TUMWACHE YESU TWENDE KWA NANI?

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze ujumbe maalumu kuhusu uzima wetu.
Ni ujumbe kwa njia ya maombi.

Tuombe.

BWANA YESU  unastahili BWANA, unastahili heshima na utukufu maana ulikufa msalabani ili tu sisi tuokolewe.  Neno lako linathibitisha likisema '' ....  Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia MUNGU kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa MUNGU wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. -Ufunuo 5:9-10''

Hakika hata sasa tumeokolewa na wewe. shetani hakutaka tuokolewe lakini hakuna wa kushindana na wewe BWANA wa uzima wetu. na shetani kwa kupitia wewe amewekwa chini ya miguu yetu kama neno lako linavyosema katika Warumi 16:20 kwamba '' Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]   '' 
walipokuchoma mkuki na kukuvika taji ya miba walidhani wamekuweza kumbe ndio mwanzo wa utukufu wako mkuu zaidi.  na siku ukirudi kila jicho litakuona kama neno lako linavyosema katika Ufunuo 1:7-8  Kwamba '' Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema BWANA MUNGU, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. '' 
Walipokuua walidhani wameshinda kumbe ndio mwanzo wa ushindi wetu ndio mwanzo wa injili kumwendea kila mtu. Walipokuua walidhani wameweza kumbe badala yake wokovu ndio kwanza unaendelea Na agizo lako linabaki kwetu likiagiza '' Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la BABA, na MWANA, na ROHO MTAKATIFU; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.-Mathayo 28:19-20'' 
ni nini kitutenge na upendo wako BWANA YESU?
Warumi 8:35-39 '' Ni nani atakayetutenga na upendo wa KRISTO? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa MUNGU ulio katika KRISTO YESU BWANA wetu. ''

Hakika  Hakipo cha kututenga na upendo wako.
Wastahili BWANA YESU maana ulibeba mizigo yetu ya dhambi na magonjwa na sasa tuko huru.  

Neno lako BWANA linathibitisha haya kwamba YESU  ''. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na MUNGU, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.-Isaya 53:4-5'' 
BWANA YESU tunakupenda na tunapenda uzima wako BWANA, ulifufuka kwa ajili yangu BWANA. Sina kile kipimo sahihi cha kukulipa ila nakutumikia maisha yangu yote, naliishi neno lako na nimeshinda kwa wewe. Damu yako ya thamani kuliko damu zote imezingira pande zote, adui wameshindwa kwa jina lako BWANA YESU. BWANA asante kwa kuja ili mimi mwanadamu niliyedharaulika nipate heshima, ulikuja ili kumtoa shetani aliyetutesa na sasa yuko kuzimu akisubiri adhabu. 
Nakutukuza BWANA YESU maana mamlaka yako ni kuu sana, ulimfunga shetani kwa uweza wako, majini ya mapepo yanatoroka yakikuona BWANA, una nguvu BWANA wa utukufu. Jina lako ni kuu sana BWANA, Neno lako linathibitisha hilo katika Yohana 14:13-15 '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya MWANA.  Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu.'' 
Unastahili heshima zote, unastahili adhama na enzi kuu, unastahili sifa na utukufu wote. unastahili kupigiwa magoti yetu yote.  unastahili BWANA wa mabwana na hakika umetukuka MFALME wa wafalme. pokea sifa BWANA. 
 ''Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.-Zaburi 98:1'' 
Nakushukuru BWANA YESU kwa upendo wako mkuu kwangu. Kama dunia haikujui lakini sisi tunajua kwamba wewe ndio uzima wetu. ''BWANA ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.-2 Timotheo 4:18'' 
 Anayekukataa BWANA YESU huyo anakataa uzima wa milele na anayekupokea wewe umesema hutamtupa nje Kamwe. Tena ulikuja ili tuwe na uzima sasa kisha uzima wa milele. Nakutukuza sana BWANA.
 ''bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.-Isaya 40:31''
Hakika wewe ni MUNGU mwenye nguvu na BABA wa milele. Dunia nzima inasubiri tu ujio wako BWANA. Wewe ndio utawahukumu wote wenye mwili, hakuna atakayeitoroka hukumu yako.  Wewe unasema katika Neno lako kwamba ''Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.-Ufunuo 22:12-13  ''
Kondoo wako tutaenda uzimani . 
BWANA YESU nakuomba uturehemu sawa sawa na fadhili zako. Tuwe uweponi mwako na tuwe kwako daima. Ya dunia yasitushinde BWANA na ROHO MTAKATIFU ambaye ulimtuma kwetu tunaomba atuongoze daima. 
Hatuwataki makristo wa uongo wala hatutayumbishwa na dunia maana uzima wako ndio dira yetu pekee.  pale kalvari kila mtu alikiri kwamba wewe una nguvu baada ya giza kuja baada ya wewe kuondoka . hakika wewe ukiwepo giza halipo na ndio maana BWANA nakuomba ubaki nasi daima. Neno lako liko wazi sana kwamba anayekukataa anaukataa uzima wa milele 
Yohana 14:6-7  '' YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na BABA; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona.'' 
Tupe ushindi wako na baraka zako. Tusonge na wewe BWANA YESU siku zote za kuishi kwetu. shetani na mawakala wake wote wameshindwa kwa jina lako BWANA YESU. Tunashinda na zaidi ya kushinda maana wewe ndio ushindi wetu. unastahili BWANA kupokea heshima na utukufu wote.
 hakika wewe ni MUNGU mkuu na mwokozi wetu. 
Tito 2:13 ''tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa KRISTO YESU, MUNGU mkuu na Mwokozi wetu; ''
kwako BWANA tunaishi na kwako BWANA tutakuja siku ya kuondoka kwetu duniani ikifika maana wewe hata sasa unatuandalia makao mazuri.
 BWANA tupe ushindi na uvumilivu ili tuifikie mede ya thawabu ya wito mkuu wa MUNGU BABA katika wewe BWANA wetu.
 asante BWANA YESU na uje BWANA
Ufunuo 22: 20-21 ''Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, BWANA YESU. Neema ya BWANA YESU na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.''
Kwa YESU KRISTO tumeomba yote na kupokea, Amen Amen.
 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA. MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
 +255714252292
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili. MUNGU Akubariki.

Comments