KWA MAANA HAKUNA UPENDELEO KWA MUNGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuna watu baada ya kupitia magumu kidogo hulalamika na kusema kwamba wale ambao hawajaribiwi wakati huo wao wamependelewa na MUNGU.
Kuna watu hujisababishia magumu hayo lakini wakati mwingine Sio kila jaribu la mtu limesababishwa na dhambi yake .
Majaribu mengine ni hatua tu ya kwenda kwenye utukufu wa kudumu.
Muhimu ni kumcha MUNGU hata wakati wa haribu na namna hiyo.

Usiseme hata siku moja kwamba MUNGU ana upendeleo.
MUNGU hana upendeleo wowote na popote.
Hukumu zake hazina upendeleo, Baraka zake hazina upendeleo.
Ushindi wake hauna upendeleo, Miujiza yake haina upendeleo.
Amani yake haina upendeleo, Na Upendo wake hauna upendeleo.

Jambo la kukumbuka ni kwamba akipandacho mtu ndicho atakachovuna.
Wagalatia 6:7-9 ''Msidanganyike, MUNGU hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.  Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa ROHO, katika ROHO atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.''

Ukipanda mabaya kisha ukavuna mabaya usilaumu wale waliovuna mema kwamba wamependelewa.

Kuna tofauti kati ya kupanda na kuvuna ulichopanda na upendeleo.
Ukipanda utakatifu utavuna mema.
Ukipanda dhambi utavuna uharibifu.
Panda wokovu Wa KRISTO ili uje uvune uzima Wa milele.
MUNGU hana upendeleo ila kila utakalopanda ndilo utakalovuna.

Matendo 10:34-35 ''Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa MUNGU hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. ''


Ni kweli ulizaliwa unalia lakini unaweza ukafa unacheka kama YESU KRISTO ni mwokozi wako na umeishi maisha matakatifu katika yeye. Mwanadamu huzaliwa analia lakini siku akiondoka kunakuwa na Mambo mawili mbele yake: kunakuwa furaha ya milele ya wateule watakatifu wa KRISTO YESU na kunakuwa na kilio cha milele kwa wadhambi.
Japokuwa ulizaliwa unalia lakini unaweza ukafa unalia vilevile kama unaukataa Wokovu wa KRISTO sasa.
nakusihi ndugu yangu  anza upya na BWANA YESU ili uwe mwenye moyo safi mbele za MUNGU muumbaji wako

Mathayo 5:8 ''Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. ''
Wenye moyo safi tu ndio watakaomuona MUNGU, Sio upendeleo huo ila ni utii wao kwa MUNGU ndio umesababisha wamuone MUNGU.


Kuna Watu Majina Yao Yako Katika Kitabu Cha Uzima. Kuna Watu Majina Yao Hayamo Katika Kitabu Cha Uzima Kwa Sababu Hawajampokea BWANA YESU Wala Hawajatubu. 
Kuna Watu Wanadhani Majina Yao Yamo Katika Kitabu Cha Uzima Kumbe Hayamo Kwa Sababu Ya Uovu Wao. 
Mwenye Uwezo Wa Kuliweka Jina Lako Katika Kitabu Cha Uzima Ni BWANA YESU Kama Utampokea Na Kuacha Dhambi. 
Mwenye Uwezo Wa Kuliondoa Jina Lako Katika Kitabu Cha Uzima Ni Wewe Kama Utaiacha Njia Ya Uzima Na Kuendeleza Dhambi Zako. 
Ni Vyema Sana Kila Mmoja Kuzitafakari Njia Zake Maana Wengine Hudhani Majina Yao Yako Katika Kitabu Cha Uzima Kumbe Uovu Wao Umeshayaondoa Majina Yao Kwenye Kitabu Cha Uzima.. Kama Mtu Anataka Jina Lake Liwe Kwenye Kitabu Cha Uzima Basi Aokoke, Atubu Na Kuacha Uovu.
Jina lako kuwa kwenye kitabu cha uzima sio upendeleo bali ni utii wako kwa MUNGU.
Warumi 2:11  '' kwa maana hakuna upendeleo kwa MUNGU.''


 Akaunti Yako Ya Kiroho Ina Hazina Kiasi Gani Katika Ufalme Wa MUNGU?
 Uzima Tulio Nao Sasa Hayo Ni Mema Ya Nchi Aliyotupa BWANA.
 Ukimjua JEHOVAH Ni Nani Katika Maisha Yako, Utamcha Na Kumtii Siku Zote.
Matokeo ya kumcha na kumwabudu katika roho na kweli huleta baraka zake na ulinzi wake na hazina zake njema, sio upendeleo huo ila ni matokeo ya kumcha MUNGU na kuishi katika utakatifu autakao.
Mithali 3:33-34 '' Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.'


Kuna watu wengine baada ya kuomba kidogo hulalamika mbona hawajibiwi kama wengine?
 Ndugu zangu, tatizo la kutokujibiwa maombi kwa wakati wala haliko kwa MUNGU ila kwa waombaji wenyewe.
Usahihi ni huu;
MUNGU Hujibu Maombi Kwa Njia Nne. 
1.  MUNGU Anaweza Kukupa Uombacho Sawasawa Na Ulivyoomba. 
2.  MUNGU Anaweza Kukupa Kikubwa Au Kitu Bora Zaidi Ya Ulichoomba. 
3.  MUNGU Anaweza Kujibu Maombi Yako Kwa Kukuambia "subiri" Maana Muda Sahihi Wa Wewe Kukipokea Kitu Hicho Haujafika. 
4.  MUNGU Anaweza Kukujibu Kwa Kukataa Kukupa Ulichoomba Maana Hakikufai Wewe Hata Kama Wewe Unakihitaji Sana.
Ndugu Usiache Kuomba(Yohana 14:13) Ila Wakati Mwingine Jifunze Kuwa Mvumilivu Huku Huachi Kuomb.
Kumbuka kwamba hakuna anayekupenda kama MUNGU.
Hiyo hewa amekupa yeye, uhai amekupa yeye, uzima ni wake na amekupa.
Yeye anakupenda kuliko wote wakupendao.
Yohana 3:16, ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.''


Kuna Watu Nafsi Zao Bado Hazijaamua Kupona Ndio Maana Hawajapona. 
Kubali Kupona Ili Upone Katika Jina La YESU KRISTO.
Ugonjwa Mkubwa Zaidi Ambao Watu Wanatakiwa Wapone Ni Dhambi Kisha Magonjwa Mengine.
Kumbuka kwamba Kwa MUNGU huwa hatulazimishi ila tunaomba kwa neema na imani mbele zake na tunapokea tulichokiomba.
Japokuwa Wakati Wa Magumu Upo Lakini Ashukuriwe YAHWEH Maana Wakati Wa Furaha Pia Upo.

Jambo kubwa kwetu ni kuendelea kumtii MUNGU Muumba wetu.
Kumtii MUNGU ni kukubali kutenda uliyoagizwa na MUNGU.
Kumtii BWANA ni bora sana na ni jambo la muhimu sana kuwa nalo kila mwanadamu.
Imani yetu lazima imtii MUNGU

 Imani ni kuamini kitu usichokiona lakini kipo na ni halisi.
Imani yako inatakiwa iambatane na utii wako kwa MUNGU BABA.
Imani yako ya kupokea lazima iambatane na kuitii sauti ya MUNGU na Neno la MUNGU.
Watu wengi huamini kwamba watakipokea wanachokihitaji kwa imani kupitia maombi, lakini watu hao wanaweza wakapishana na baraka hiyo waliyoamini kuipokea kwa sababu tu ya kutokumtii MUNGU na Neno lake. MUNGU hana upendelea na anawapenda watu wote ila kanuni yake tu ni utakatifu. Bila utakatifu unaweza ukabishana na mambo mengi ya MUNGU na ukabaki ukishangaa.

Sio upendeleo ila kufanikiwa kwako kutategemea na utii wako kwa KRISTO.
Warumi 8:36 '' Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.''

 Kuna watu MUNGU amewapa macho ya rohoni.
Katika makanisa watu hao wapo sana lakini wengi wao ndio wanaoongoza kuchukiwa kwa sababu ya kile wanachokiona na kukisema.
Mimi namshauri kila mtu kwamba;
''Usimlaumu anayeona rohoni bali fumbua macho yako au omba ufumbuliwe macho ya rohoni ili na wewe uone''


 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.

Comments