USHUHUDA ULIOTENGENEZA WIMBO BORA.


USHUHUDA ULIOTENGENEZA WIMBO BORA.
 
Shalom Mteule wa MUNGU uliyeokolewa na Bwana YESU.
Karibu nikupe ushuhuda mfupi utakaokujenga kiimani.
Kuna Wimbo na wimbo huo ni maarufu sana na huwa unaimbwa kama Pambia makanisani, naamini hata wewe umewahi kuuimba;
 
Wimbo huo kwa ufupi unaimbwa hivi.
 
''Nimeamua kumfuata YESUUUUU,
Nimeamua kumfuata YESUUUUUU,
Nimeamua kumfuata YESUUUUUU,
Sitarudi nyuma kamweeeeeeeeeeeee.
Baba na Mama wakiniachaaaaa, Babu na Bibi wakiniachaaaaaa, Ndugu rafiki wakiniachaaaaaa, Sitarudi nyuma kamweeeeeeeeeeee.''

Wimbo huo huimbwa kwa namna nyingi na kwa maneno mengi ya kumpa MUNGU utukufu.
Unajua mtu wa kwanza kuuimba wimbo huo?
Kama hujui ngoja nikupe ushuhuda sasa.
Binti mmoja Mhindi raia wa India alikutana na injili ya YESU KRISTO na akaamua Kumpokea YESU KRISTO kama BWANA na Mwokozi wake.
Baada ya kuokoka wazazi wake walichukia sana sana. Baba yake akasema aachane na YESU la sivyo atamuua.
Binti alikuwa amekionja kipawa cha ROHO MTAKATIFU hivyo haikumsumbua hata kidogo, aliamua kuendelea na Mwokozi pekee wa wanadamu wote yaani Bwana YESU.
Baba yake alianza kumnyanyasa lakini hayo yote ni kama yalimuongezea imani kwa Bwana YESU.
Binti wakati huo ndipo alianza kuimba wimbo huo ambao alijikuta tu ameutunga kulingana na mazingira magumu aliyokuwa anakutana nayo.
Siku moja Baba yake na binti huyo alidhamilia kumwangamiza binti yake kwa sababu tu ameokoka.
Mzee yule alimfunga binti yake na kumpakia kwenye gari yake na kwenda naye Bandarini ili amtupe kwenye maji akiwa amefungwa. Yule mzee alilimfungia yule binti na kitu kama jiwe kubwa ili yule binti akitupwa ndani ya maji basi asielee bali afe kimya kimya na maiti yake iliwe tu na samaki ndani ya maji.
Chanzo cha yote hayo ni kwasababu yule Binti ameokoka.
Yule baba alipofika Bandarini eneo ambalo hakuona watu alimtupia binti yake ndani ya maji karibu kabisa na Winchi ya kupakulia mizigo bandarini.
Baada ya kufanya hivyo yule mzee alihakiki kama yule binti amezama na baada ya kujiridhisha aliwasha gari yake na kuondoka akijua kabisa amemuua binti yake.
Jambo la ajabu ni kwamba wakati binti anatumbukizwa baharini kuna mlinzi wa bandari alisikia kishindo cha maji na akaamua kufuatilia kwa kwa kaibu. Alipokaribia lile eneo alijua kabisa kuna kitu cha thamani kitakuwa kinataka kimetupwa mlo habarini karibu na eneo la kushushia mizigo katika bandari ile, yule mlinzi wa bandari akaamua kujirusha ndani ya maji ili ajue ni nini.
Jambo la ajabu alikutana na binti huyo kiajabu sana akaamua kumuokoa na kwa msaada wa wenzake wakamuokoa yule binti na kumpeleka Hospital. Baada ya siku kadhaa yule binti alirudi katika hali ya kawaida na kuwa mzima kabisa.
Binti yule aliamua kutorudi nyumbani kwao bali aliendelea na kazi ya MUNGU.
Baada ya muda mwingi kupita Yule binti akiwa katika jiji lile lile  siku moja alikutana uso kwa uso na Baba yake mzazi. 
Binti baada ya kumwona Baba yake alianza kulia sana sana.
Baba yake kwa mshangao sana akijikuta anasema hivi ''Kama nilikuua na huyo YESU  amekuponya basi na mimi naokoka''
Mzee Yule akampokea Bwana YESU kuwa Mwokozi wake tangu wakati huo na familia nzima wakaokoka.
Mwisho waushuhuda huu mfupi.
Nimukushuhudia kwa ufupi ndugu yangu ili usikubali kumwacha YESU kwa ajili ya chochote.
 Ndugu usikubali kumwacha YESU kwa sababu ya wazazi au ndugu.
Ndugu usikubali kumwacha YESU kwa ajili ya marafiki , familia, ukoo au kazi.
Bwana YESU ni zaidi ya vyote na zaidi ya wote.
Wokovu ni wako Binafsi ndugu hivyo usikubali kuuacha Wokovu wa KRISTO.
Kumbuka Ukimkataa Bwana YESU umeukataa uzima wa milele.
 
Yohana 3:17-21 ''Maana MUNGU hakumtuma Mwana(YESU) ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU.''

Tena Bwana YESU Mwenyewe anasema mambo muhimu sana kwako, Bwana YESU anasema '' Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona. ''
Kwa Lugha ya kiingeleza wimbo huu na waimbaji wengi akiwemo mwimbaji huyu Marisa

  Kwa lugha ya kiswahili pia kuna waimbaji wengi wameuimba wimbo huo, Mfano mmoja ni mwimbaji huyu.
MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa  ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka. Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments