MADHARA YA DHAMBI NI MABAYA SANA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu kujifunza Neno la MUNGU.
Wanadamu Wa Ajabu Sana.
Kuna Watu Wako Tayari Kununua Moto Kwa Pesa Zao Wakati Uzima Wa Milele Upo Na Unapatikana Bure.
Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Zao Kwa Kwenda Kwa Waganga Wa Kienyeji.
Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Zao Kwa Kulipia Gesti Ili Afanye Uzinzi.
Kuna Watu Hununua Moto Kwa Pesa Kwa Kutoa Mimba,
Kuna Watu Hununua Moto Kwa Pesa Zao Kwa Kununua Pombe.
Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Zao Kwa Kwenda Disko Kumshangilia Shetani Na Wanaye.
Kuna Watu Hununua Jehanamu Kwa Pesa Kwa Kusema Uongo Baada Ya Kupewa Pesa..
Kuna Watu Hununua Moto Kwa Pesa Kwa Kutoa/kupokea Rushwa.
Ni Hatari Na Ajabu Mwanadamu Ananunua Moto Kwa Pesa Zake Ilihali Mbingu Ipo Na Inapatikana Bure Bila Kutoa Hata Senti 5.
BWANA YESU Anaokoa Na Ukimpokea  Bure Unaokoka Na Huko Ndiko Kununua Uzima Wa Milele Bure

Yohana 3-16-21 '' Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.''


Ndugu, Leo Ndio Yako Itumie Kwa Kuokoka Maana Kesho Haijulikani Kama Ni Yako Au Sio Yako.
BWANA YESU Yuaja Na Atamlipa Kila Mwanadamu Sawa Na Matendo Yake.

 Warumi 10:9-11 '' Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.''

Unafanya dhambi kwa faida ya nani?
Kama ulikuwa hujui sasa na naomba ujue kwamba ukifanya dhambi ni kwa faida ya shetani na pia ni kwa hasara yako binafsi.
Faida ya shetani ni kwa sababu utajinajisi na kumkosea MUNGU pia dhambi hiyo inaweza kusababisha ukose mbingu, usipopata neema ya kutubu basi kinachofuata ni jehanamu.
MUNGU anatutaka tuishi maisha matakatifu kwa faida yetu wenyewe.
Usipookoka na kuishi maisha matakatifu ni kwa hasara yako mwenyewe.

Ni heri sana kila mwanadamu kumcha MUNGU kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi na kuishi maisha matakatifu katika yeye.

Haijalishi ni nani lakini kama anakuambia kitu cha ki-MUNGU kipokee maana kitu hicho kitakusaidia sana maishani mwako.
Kumbuka MUNGU hutumia watumishi wake hata kama watumishi hao kibinadamu wataonekana ni wanyonge wa kawaida sana.

Ndugu usiwakinai watumishi wa kweli wa MUNGU.
Usikinai mafundisho yao na usikinai ushauri wao kwako.
Usikinai Neno la MUNGU wafundishalo na usikinai maelekezo yao kwako.
Usikinai maonyo yao wapewayo na MUNGU Baba kwa ajili yako.
Usikinai kuhudhuria ibada wanazofundisha Neno la MUNGU.

Usikinai injili yao ya kweli katika KRISTO YESU Mwokozi.
Ndugu nakuomba sana usiwakinai watumishi wa kweli wa MUNGU katika Wokovu wa YESU KRISTO
.

Yakobo 4:7-9 '' Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.  Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza. ''

Kumbuka pia hii kwamba Dini ni mpango wa mwanadamu kumtafuta MUNGU au mungu na kumwabudu.
Kwa maantiki hiyo tunagundua kwamba dini inaweza ikamwabudu MUNGU wa kweli lakini pia dini inaweza ikamwabudu mungu yaani shetani.
Ukitaka dini ya kweli basi hiyo inaanza na neno la KRISTO.

Warumi 10:17 "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO."

Ni Kwamba "Kila Akiriye Ya Kuwa YESU Ni Mwana Wa MUNGU, MUNGU Hukaa Ndani Yake, Naye Ndani Ya MUNGU- 1 Yohana 4:15.

Kukiri Huku Ni Kumkiri Kama Mwokozi Na Kisha Kumpokea Kama Wokovu Wako.
Unadhani Ni Kwa Nini Ni Muhimu Sana Kumkiri YESU?
Ni Kwa Sababu Katika YESU KRISTO Unakaa Utimilifu Wote Wa MUNGU Kwa Jinsi Ya Mwili(Wakolosai 2:9) Ndio Maana Agizo La MUNGU Kwa Sauti Lilisikika Live Mbele Ya Wanadamu Kwamba "Huyu Ndiye Mwanangu, Mpendwa Wangu, Ninayetendezwa Nae; Msikieni Yeye-Mathayo 17:5".
Ndugu Yangu Kumbe Usipomsikiliza Na Kumtii YESU KRISTO Hakika Hautakuwa Upande Wa MUNGU. Na Kama Wewe Hauko Upande Wa YESU Hakika Uko Upande Wa Shetani. Na Upande Wa Shetani Wanasubiri Jehanamu.

Ndugu Geuka Leo Na Mpokee YESU KRISTO Na Anza Kutii Neno Lake.
Ubarikiwe Sana Kwa Kuusoma Ukweli Na Kuuelewa Na Naimani Ukweli Huu Utaufanyia Kazi Njema Ya Kumpokea YESU.

                      Hasara za dhambi.

1. Jehanamu kwa asiyepata neema ya KRISTO.
Ufunuo 21:8 ''Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. '' 
 
2. Kukosa kibali cha MUNGU.
Mwanzo 4:7 ''Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.''
 
3. Kukosa baadhi ya Baraka za MUNGU.
Yeremia 5:25 ''Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.''
 
4. Shetani kukuonea sana maana ulinzi wa MUNGU unaondoka baada ya kufanya dhambi.
 1 Petro 5:8-9 ''Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. ''
 
6. Nguvu za MUNGU inaondoka kwako.
 Isaya 59:1-4 ''Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;  lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya. Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu. ''

Dhambi ni hatari sana hivyo ikimbie dhambi, ikatae dhambi, iepuke dhambi na usifanye dhambi tena.
 Mcheni BWANA enye watu wote. Mcheni mchana na usiku, asubuhi na jioni, alasiri na alfajiri.
Amelaaniwa Mwanadamu Yule Anayemtegemea Mwanadamu Mwenzake Kuwa Ndio Kinga Yake Na Huku Moyoni Mwake Amemwacha MUNGU.
Amelaaniwa Mwanadamu Yule Anayedhani Anaishi Kwa Sababu Tu Ya Chale Alizochanjwa Na Mganga Mwaka Jana.
Amelaaniwa Mwanadamu Yule Anayedhani Yuko Hai Leo Kwa Sababu Tu Ya Hirizi Kubwa Alilovaa Kiunoni,
Amelaaniwa Mwanadamu Yule Anayedhani Amepata Mke/mume Kwa Sababu Tu Alitembea Uchi Usiku Kwa Amri Ya Mganga.
Amelaaniwa Mtu Yule Anayedhani Kujipendekeza Kwake Kwa Wenye Mali Ndiko Kulikompa Uzima.
Ndugu, Mtegemee MUNGU Kwa Maombi Na Sio Kuwategemea Wanadamu. Bwana YESU Yuaja Ili Kumlipa Kila Mwanadamu Kama Matendo Yake Yalivyo.
Yeremia 17:5-8 '' BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. ''


Ndugu jitahidi sana haya yasikukute.
Haya hapa; Taarifa kuhusu huyu ndugu anayetarajia kuingia jehanamu muda mfupi ujao.
1. Alikataa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wake.
2. Alikuwa mtenda dhambi.
3. Alikataa kutubu na kuacha dhambi.
4. Alikuwa na roho ya kiburi.
5. Aliipenda dunia kuliko MUNGU.
6. Hakutaka kusikia habari za injili ikihubiriwa.
7. Alimwabudu shetani na maroho kutoka kuzimu akidhani anamwabudu MUNGU wa mbinguni.
8. Aliokoka kwa muda kisha akamwacha YESU na kurudi kwa shetani.
9. Hakumcha MUNGU na wala hakuishi maisha matakatifu.
10. Alikuwa anasema hakuna kuokoka ndio maana hakuokoka.
11. Alikuwa mzinzi, mwasherati, mwizi, muongo na mtumishi wa shetani.
12. Hakumhitaji ROHO MTAKATIFU na alimkataa.
Ndugu, chukulia huo ndio wasifu wa mtu anayejiandaa kuingia jehanamu na wasifu huo unasomwa siku ya mwisho huku jehanamu imeachama ili kummeza ndugu huyo.
Ndugu wakati huu ni wakati wa kumpokea YESU kwa upya kama ulikuwa unasuasua na kisha anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU.
Ni siku za mwisho hizi ndugu.
Nakushauri Okoka na acha dhambi, ogopa dhambi, ikimbie dhambi na usifanye dhambi tena.
Ufunuo 2:29 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa."

Naamini utatengeneza maisha yako kwa Bwana YESU KRISTO Leo 
 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments