KUWA HIVYO ULIVYO ISIWE SABABU YA KUTOKUMCHA MUNGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu nikujulishe kusudi la MUNGU kwako ili ujue na utengeneze kwa Bwana YESU KRISTO Mwokozi wa watu wote duniani wale watakaoamua kumpokea na kuliishi Neno la MUNGU kwa utakatifu..
Kuwa hivyo ulivyo isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa tajiri isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa na elimu nzuri isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuoa au kuolewa isiwe sababu ya kutokumcha BWANA.
Ni muhimu sana wewe kumcha MUNGU, Kuwa hivyo ulivyo isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU. 


Mathayo 13:49-51 ''Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. YESU aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.'' 


Siku hiyo waovu na uovu wao utakuwa dhahiri. Hukumu ya MUNGU sio kama hukumu za kibinadamu, hukumu ya MUNGU ni halisi maana kila kitu kitakuwa wazi siku hiyo.

Ndugu, Kuwa masikini isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa mheshimiwa isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Waziri isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa mbunge isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa kiongozi mkubwa isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.-Warumi 6:23''

 
Ndugu zangu huu sio wakati wa kujifurahisha katika dhambi bali ni wakati wa kutubu na kuacha dhambi.
Huu sio wakati wa kushanglia dhambi bali ni wakati wa kumrudia BWANA YESU na kutubu kisha kuanza kuishi maisha matakatifu.

Ndugu yangu, Kuwa na watu chini yako isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa na kazi isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa na nyumba isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa na gari isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa wa kwanza darasani isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa mzee wa kanisa isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa mchungaji au Askofu isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema '' Kwa maana MUNGU ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.-Mhuburi 12:14 '' 

 
Ndugu, hakuna kukwepa siku hiyo ya mwisho,Ni siku ya mambo yote peupe.

Ndugu yangu, Kuitwa nabii au mtume au Kujiita Nabii au mtume isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Mtumishi wa serikali isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa na afya njema isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuishi mji mkubwa na sio kijijini isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuishi mataifa ya nje isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema kwamba siku ya mwisho MUNGU atazihukumu siri zote za wanadamu.


Warumi 2:16 '' katika siku ile MUNGU atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa KRISTO YESU.''

 
Je una siri gani ambayo watu hawaijui?
Una uovu gani ambao unadhani uko peke yako ujuaye?
Ndugu hakuna jinsi ila ni kutubu sasa kwa Bwana YESU, kuokoka na kuanza kuishi maisha matakatifu katika Wokovu wake ulio wa thamani sana, MUNGU BABA anakupenda sana na ndio maana amenituma nikujulishe Neno lake hili leo ili utengeneze njia zako.
Biblia inasema '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa.Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.-Isaya 55:6-8''


Ndugu yangu, Kuishi kijijini isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kumuoa mtoto wa kigogo serikalini isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Wewe kutokea ukoo au familia ya kitajiri isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema ''Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.-Mathayo 3:2''


Ndugu yangu, Wewe kutokea familia maskini isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa maarufu isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema ''Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake.Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA , bali vyatokana na dunia.Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele.-1 Yohana 2:15-17''


Ndugu yangu, Kuwa na duka isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Askari isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa meneja isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Mwanajeshi isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema '' Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze. Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;-Isaya 13:9-11'' 


Ndugu yangu, Kuwa balozi isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Mwanamichezo isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Mtangazaji maarufu isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa Mwimbaji anayependwa sawa isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa star isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuwa na upako isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Biblia inasema '' Lakini siku ya BWANA itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya MUNGU, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?-2 Petro 3:10-12 '' 


Ndugu yangu, Kufanya kazi ikulu au ofisi kubwa au ofisi ya rais au waziri isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Wewe ni mwanadamu tu na mwanadamu ana mwisho wake.
Mwanadamu ipo siku atasimama yeye kama yeye peke yake na kufa peke yake. Maiti yake hata waliompenda sana wataogopa hata kuigusa.
Ipo siku utasimama wewe kama wewe na kuondoka duniani.
Ipo siku utasimama wewe kama wewe katika hukumu ya MUNGU.
Biblia inasema juu ya siku ya mwisho kwamba ''Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.-Ufunuo 20-12 ''


Ndugu yangu, Kuwa mke wa tajiri au mtoto wa tajiri isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuzaliwa mjini isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Kuzaa watoto isiwe sababu ya kutokumcha MUNGU.
Ndugu, unataka niseme nini tena?
1 Petro 3:10-11 ''Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.''

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Umeshashare sana jumbe zisizo na maana leo
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments