LAANA

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Shalomu Kanisa la MUNGU.
Neno la MUNGU ni mzani wetu wa kiroho.
Hapa leo kuna laana 12 zilizotajwa katika Kitabu cha Kumb 27:15-27.
Je ni laana ipi inakuhusu?
Kama inakuhusu tengeneza kwa KRISTO YESU..

Biblia inasema;

Laana ya 1. Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa BWANA, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.

Laana ya 2. Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 3. Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 4. Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 5. Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 6. Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 7. Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 8. Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 9. Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 10. Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.

Laana ya 11. Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.

Laana ya 12. Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.

Kutokuyaweka maneno ya MUNGU moyoni na kuyatii na kuyaishi nayo ni laana.
Kutenda dhambi ni kuitafuta laana.
Kutokutoa Zaka ni laana.
Kumkataa KRISTO na Wokovu wake ni laana na waliolaaniwa hawataurithi ufalme wa MUNGU.
Bwana YESU siku ya mwisho atawaambia waliolaaniwa wote kwamba, '' Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;-Mathayo 25:41''
Kumbe waliolaaniwa wanakwenda jehanamu.
Dhambi ndio iliwafanya kulaaniwa.
Kumkataa YESU na Wokovu wake kumbe ni kuitafuta laana, wengi wameipata laana hiyo.
Ndugu zangu ni muhimu sana tuokoke haswaa na kutubu dhambi zetu na kuanza kuishi sasa kama Neno la KRISTO litakavyo.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Umeshashare sana jumbe zisizo na maana leo
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments