGU.
3. Ni Mgumu kupokea lawama na ni mkweli daima.
4. Anasamehe mapema
5. Ana ROHO MTAKATIFU ndani yake.
6. Anasaidia wengine kiroho.
7. Ana kiu ya kufunga na kuomba
8. Anategemea neno la MUNGU.
9. Kadri MUNGU anavyompandisha ndivyo anavyozidi kuwa mnyenyekevu
10. Mwepesi wa kutubu
11. Anatafuta amani na kuitetea
12. Anapenda watu na ana huruma
13. Anajua wakati gani wa kuongea na wakati gani wa kukaa kimya
14. Amejawa na hekima katika nyanja nyingi za maisha
15. Anaheshimu watu na anaguswa sana na hisia za watu
16. Ana uvumilivu wa kutosha na hakasiriki mapema.
17. Ana hofu ya MUNGU na ana mtii KRISTO na neno lake.
18. Anatoa heshima panapo staili.
20. Ana ujuzi mzuri wa Uongozi
21. Ni Mkarimu
22. Hachukuliwi na aina yote ya Mafundisho potofu ambayo siku zote yako kinyume na KRISTO.
23. Ni mwanafunzi mzuri wa kuukulia Wokovu na maombi neno la MUNGU.
24. Ana roho ya utoaji
25. Hawashushi watu wengine wala kuongea umbea
26. Ana Imani thabiti katika KRISTO.
27. Ana nafasi katika shughuli za kanisa na na anahudhuria kanisani mara kwa mara.
28. Ni msafi katika kila Nyanja zote za Maisha.
29. Roho yake ipo Sensitive na anachukia dhambi.
30. Hashindani na wengine.




Ni heri kuishinda dhambi kuliko dhambi ikushinde wewe. 
 Biblia inasema.

2 Petro 2:14,21--22 '' wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kuhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana; Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua BWANA na Mwokozi Yesu KRISTO, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa.
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
''


Tena Biblia inasema 
 ''Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza.-Yakobo 4:8-10''
Kisha Biblia inasema
 
1 Petro 1:14-16 ''Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.'' 

Sasa naomba ujue haya  hapa chini.
 
UNAWAJUA WAKRISTO JINA?
 
1- Wanamiliki Bar Na Kanisani Wanaenda,
2-Ni Wachawi Na Wanahudhuria Ibada,
3-Wanawachukia Watu Na Kanisani Wanaenda,
4-Ni Wazinzi Wanafanya Kanisa Sehemu Ya Kufichia Maovu Yao,
5-Wanaukataa Wokovu Wa YESU,
6-Wanaabudu Sanamu,
7-Wameweka Matumaini Yao Kwa Watu Badala Ya BWANA YESU,
8-Hawataki Mahubiri,
9-Hawamtii KRISTO,
10-Wanamwabudu MUNGU Kwa Midomo Yao Huku Mioyo Yao Iko Mbali Nae,
11-Sio Waombaji,
12-Hushika Sheria 2 Za Torati Huku Wakiziacha Sheria 611 Zilizobaki Kwenye Torati,
13-Wanaombea Wafu,
14-Hawamtaki ROHO MTAKATIFU,
15-Huenda Kanisani Jumamosi Au Jumapili Tu,
16-Wakitoa Sadaka Hudhani Wanamtolea Mchungaji Na Sio MUNGU,
17- Husema Uongo
18-Hudhani Kwamba Watakaoenda Mbinguni Ni Dhehebu Lao Tu,
19-Hudhani YESU Ni Malaika Tu Mwenye Cheo,
20-Huchukia Semina Na Mikutano Ya Injili
21-Na Hawana Hofu Ya MUNGU.

22-Mwongozo Wao Sio Biblia Ila Ni Vitabu Walivyojitungia Wao
23- Hawajui kusamehe watu makosa yao.
24-Ni waongo
25-Huenda kwa waganga wa kienyeji.
26- Hutumia mizimu.
27- Wanaipenda dunia na mambo yaliyomo mabaya.
28-Huimba nyimbo za kidunia na kuzisikiliza kila muda.
29-Huwategemea wanadamu badala ya kumtegemea MUNGU.
30- Hutoa rushwa na kupokea rushwa.

  Ndugu Zangu Biblia nasema "Enyi Wagalatia Ni Nani Aliyewaroga?-Galatia 3:1".
 BWANA YESU Anasema "Nyumba Yangu Ni Nyumba Ya Ibada Why Mmeifanya Pango La Wanyang'anyi?"

Marko 11:17 ''Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.'' 
Ndugu yangu nakusihi sana amua kumtii MUNGU kuanzia leo.
acha dhambi na jitenge na maovu yote.
MUNGU akubariki.
By Maisha ya ushindi blog.

Comments