USHUHUDA MFUPI WENYE FUNDISHO NDANI YAKE.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Usiku wa kuamkia leo nilikuwa naandika somo la maombi ya kubatilisha maneno mabaya aliyojinenea mtu zamani.
Katikati ya somo nikiwa naandika ghafla nikaona maono akina dada fulani nisiowajua wanalia baada ya kusoma somo hilo.
Baada tu ya kuamka leo asubuhi simu ya kwanza kupokea ni ya Dada mmoja kutoka mbalia sana ambaye aliniambia kwamba baada ya kusoma somo hilo alilia sana huku akisema kwamba hata yeye madhara ya kujinenea mabaya na kunenewa yameshampata na kumpiga.
Nimebaki nikitafakari maono hayo na simu ya Ndugu huyu nikabaki naamini kwamba YESU KRISTO kuna wengi sana huwaweka huru pale wanapozingatia Neno la MUNGU.

Ndugu yangu unayesoma ujumbe huu, nakuomba sana uwe unazingatia Neno la MUNGU maana mahubiri mengine unayofundishwa Kanisani kwenu au Kwenye semina au redioni au popote hakika wakati mwingine ujumbe huo ni ujumbe wako binafsi ili ama utengeneze na MUNGU ama ujue jinsi ya kutoka katika vikwazo vya kipepo vilivyokufunga.

Yeremia 23:29 ''Je! Neno langu si kama moto? Asema BWANA; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande? ''
Neno la MUNGU ni la MUNGU tu na Neno hilo lii hai.'
Changamoto katika baadhi ya watu ni kuwadharau wachungaji wao au watumishi wa MUNGU katika maeneo yao kiasi kwamba hawawezi kuzingatia Neno la MUNGU wanalotoa.
Mfano kama wewe unamdharau mchungaji wako hakika ni vigumu kuzingatia Neno la MUNGU ambalo MUNGU anampa Mchungaji huyo ili likusaidie wewe.

Waebrani 4:12 ''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.''

Katika makanisa ya leo kuna watu hata kutoa sadaka ni tatizo kanisani lakini akija mchungaji mgeni Kutoka nchi ya mbali kuhubiri kisha akasema weka sadaka nzuri kwenye bahasha hakika kuna watu wanaweza hata kuuza viwanja ili wapate sadaka ya kutoa, sio vibaya kutoa huko lakini MUNGU wakati mwingine huvitumia vinyonge kwa ajili yako.
MUNGU anaweza akamtumia Mchungaji wako huyohuyo na ukafunguliwa hakika.
MUNGU anaweza akamtumia Mzee wako wa kanisa huyohuyo na wewe ukawa huru.
Jambao muhimu kulizingatia ni kwamba zingatia Neno la MUNGU haijalishi anayelitoa hilo neno ni nani.
Kama ni Neno la MUNGU hilo lina sauti ya MUNGU ndani ya Neno hilo ili kukusaidia wewe.

Moja ya vitu ambavyo mimi naviogopa sana ni kuwa Mchungaji. Huwa natamani niwe Mwinjilisti tu wa kuhubiri kila wilaya na kila mkoa lakini kuchunga Kanisa la mahali ni kazi ngumu sana.
Ndugu zangu ni vigumu kuisikia sauti ya MUNGU na kuitii kama wewe una roho ya kiburi kwao hao ambao MUNGU anawasemesha na kuwapa Neno kwa ajili yako.

Mchungaji wako anaweza kuwa ni mzee lakini hiyo haimzuii MUNGU kumpa Neno Mchungaji huyo kwa ajili yako.
Kuna maneno ya MUNGU mengi ni kama Password za Kadi ya Benki kwako. Unaweza ukawa na pesa nyingi benki na Atm card unayo lakini kama huna password hakika huwezi kutoa pesa na ukaipata.
Kuna maneno ya MUNGU mengine ni Password kwako, ukitendea kazi kwa maombi yako kwa YESU hakika unaweza kupata baraka yako ambayo umekuwa unaiona kwenye ndoto tu ila haijawahi kuidhihilika katika mwili.
Kuna maneno ya MUNGU ni yako kabisa ili utengeneze na MUNGU kwa toba au ujue jinsi ya kuomba.
Neno la MUNGU ni la MUNGU tu haijalishi Neno hilo analitoa nani, kama ni la MUNGU katika kweli ya MUNGU hakika hilo Neno ni la muhimu sana kwako.

Sitasahu sikumoja moja Mwaka 2011 usiku nikiwa Zanzibar nikisikiliza Redio Wapo. Usiku ule nilikuwa kwenye wakati mgumu sana na nilikuwa kwenye hatari kubwa sana lakini ghafla muhubiri aliyekuwa anahubiri alinitaja jina langu katikati ya mahubiri, hakunijua jina na nahakika hata hakumbuki kama alinitaja lakini aliponitaja alinitia moyo sana kwa maneno ya MUNGU ya kuniimalisha, sitasahau siku hiyo.
Siku moja nikiwa sekondari Biharamulo Mwaka 2003 nilikuwa naumwa sana sana baada ya kula Biskuti ambayo mimi naamini ilikuwa ya simu na Neema ya MUNGU nikafungulia redio na kukuta Mwl Mwakasege anahubiri. Alipomaliza kuhubiri alisema mtu anayeumwa ashike eneo analoumwa, Nikashika na kuombea na kupona. Sasa jiulize kwamba Mwakasege hakuwa anahubiri live bali ni CD ya magubiri yake ilikuwa imewekwa, lakini Cd ile ilikuwa na Neno la MUNGU na Neno la MUNGU siku zote li hai na nilipona.
Ningedharau hakika ningeendelea kuumwa.

Kuna watu leo MUNGU anaweza akawasemesha kwa kupitia mahbiri ya watu wanyonge kabisa ili tu watubu maana wako katika wakati wao wa mwisho kuishi, mtu kama huyo akidharau anaweza akapishana na uzima wa milele.

Kuna watu wameaacha kuabudu makanisani kwao kwa kisingizio kwamba wachungaji huwahubiri wao tu.
Kumbe wachungaji wao wala hawajui kwamba huwa wanawahubiri watu bali wao husema kile ambacho MUNGU amewapa.
Hebu jiulize umekutana na Neno la MUNGU na akili yako ikakutumwa kwamba ni mtumishi huyo tu anasema na wewe kwa chuki zake, kumbe ni MUNGU nasema na wewe kupitia Neno lake ili utengeneze.

Ndugu zangu naomba tujue kwamba MUNGU huzunguza sana sana kupitia Neno lake.
Mimi naamini MUNGU huzungumza zaidi na sisi kwa njia ya Neno lake hata kuliko vitu vingine.
Ni vyema kulitiii Neno la MUNGU.

Mimi sijui umejifunza nini katika ujumbee huu ambao nimekuletea lakini nakuomba tu mtii Mchungaji wako na viongozi wako wa Kanisa.
Waheshimu watumishi wa MUNGU walio karibu yako maana wakati mwingine MUNGU anaweza kusema na wewe kupitia wao na hata wao wasijue kwamba ni MUNGU nasema na wewe kupitia wao.
Asante kama umeelewa ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments