HII SIKUIPENDA HATA KIDOGO

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Mara moja hii nimejisikia vibaya sana.
 Siku za karibuni usiku niliota ndoto nikimuona mtu mmoja kwa sura yangu mimi akiwa mbali kidogo na Mimi nilipokuwa. Mtu yule sio Mimi ila alikuwa anapost kila ambacho Mimi nilipost na alitumia majina yangu ila alikuwa anapost kwa kuwaomba watu pesa akitaja maeneo mbalimbali kwamba yuko huko kuhubiri hivyo wamtumie pesa. Mtu huyo ana group za WhatsApp na covers za group hizo ameweka picha za kitabu kiitwacho UJUZI KATIKA MAOMBI, Kitabu hicho ni masomo yangu yaliyobadilishwa vichwa vya somo tu, huku icon za groups hizo akiweka picha yangu Mimi nikiwa nimevaa shati la kitenge.
Ana/wana profile Facebook na ana/Wana page Facebook.
Lengo lake/lao ni kuwaibia watu pesa zao kwa kuwaambia wawatumie pesa wako vijijini kuhubiri wanahubiri, Mara wako mijini na maeneo tofauti tofauti wakihubiri kumbe wala si kweli.

Ndugu zangu, Mimi Peter Michael Mabula sio mtumishi mkubwa kiasi kwamba watu watumie jina langu kuibia pesa watu.
Mimi wala sina umaarufu wowote, na siutaki huo umaarufu.
Mimi napenda sana watu wanapochukua masomo yangu au post zangu na kuziposti sehemu mbali mbali, nabarikiwa sana na hilo. Napenda mno mtu achukue Neno la MUNGU nililipost na kulipeleka kwingine kwa lengo la kuwafungua watu ili tu wauijie Wokovu wa Bwana YESU KRISTO na kukombolewa.
Sijwahi kumzuia mtu kuchukua Ujumbe wangu haijalishi amenijulisha au hajanijulisha.
Natambua kabisa kwamba Kanuni ya KRISTO katika injili yake ni kwamba Ukifundishwa Neno la MUNGU basi neno hilo ulilofundishwa na wewe kawafundishe wengine, Ndivyo mtume Paulo alivyomwambia Timotheo.
2 Timotheo 2:2 "Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine."


Baada ya ndoto hiyo yalipita kama masaa 7 tu ndipo nilipoujua ukweli katika uhalisia.
Ndugu mmoja aliniandikia Meseji WhatsApp akiomba nimuadd mwenzi wake kwenye group langu la WhatsApp maana anabarikiwa sana na masomo yangu kila ninapopost. Nilipoangalia namba yake nikagundua kwamba siko naye katika group lolote la WhatsApp. Nikamwambia group linaitwaje? Akanijibu na kunishangaa kidogo maana Mimi ndio admin na mwanzilishi wa group na ni muda mrefu ameona nikipost na kuelekeza watu wanipe pesa Niko pahali nahubiri kumbe sio kweli. Nikaamua kuongea na huyo ndugu kwa simu maana alisema mambo magumu na ambayo siyajui na wala hayanihusu.
Kwenye simu alinieleza mambo mengi sana ambayo huyo Peter Mabula fake anayafanya kwa lengo la kupewa fedha. Yule ndugu aliyekuwa ananieleza inaonyesha kabisa kwa neema ya MUNGU alisoma maoja ya masomo yangu na kuchukua namba na Leo kwa neema ya MUNGU akanipigia simu Mimi akidhani anampigia simu huyo Peter Mabula fake.
Aliongea mengi tu yule ndugu na baadae nikasema kwamba huyo Peter Mabula anayemsema yeye ni mwingine na kwa sababu anatumia masomo yangu kwa hila basi ni mtu fake na Mimi siamini kama mtu huyo ameokoka na siamini kama ni mtumishi wa kweli wa MUNGU Bali ni tapeli anayewahadaa watu akitumia picha zangu na masomo yangu. Hadi baada ya Mimi kutoa kitabu cha MAOMBI YA KINA naye katoa cha kwake kwa kutumia masomo yangu.
Yule ndugu baada ya kumweleza alinishangaa kwa jinsi alivyomwamini huyo Peter Mabula fake. Ghafla akaanza kuniambia maneno magumu akisema kwamba Mimi ndio Peter Mabula fake Bali yule ndio Peter Mabula ariginal. Nilimwelekeza Kanisani kwetu Kawe na hata kesho anaweza kunipata lakini msimamo wake ni kwamba namdanganya.
Neno hili liliniumiza.
Alieleza hadi post ya mwisho ya huyo Peter fake ni somo langu alilolibadili.
Ndugu zangu hiki ni nini?

Mimi binafsi naomba niseme yafuatayo.
Mimi napatikana kwa email ya mabula1986@gmail.com na sio vinginevyo.
Najua masomo yangu yanatumika kwenye blog nyingi na website nyingi tu lakini Mimi binafsi napatikana kwenye blog ya Maisha ya ushindi ambayo hupatikana kwa anuani ya www.maishaushindi.blogspot.com na sio kwingineko. Kuna blog wanaweza kubadili namba za simu chini ya somo lakini ukitaka kunipata Niko kwenye blog yangu mwenyewe ambayo zaidi ya Mara Milioni 2 watu wameifungua na kujifunza neno la MUNGU.

Facebook napatikana kwa Page mbili yaani page iitwayo Maisha ya ushindi ambayo ni page ya blog yangu, page hiyo ina marafiki hadi sasa Elfu 7 na kidogo.
Page yangu nyingine ni Mwinjilisti Peter Mabula ambayo ina marafiki elfu 5 na kidogo.
Profile yangu ya Facebook ni Peter M Mabula yenye marafiki elfu 5 na followers 1800 na kidogo kwa sasa .
Namba zangu za simu za Huduma ni 0714252292 na 0786719090 tu japokuwa wachache nimewahi kuwatumia namba ya voda kwa sababu maalumu maana simu ninayotumia kwenye Huduma ina line mbili hivyo nikitoa namba ya voda mtu anaweza kunitafuta hata mwaka bila kunipata maana simu ninayotumia ina laini 2.
Ukiona mtu anakutafuta kwa jina la Peter Mabula kwa namba zingine nje na hizo akisema ni Mimi mkatae na muonye aache ujinga wake, kwanza Mimi huwa siwapigii watu simu Bali wao ndio hunipigia maana ni wengi.
Facebook pia nilianzisha group liitwalo Neno la MUNGU lenye marafiki laki na 34 elfu hadi sana na group lingine linaitwa Biblia takatifu lenye watu elfu 20 na kidogo.
WhatsApp Nina magroup mawili tu ambayo yanaitwa Neno la MUNGU original na Neno la MUNGU original 2. Najua kwa WhatsApp watu wameshaniadd kwenye groups zaidi ya 40 lakini yangu mwenyewe ni hayo mawili tu.

Wewe unayetapeli watu nakuonya kwa jina la YESU KRISTO, acha na okoka.
Unaweza ukawaficha wanadamu lakini huwezi kumficha MUNGU Baba ndio maana kwa Neema ya MUNGU nimefunuliwa Leo na kugundua.
Ndugu zangu ni kweli kabisa wakati mwingine nimewahi kuwaomba watu sapoti ili inisaidie hiyo sapoti kuchapisha Vitabu. Kwa neema ya MUNGU nimeshachapicha kitabu cha kwanza na kwa neema ya MUNGU na sapoti ya watakaopenda mwezi wa kumi nitachapisha kitabu kikubwa sana cha maombi, sikitaji Leo ili huyu tapeli asianze yake.
Kuna watu waliguswa kunisaidia na pesa yao hiyo nilitumia hata kununua computer ya kuandalia masomo, Mara chache pia kuna watu wamewahi kunitumia zawadi na mara zote nimekuwa nawaombea sana watu waliowahi kunisapoti.
Ni Mara chache sana sana imewahi kutokea kusapotiwa katika hayo niliyoyasema lakini ilinisaidia sana sana.
Ndugu zangu najua siku Bwana YESU aliponitokea kwenye maono ya kunipa jukumu la kuhubiri injili yake, najua wajibu wangu kwenye injili ya KRISTO iokoayo. Nimewahi hadi kukwazana na watumishi wa MUNGU wakiniomba niwe napost vipande tu vya masomo na sio kila siku. Nilikataa kwa sababu sikuitwa katika kulingishia watu Ujumbe kisha niwaambie wakitaka ufafanuzi zaidi wanitafute. Najua kabisa watu wengi tu wanayatumia masomo yangu vibaya lakini hiyo haitakiwi kunifanya niache kuhubiri maana wengi tu wanaokoka ma kufunguliwa na wananijulisha hivyo nikiwabania hao kwa hofu ya wengine wenye nia mbaya nitakuwa nawazuilia kuokoka hawa walioandaliwa na MUNGU wanisikilize kwa maandishi na kufunguliwa wakizingatia.
Ningeweza ningebadili template ya blog yangu na kuweka pin kiasi hakuna ambaye angeweza kukopi somo langu kutoka kwenye blog yangu, ningekuwa natuma tu link Facebook ili mtu akitaka kusoma somo alifuate kwenye blog na huko hawezi kuliondoa kwa vyovyote.
Hayo sikuyafanya ili kila mtu ajifunze neno la MUNGU kwa Uhuru na uwazi.

Nina mengi mno ila ngoja niishie hapo.
Kama ni muombaji omba katika kweli na MUNGU Baba atajibu.
Najua tapeli atauedit Ujumbe huu pia ila naomba ajue pia MUNGU hadhihakiwi na Neno la MUNGU huwa halidhihakiwi.
MUNGU akubariki.
By Mwinjilisti Peter Mabula.
0714252292
0786719090
Mabula1986@gmail.com.

Comments