PETER MABULA ANAZINDUA KITABU CHAKE CHA KWANZA.



Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU KRISTO apewe sifa wateule wa MUNGU.
Jumapili wiki hii yaani tarehe 9 April 2017 Kitabu changu kiitwacho MAOMBI YA KINA kinawekwa wakfu kwa maombi kisha kuanzia jumapili hiyo kitapatikana kwa kila anayekihitaji.
Kitawekwa wakfu Kanisani Kawe Pentecostal Church saa saba Mchana, Jinsi ya kufika panda gari zozote za kwenda Kawe na ukifika kituo cha Ukwamani au Kituo cha Kanisani Ulizia Hospitali ya Dk Mambo, Pembeni tu ya Hospitali hiyo ndipo Kanisa lilipo.
Nakukaribisha ndugu yangu na rafiki yangu uniunge mkono katika hili.
Kitapatikana kwa bei ya Tsh 8,000 tu na wanaohitaji kwa bei ya jumla tuwasiliane, utapata kwa bei nafuu sana.
Pia unaweza kumnunulia na mwenzako na utakuwa umeipeleka injili ya KRISTO mbali sana.
Ndani ya kitabu hivyo Kuna masomo na maombi mengi, Kwa Uchache utakutana na haya ndani ndani ya kitabu hicho.
1. Jinsi ya Kuomba katika ROHO MTAKATIFU.
2. Aina za maombi.
3.Jinsi ya kutumia madaraka yako ya siri ili kuwashinda maadui zako katika ulimwengu wa roho.
4. Faida saba za maombi ya kufunga.
5. Maombi ya kuiharibu mitego ya mwindaji anayekuwinda.
6. Maombi ya kuing'oa na kuizima mishale yote ya shetani iliyorushwa kwako.
7. Maombi ya kuiangusha mipango mibaya dhidi yako.
8. Maombi ya kuzifuta alama za kishetani zinazokufanya uonekanae na mawakala wa shetani.
9. Maombi ya kukirudisha kilichoibiwa kiroho.
10. Maombi ya kusambaratisha vikao vya wanaokujadili kwa hila.
11. Kumwomba MUNGU ili afanye jambo jipya
12. Maombi ya kuomba nguvu za rohoni ziongezeke.

MUNGU wa mbinguni akubariki sana sana.
Mwisho kabisa nawashukuru sana sana wale wote waliotoa sadaka zao za hiari ili kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki, Hawa katika maombi yangu huwa ninawaombea sana na MUNGU wa mbinguni naamini ametenda na atatenda tena na tena ushindi.
2 Kor 13:14 ''Neema ya Bwana YESU KRISTO, na pendo la MUNGU, na ushirika wa ROHO MTAKATIFU ukae nanyi nyote. ''
AMEN AMEN AMEN.

 

Comments