MAOMBI YA KUHARIBU VITU BANDIA KATIKA MAISHA YAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU

 Shalom mteule wa KRISTO upendwae sana na MUNGU BABA.
Karibu tujifunze kisha tuombe maombi ya ushindi.
 Ilikuwa ni siku moja katika maombi ambapo ROHO wa MUNGU alinisemesha kwamba ''Omba maombi ya kuharibu vitu bandia''
Kama kawaida yangu, huwa nafundisha vitu ambavyo mimi mwenyewe nimevifanyia mazoezi baada ya kujulishwa rohoni.

Shetani kazi yake ni kuleta vitu bandia katika maisha ya mtu ili tu mtu huyo asipate vitu halisi au original.
Ukisikia kwamba kuna vitu bandia basi tambua pia kwamba vitu halisi pia vipo.
Ngoja tuanze na mfano huu.
1 Wafalme 3:17-21  ''7 Na mwanamke mmoja akasema, Ee bwana wangu, mimi na mwanamke huyu tunakaa katika nyumba moja; nami nalizaa nilipokuwa pamoja naye nyumbani. Kisha, siku ya tatu baada ya kuzaa kwangu, ikawa mwanamke huyu naye akazaa; na sisi tulikuwa pamoja; hapakuwa na mtu mwingine pamoja nasi nyumbani, isipokuwa sisi wawili tu. Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia. Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu. Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.''

Mwanamke huyu aliwekewa kitu bandia ilihali kitu halisi kipo.
Mwanamke huyu aliwekewa mtoto aliyekufa huku mtoto wake halisi yupo na ni mzima ila amechukuliwa na adui.
Mwanamke huyu asingegundua kitu bandia hakika tangu siku hiyo angeitwa mfiwa wakati ukweli hajafiwa.
Hiyo ndiyo kazi ya shetani, kuleta vitu bandia katika maisha yako, Leo omba ukibatilisha vitu bandia vyote.
Ukimuona mtu ni kichaa kama karogwa maana yake ameondolewa ufahamu na kuwekewa ufahamu bandia kichawi.
Magonjwa ni vitu bandia ndani ya mwili wako.
roho ya kukataliwa ni kitu bandia cha shetani ndani yako.
roho ya kupuuzwa na kudharauliwa ni kitu bandia ambacho shetani amekipanda ndani yako.
laana za wachawi na wanadamu kwako ni vitu bandia ambavyo wakuu wa giza wanaweza kukuwekea maishani mwako.
Leo haribu kwa maombi vitu bandia vyote, haribu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kuna watu leo wako katika mahusiano ya Boyfriend na Girlfriend, jambo hilo ni kitu bandia ambacho kinaweza kumfanya binti akose kuolewa baada ya kuwakataa waoaji huku aking'ang'ania boyfriend ambaye atamwacha kipindi ambacho waoaji hawatakuwepo. Kumbuka ''Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.-Mhubiri 3:1''

Mtu kuwa na mapepo ni  vitu bandia ambavyo vitamfanya awe na akili bandia itakayomwezesha kuamua machukizo ambayo ndio kiini cha bandia.
 Kijana au Binti kuwa na mwanaume wa rohoni wa kipepo huko ni kuwa na kitu bandia kitakachokufanya ukose kitu halisi au original.
Huyo mke au mume wa kipepo ni yule ambaye unamuona ndotoni akitumia sura za watu japokuwa yeye ni jini.
Mke au mume wa rohoni wa kipepo kazi yake ni kuwafukuza wachumba halisi na kuzuia uzao baadae kama huyo mume/ mke wa rohoni hataharibiwa kwa maombi.
Kumbuka majini/Mapepo/Mashetani ndani ya mtu hayawezi kutoka hadi kwa maombi tu katika jina la YESU KRISTO.
Kama uko katika ndoa na bado unasumbuliwa na mke/mume bandia wa kijini hakika ndoa yako itakuwa na migogoro mingi sana, jini huyo usipomfukuza kwa jina la YESU anaweza kuua ndoa yako kabisa, huyo ni kitu bandia kinachotakiwa kuharibiwa kwa damu ya YESU KRISTO.
Leo haribu mambo ya bandia yote ambayo shetani ameyapanda katika maisha yako maana hayo yanakuzuia kiroho na kimwili.
Katika ndoa pia kunaweza kutokea mgogoro kwa sababu tu ya mtu bandia aitwaye hawara au buzi, leo wafukuze hao bandia kwa jina la YESU KRISTO.
Mmeo/Mkeo kuwa na hawara hicho ni kitu bandia ambacho shetani amekipanda katika maisha yako.
Mmeo kuwa wa nyumba ndogo hicho ni kitu bandia ambacho shetani amekipanda katika ndoa yako ili ife.
Wafukuze hao bandia leo kwa damu ya YESU KRISTO ili waiachie ndoa yako iliyo katika matatizo.
shetani anaweza kuondoa furaha na amani katika ndoa yako na kukuletea vita na migogoro, Furaha na amani ni kitu halisi kinachotakiwa kuwepo katika ndoa yako na vita na migogoro ni vitu bandia ambavyo vinatakiwa viondoke kwako kwa jina la YESU KRISTO.
Kuna watu wamerogwa ili ufahamu wao halisi usifanye kazi na sasa ufahamu bandia wa kichawi ndio unafanya kazi ndani yao hata hawawezi kufaulu.
Katika kazi yako naomba utambue kwamba shetani anaweza akapandikiza wafanyakazi bandia(Wanaotumika kipepo) ili tu wewe uonekane mbaya au ufukuzwe kazi.
Leo haribu kwa maombi vitu bandia vyote, haribu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Inawezekana kwa jina la YESU kwa maombi, Biblia inakushauri kuomba,
 Mathayo 7:7-8 '' Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;  kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. ''

Katika kanisa kunawezwa kupandwa waumini bandia(Mawakala wa shetani) ili tu kuharibu utakatifu kwa kanisa na kulivuruga kanisa kiuchumi na kuleta migogoro.
Vitu bandia ni vingi sana hivyo nakushauri leo viharibu vyote vilivyo katika maisha yako, biashara yako, uchumba wako, ndoa yako, masomo yako, uzao wako, ukoo wako na hata taifa lako na kanisa lako pia.
iko tofauti kati ya mtu na mtu juu ya kitu bandia ambacho shetani anaweza kuweka.
Binti mmoja katika maono wakati wa ibada ya mkesha alimuona baba yake mzazi akiwa hana mikono wala miguu bali amewekewa mikono bandia na miguu bandia, Yule binti alinishirikisha juu ya kuombea jambo hilo. Nikamuuuliza maswali kabla na yaliyokuwepo kwa baba yake ni kwamba alikuwa ni maskini sana na kila akijaribu kilimo, biashara hakuwahi kufanikiwa ana juhudi sana sana lakini hakuwahi kufanikiwa hata kidogo.
Kumbuka mikono ya baraka chanzo chake  ni rohoni na sio mwilini, ipo siku nitafafanua kwenye somo lingine juu ya mikono kibiblia.
Sio kwamba mtu mwenye mikono bandia au miguu bandia katika hali kimwili halisi ni kosa, lakini ukimuona mtu kwenye ulimwengu wa roho ana mikono bandia au miguu hilo ni jambo baya na omba ukifuta vitu bandia hivyo kwa damu ya YESU KRISTO.
Kuna wanandoa hawajapa watoto sio kwa sababu ya mama bali ni baba kwa sababu tu huyo baba amewekewa uume bandia kichawi. Huwa wakipima hospital wanaambiwa ni wazima lakini kupata mtoto imeshindikana kwa sababu tu ya uume bandia.
Kuna ndoa hakuna furaha ya ndoa kwa sababu tu ya uume bandia ambao hauwezi kufanya kazi yake vyema kumtosheleza mwanandoa wa kike, msilaumiane bali ombeni na hata ombeni maombi ya kufunga.

Baba mmoja alikuwa hajaokoka na alikuwa ana tatizo kubwa katika ndoa yake, hawara alimroga kiasi kwamba akiwa tu kwa hawara ndipo uume wake unafanya kazi, akiwa kwenye ndoa yake anakuwa na uume bandia. Ndugu acha dhambi na tafuta msaada kwa YESU.
Ndugu Leo haribu kwa maombi vitu bandia vyote, haribu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.

Wakati mwingine dhambi zako ni mlango wa shetani kukushambulia, na njia mojawapo ya shetani ni kukuletea vitu bandia maana ni wewe umemfungulia mlango.
unaweza kuwa katika uchumba halisi kabisa lakini uasherati ukakuletea ndoa bandia.
Kumwacha YESU KRISTO ni kuutafuta msaada bandia.
Kwenda kwa waganga na wachawi ni kufuata vitu bandia ambacho vitakutesa miaka mingi.
Ndugu Leo haribu kwa maombi vitu bandia vyote, haribu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
 MUNGU akubariki sana na jiandae kununua kitabu changu cha MAOMBI YA KINA ambacho kimechachapishwa tayari na kinasubiria tu uzinduzi siku chache zijazo. Ukipenda pia kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu na MUNGU akubariki sana.
Maombi haya chini naomba yamsaidie muombaji mchanga katika kuliendea hitaji lake mwenyewe, kwa waombaji wazoefu najua baada tu ya kusoma somo wanajua waombee nini na kipo wapi ambacho ni bandia.

MAOMBI YA KUHARIBU VITU BANDIA.

JEHOVAH MUNGU wangu wa upendo ninakuabudu na kukushukuru. Ninaungana na malaika mbinguni kukuabudu na kukusifu Muumba wangu.
Niko sasa katika eneo hili na muda huu nikiomba damu ya YESU KRISTO iachiliwe sasa kuja katika eneo hili na ardhi yake, Ninaomba ROHO wa MUNGU anisaidie kuomba na kuniondoa katika mitego ya vitu bandia ambavyo mawakala wa shetani wametega vinipate.
Damu ya YESU KRISTO inenayo mema sana naomba sasa katika jina la YESU KRISTO ikanene mema kwangu, katika mwili wangu, afya yangu, kazi yangu na kipato changu.
Kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninaharibu vitu bandia vyote ambavyo shetani anavitumia kama antena na kuninasa, Naharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila kitu bandia katika nafsi yangu, mwili wangu na roho yangu Naharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila kitu bandia katika akili yangu, mawazo yangu na fikra zangu Naharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila kitu bandia katika familia yangu na ndoa yangu Naharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Mchumba bandia anayemuwinda mchumba wangu, namfukuza huyo bandia kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mfanyakazi bandia anayetaka nifukuzwe kazi namfukuza huyo bandia kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mchawi anayetaka nisifaulu na nisifanikiwe namfukuza huyo bandia kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
watu bandia wanaoifuatilia ndoa yangu nawafukuza wote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Marafiki bandia wanaonishauri na kuwa karibu na mimi kwa lengo baya  nawafukuza wote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila kitu bandia katika maisha yangu  naharibu na kufuta hicho kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Viungo bandia katika mwili wangu au wa wanangu au wa mwezi wangu wa ndoa  naharibu na kufuta hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kazi bandia ambazo nazifanya bila kujua na hizo sio kusudi la MUNGU kwangu  naharibu na kufuta hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
migogoro na chuki katika ndoa naharibu na kufuta hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
magonjwa yote ni vitu bandia kwangu, sasa naharibu na kufuta  kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kuchanganyikiwa nakuondoa sasa,  naharibu na kufuta  kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Chuki katika familia na ukoo wangu ni kitu bandia na sasa naharibu na kufuta  kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila kitu bandia kokote kilipo katika maisha yangu naharibu na kufuta hicho kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila eneo la maisha yangu na kila nafasi yangu iliyovamiwa na vitu bandia naharibu na kufuta hivyo bandia  kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Nakushukuru MUNGU Muumba wangu maana katika wewe mimi nimeshinda.
Nakushukuru Bwana YESU Mwokozi wako maana umeniokoa na kunikomboa leo na kwa jina lako vitu bandia nitaviona vikitoweka katika maisha yangu kuanzia muda huu.
YAHWEH wewe ni  MUNGU tangu milele iliyopita na milele ijayo, Nakushukuru MUNGU wangu maana umejibu maombi yangu leo.
Katika jina la YESU KRISTO Mwokozi wangu AMEN AMEN AMEN.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments