MAWAKALA WA SHETANI WANAOJIINGIZA KWA SIRI KANISANI.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Baadhi ya sifa au kazi wanazozifanya Mawakala wa shetani zimeainishwa katika maandiko kama ifuatavyo,
Neno la Msingi ni Warumi 1: 18-32''
Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao. Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema; ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao. '
'


1. Wanamjua MUNGU lakini hawamtukuzi.
Warumi  1:21 '' kwa sababu, walipomjua MUNGU hawakumtukuza kama ndiye MUNGU wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.'' 
Leo kuna baadhi ya watumishi hujitukuza wao na sio MUNGU.
Leo kuna watu wanaujua kabisa mpango wa MUNGU wa Wokovu na wanajua kabisa bila YESU hakuna uzima wa milele, lakini watu hao hao hujitenga na YESU na kuanza kufuata machukizo ingawa wanajua kabisa kwamba kwa makosa hayo wanajitenga na uzima wa milele.
Wanohubiri uzushi wao hao ni mawakala wa shetani na ni rahisi tu kuwagundua. Tunawajua kwa kuwapima katika Neno la MUNGU.
1 Yohana 4:1-3 ''Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Katika hili mwamjua ROHO wa MUNGU; kila roho ikiriyo kwamba YESU KRISTO amekuja katika mwili yatokana na MUNGU.  Na kila roho isiyomkiri YESU haitokani na MUNGU. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.''

2. Wazushi.
Uzushi ni ni tendo la kuzua mambo yasiyo ya kweli.
2 Petro 2:1-3 '' Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata BWANA aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.  Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.'' 
 Wazushi wengi wapo leo wakizusha vitu ambavyo wala sio Biblia inaagiza ili tu kuwakosesha watu.
Wanazusha ili kujipatia faida, hao ni mawakala wa shetani.

3. Wanajifanya wana hekima ya MUNGU wanaponena.
Warumi 1:22 '' Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;''
Kuna watumishi leo hujifanya wana hekima sana lakini hicho wanachofundisha kwa hekima ni cha kishetani.
Kuna watu leo husema kwa hekima na upole kwamba MUNGU ni wa huruma sana na hivyo hatawaadhibu wanadamu katika jehanamu ya moto, hiyo ni hekima lakini ni ya shetani.
Kumbuka shetani hafanyi kazi kwa hasara, anajua kabisa kuna watu wakiambiwa kwamba hata wasipotubu hakuna adhabu kwao basi huacha kutubu na kunyenyekea kwa MUNGU kwa sababu tu wameisikia hekima fulani lakini ni hekima kutoka kwa shetani. Hiyo ndio kazi ya mawakala wa shetani.
Wengine husema kwamba tunaweza kuwaombea wafu hata wakabadilishiwa makazi kutoka kuzimu na kupelekwa mbinguni, hiyo ni hekima ya kishetani maana Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu, hivyo kama kuna watu wanatubu kwa ajili ya marehemu basi hiyo ni hekima ya kibinadamu ambayo haina msaada wowote kwa aliyekufa. Elimu kama hiyo huzaa matunda kwa watu kudhani kwamba hata wakifa katika dhambi basi kuna watu huku duniani watawaombea na wataenda uzima wa milele, huo ni uongo wa shetani.
Waebrania 9:27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;''

4. Wanaubadili utukufu wa MUNGU asiye na uharibifu kwa mfano wa binadamu aliye na uharibifu na ya ndege na wanyama.
Warumi 1:23-25 ''wakaubadili utukufu wa MUNGU asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo MUNGU aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya MUNGU kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. ''
Kuubadili utukufu wa MUNGU ni kubadili mpango wa MUNGU na kujipata utukufu.
Leo kuna watu huabudu sanamu, MUNGU wala hafanani na sanamu, hayo ni machukizo na huko ni kuubadili utukufu wa MUNGU.
Leo kuna wakristo hutambika, huko ni kutokujitambua.
Leo kuna watu hubadili taratibu za MUNGU kwa kufanya machukizo, huko ni kuubadili utukufu wa MUNGU.


5. Wanafuata tamaa za mioyo yao na kuvunjiana heshima miili yao pia Wamebadili matumizi ya asili ya mke au mme na kufuata yasiyo ya asili na kwa njia hiyo Wamebadili kweli ya MUNGU na kumtukuza shetani.
Warumi 1:26-27 '' Hivyo MUNGU aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.'' 
Leo kuna hadi watumishi wanafungisha ndoa za mashoga makanisani, huo ni ushetani ni ni alama muhimu ya kuonyesha uwakala wa shetani.
Leo wanaume waliooa wanawaingilia wake zao kinyume na maumbile, huo ni uwakala wa shetani.
Leo kuna wanaume wanalawitiana, huo ni uwakala wa shetani.

6. Wanapenda ubaya, husuda, uuaji, fitina, hadaa, nia mbaya, wasengenyaji na wasingiziaji na wasioheshimu wazazi wao wa kiroho na wa kimwili
Warumi 1:29-30 '' Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya, wenye kusingizia, wenye kumchukia MUNGU, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, '' 

17. Wanajua kabisa mambo ambayo MUNGU hataki lakini wao wanayatenda.
 Warumi 1:32 '' ambao wakijua sana hukumu ya haki ya MUNGU, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.''

Hao ndio mawakala wa shetani.
Ni Wenye kumchukia MUNGU, majivuno, kutunga ubaya na  jeuri
Hawatii maagano ya MUNGU na hawapendi jamaa zao.
Hawana rehema n.k

Machoni wananena ya amani, moyoni wanaotea.
Walalamikaji, wanungunikaji, wenye vinywa vinenavyo maneno ya kiburi, wanapendelea wenye cheo kwa ajili ya faida.
Mteule wa MUNGU uwe macho maana hizi ni siku za mwisho.
2 Yohana 17-11 '' Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa YESU KRISTO yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo. Jiangalieni nafsi zenu msiyapoteze mliyoyatenda, bali mpokee thawabu timilifu. Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya KRISTO, yeye hana MUNGU. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba(MUNGU) na Mwana(YESU) pia. Mtu akija kwenu, naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu, wala msimpe salamu. Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.'

MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu

Comments