KUMTAFUTA MUNGU NI KUISHI

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kumtafuta MUNGU Ni Kuishi. 
Wanaomtafuta MUNGU Wanakuwa Wanatafuta Uzima Wa Milele. Tunamtafuta MUNGU Ili Tuishi. 
Kuna Nguvu Ya Mauti Ukiishi Bila Kumtegemea KRISTO.
 Isaya 55:6-7 ''Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa.''

Kuna nguvu katika kumtafuta MUNGU.
Ngoja nikupe mfano huu.
Ilifika Kipindi Mfalme Hezekia Siku Zake Za Kuishi Zikaisha Kwa Sababu Ya Nguvu Ya Mauti Lakini Alipomtafuta MUNGU Aliishi Miaka 15 Zaidi Hadi Ratiba Ya MUNGU Ilipotimia.
 Isaya 38:1-5 '' Siku hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, BWANA asema hivi, Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.  Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba BWANA, akasema, Ee BWANA, kumbuka haya, nakusihi, kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana. Ikawa, neno la BWANA likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, BWANA, Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona machozi yako; tazama, nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.''

 Kumtafuta KRISTO Ni Kuishi, Ndugu Mtafute MUNGU Kwa Maombi Siku Zote.
Umeshawahi kujiuliza kama Hezekia asingemtafuta MUNGU ingekuaje?
Hakika angekufa.
Hata wewe yapo mambo yako mengi yamekufa kwa sababu tu ulishindwa kumtafuta MUNGU ili akusaidie.
Kuna ndoa zimekufa kwa sababu tu wanandoa wale walishindwa kumtafuta MUNGU ili aiponye ndoa yao.
Kuna wachumba uchumba wao ulikufa kwa sababu tu walishindwa kumfatuta MUNGU ilia awaokoe.
Kuna watu walifukuzwa kazi kwa sababu tu walishindwa kumtafuta Mwokozi YESU ili awaokoe na aokoe kazi zao.
Kumtafuta MUNGU ni kuishi.
Kuna wagonjwa walikufa kwa sababu tu wao au ndugu zao walishindwa kumtafuta Mwokozi YESU ili amponye mgonjwa yule, badala yao wao wakaenda kwa waganga na ndio maana mgonjwa akafa.
Kama kuna kitu muhimu kwa kila mtu basi ni kumtafauta MUNGU maana kumtafuta MUNGU ni kuishi.

Wewe imani yako inaona nini?
MUNGU analiangalia Neno lake ili alitimize.
Yeremia 1:11-12 ''Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.''

Je wewe kwenye maombi yako unaona nini?
Kwenye maisha yako unaona nini?
Kama unaona vyema basi MUNGU ataliangalia Neno lake ili akutendee wewe muujiza wako.



Kama Hudumu Katika Fundisho La KRISTO, Je Unadumu Katika Fundisho La Nani?

Japokuwa wapingaKristo hukiri na kutaja mambo yao lakini sisi wateule wa KRISTO tutalitaja jina la MUNGU wetu.
Tutakiri uzima wa milele ulio pekee katika MUNGU wetu.
Tutamtaja YESU KRISTO Mwokozi wetu.
Tutamtaja ROHO MATAKATIFU kiongozi wetu na kuenenda katika yeye.
Tutamkiri JEHOVAH MUNGU wetu na kulitii Neno lake na kuishi katika Wokovu wake.
Zaburi 20:7-8 '' Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, MUNGU wetu. Wao wameinama na kuanguka, Bali sisi tumeinuka na kusimama.''


Nampenda YESU KRISTO Mwokozi wangu maana ametenda makuu maishani mwangu, amenipa uzima wa milele na uponyaji wa nafsi na roho yangu.
Ninaishi kwa sababu YESU KRISTO anaishi ndani yangu.
Hao ndio wateule wa MUNGU, na ndivyo tulivyo.
  Ondoa Vibao Vya Waganga Katika Moyo Wako. Ondoa Vibao Vya Waganga Vilivyowekwa Moyoni Mwako Siku Ulipoviona Na Ukachukua Namba Zao Za Simu Ili Uje Utafute Muda Wa Kwenda Kwa Hao Waganga. Ni Dhambi Na Laana Ndugu.
Ni heri kumtafuta MUNGU maana kumtafuta MUNGU ni kuishi.

Fanya kitu ambacho kitakupa faida baadae
Moja ya vitu vinavyoweza kukupa faida kubwa baadae ni;

1. Maisha matakatifu.

1 Petro 14:19  '' Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita BABA, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO. ''

2. Sadaka sahihi inayompendeza MUNGU.

Isaya 58:10-11 ''na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.''

3. Kujifunza neno la MUNGU.

Wafilipi 4:8-9 ''Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo. Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na MUNGU wa amani atakuwa pamoja nanyi.''
 
4. Zaka kamili.

Malaki 3:10-11 '' Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi.''

 
5. Kusaidia watu kiroho.

Wagalatia 6:1-2 ''Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa ROHO mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya KRISTO.''


6. Kutoa muda wako kumtumikia KRISTO.

Marko 8:34-35 ''Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. ''

7. Maombi.

Mathayo 7:7-8 '' Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. '' 

Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
 Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments