UNA LAANA GANI?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu .
Karibu tujifunze somo hili fupi kuhusu laana.

Laana ni kitu kinachomkamata/Kumfunga mtu ili asifanikiwe katika mambo Fulani.

Kuna laana za aina 3.

1. Laana ya kulaaniwa na MUNGU.
 
Hii hutokea kwa sababu ya kutokutoa fungu la kumi sahihi
Malaki 3:9-10 "Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la."


Laana nyingine ya MUNGU huja kwa sababu ya kufanya kazi ya MUNGU kwa ulegevu au kukataa kufanya maagizo ya MUNGU.
Yeremia 48:10A "Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; "


Ngoja nikupe mfano huu; Mchungaji mmoja ambaye ni rafiki yangu alisikia sauti ya MUNGU kwamba amtumikie kwenye nafasi ya uchungaji. Yule ndugu alikataa, baadae sauti ili iliendelea lakini hakutii. Baada ya hapo kilichofuata ni yule ndugu kufukuzwa kazi alikokuwa ameajiriwa, baada ya pale matatizo mfululizo yalimwandana sana, alitafuta kila sehemu lakini alifukuzwa au alikataliwa kupewa kazi. Ukame usio wa kawaida wa pesa ulimwandama, baadae aliikumbuka sauti ya MUNGU na alipoanza tu kumtumikia MUNGU baada ya kutubu matatizo yote yakaisha.
Huo in mfano hai.
Jinsi ya kuondokana na laana ya MUNGU ni kutubu kwa MUNGU na kuacha uovu uliosababisha ukapata laana.


2. Laana ya kujilaani mwenyewe.
 
Maneno huwa yanaumba
Mithali 18:21 "Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake."


Kuna watu hujilaani kwa kujitamkia maneno yatakayowafunga.
Kuna watu wanateseka sasa kwa sababu tu ya maneno mabaya waliyojinenea wenyewe.
Biblia inasema kwamba mwanadamu anaweza akafungwa kwa maneno yake.

Mithali 6:2 "Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,"

Tena Biblia kwa maneno yako utahukumiwa na kwa maneno yako utahesabiwa haki.
Mathayo 12:37 "Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa."


3. Laana ya kutamkiwa na wanadamu na laana inayotoka nguvu za Giza.

Hii ndio laana ambayo huwatesa wengi sana.
Kuna watu wamelaaniwa na wachawi kichawi.
Kuna watu wamelaaniwa na ndugu zao au wazazi wao.
Kuna watu wamelaaniwa na waganga kwa njia ya watu kuwaendea kwa waganga.
Kazi ya shetani ni kuleta uharibifu na uharibifu laani ni sehemu moja katika hizo.
Shetani anaweza kutumia majini, mizimu au maadui zako wanadamu ili kukulaani.

Jinsi ya kuondokana na laana hizi ni maombi ya kina katika jina la YESU KRISTO.
 
Kazi ya YESU KRISTO ni kutuweka huru lakini ni hadi tuamue kuwekwa huru
Yohana 1:12" Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake;"


Jinsi ya kuwekwa huru ni kumpokea YESU kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu na maombi
Yohana 14:13 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana."


Baada ya kuokoka na kudumu kwenye kusudi la MUNGU laana zitakazofuata za kutoka kwa wanadamu au walioupande wa shetani zinaitwa laana zisizo na sababu hazitakupata hata kama watakulaani Mara nyingi kiasi gani.
Watu wengi wa MUNGU husumbuliwa na laana za zamani kabla hawajaokolewa na Bwana YESU, hizo zinaweza kuendelea kuwepo na kumtesa mhusika kama hataomba kufuta laana hiyo.
Neno la MUNGU hutupa nuru ya kufahamu jinsi ya kuomba na maombi yetu tukiwa katika Wokovu wa KRISTO.


MUNGU akubariki na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Umeshashare sana jumbe zisizo na maana leo
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments