KUFANYA MAPENZI KIPEPO NDOTONI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Shalom mteule wa KRISTO upendwae sana na MUNGU.
Karibu kujua jambo hili linalowatesa wengi.
Kufanya mapenzi kipepo ndotoni chanzo cha tatizo ni shetani kuchukua nafasi na kufanya maagano na mtu husika.

Kuna mambo mengi huhusika:
1. Kuna watu huingia maagano kupitia vitu wasivyoombea ambavyo huvinunua ili kutumia.

2. Kukosa ulinzi wa MUNGU kwa sababu ya michanganyo.

3. Kukosa neno la MUNGU na kushindwa kuomba ipasavyo.

4. Jina lisilotakaswa kwa damu ya YESU KRISTO.

5. Urafiki na shetani

Nimewahi kuombea watu wengi kwa suala hili na wakapona.
Yakobo 4:4, 7-8 ' Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU. Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili."

Ili kupona kunahitajika mambo matatu.
1. Kumtii MUNGU.
2. Kumpinga shetani na vitu vyake.

3. Kuomba katika ROHO MTAKATIFU
 
Changamoto ni kwamba waathirika wa mapenzi ya ndotoni wengi hawana nafasi ya kuomba katika ROHO MTAKATIFU.
Kama mtu kila siku lazima aangalie picha za ngono au video za ngono kisha asome habari ya mapenzi na aangalie filamu ya mapenzi hata ufahamu wake utekwe na ngono, ataponaje huyo?
Hatapona kwa sababu baada ya kumaliza kutazama au kuangalia au kusoma ndipo atakuwa anatamani ngono na ngono hiyo shetani haimsumbui kuileta kwa njia ya mawakala wake waitwao majini.

Ili kupona mtu husika anatakiwa aombe au aombewe MAOMBI YA KUVUNJA CONNECTION ZOTE KATI YAKE NA ULIMWENGU WA GIZA.
ulimwengu wa roho wa giza kuna majini, mizimu, shetani mwenyewe, wachawi, waganga wa kienyeji, wanajimu, wasoma nyota, wasoma bao na kila mtu aliye upande wa shetani dhidi yako ili kukumaliza au kukuharibia.
Hivyo kuifuta connection kati yako na ulimwengu wa roho wa Giza kutasababisha milango walioitumia kuingia kwako wasiione tena na wasiweze tena kuingia kwako, ni rahisi kabisa.


''Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.-Mithali 18:10 ''


Lakini haitupasi kumkimbilia YESU huku tumebeba machukizo ya dunia rohoni mwetu.

''Ukaniite siku ya mateso; Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.-Zaburi 50:15 ''

Lakini hatuwezi kumwita MUNGU huku hatuachi Yale machukizo yaliyomkaribisha shetani.

Mathayo 16:19 ''Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. ''


JINSI YA KUIFUNGA MILANGO YA DHAMBI ILIYOFUNGULIWA KWAKO.

1. Maombi ya toba juu ya kilichosababisha mlango huo wa uovu ufunguliwe.
Matendo 3:16 '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA; ''

Toba huleta furaha na toba husababisha kukubaliwa na MUNGU na kwa njia hiyo milango ya dhambi hujifunga.
Isaya 57:15 '' Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.''


2. Kuacha dhambi.
Mwanzo 4:7 '' Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. ''
Usipotenda vyema dhambi iko inakuotea mlangoni lakini kuacha dhambi hiyo maana yake mlango wa dhambi umejifunga.
Ni muhimu sana kuacha dhambi zote maana dhambi hufungua milango ya mabaya mengi tu.


3. Kuishi maisha matakatifu.
2 Kor 5:17 '' Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.''

Ukiwa ndani ya KRISTO ni lazima ya kale yapite.
Ya kale ni uovu na machukizo yaliyosababisha kufunguliwa milango ya dhambi kwako.
Utayaacha ya kale kwa kuishi maisha matakatifu na kwa njia hiyo milango ya mabaya itajifunga.


4.Kumtii ROHO MTAKATIFU.
Warumi 8:9 '' Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.''

Kumtii ROHO MTAKATIFU hukufanya umpendeze MUNGU na kwa njia hiyo milango ya uovu hujifunga.
ROHO MTAKATIFU anajua mwisho hata kabla ya mwanzo, akikukataza jua tu kwamba anakuwazia mema maana katika hayo anayokukataza mengine yanaweza kufungua milango mibaya kwako, kwa njia ya kumtii ROHO MTAKATIFU hakika milango ya adui hutaiona na haitafunguliwa kwako.
Waefeso 4:30 '' Wala msimhuzunishe yule ROHO MTAKATIFU wa MUNGU; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.'' 


5. Kubadili tabia, kutoka kutii kile kilichosababisha mlango wa uovu ufunguliwe, na sasa unaanza kulitii Neno la MUNGU.
Yakobo 4:14-17 '' walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.''

Kutenda mema hupelekea milango mizuri kufunguliwa na milango mibaya kujifunza.
Hivyo njia mojawapo ya kuifanya milango ya dhambi iliyofunguliwa kwako ifungwe ni wewe kubadili tabia kutoka kutii kitu kibaya na sasa unaanza kutenda mambo mema.
BWANA YESU ametupa funguo za kufunga mipango ya kipepo na inafungika hakika.
Kuharibu kila jambo la shetani kwetu na linaharibika.
Ukiifuta connection kati yako na ulimwengu wa roho wa Giza hakika wanokuja ndotoni ili uingiliane nao hakika hutawaona tena.

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

BWANA YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.

Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.

Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.

Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.

Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

0714252292.
0786719090

mabula1986@gmail.com
 Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments