HAKIKISHA UMEOKOKA NA UNAISHI MAISHA MATAKATIFU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu sana kujifunmza Neno la MUNGU.
Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yajayo yasiyoonekana kwa macho kwa sasa.
Waebrania 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."

Kwa kuamini na maombi katika jina la YESU KRISTO mtu anaweza kupata haki yake.
Warumi 10:10 "Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."
Kwa sababu imani chanzo chake ni kusikia basi zipo imani nyingi sana ambazo watu walizipokea kwa kusikia tu.
Nisikilize ndugu itakusaidia.
Kuna wenye haki( Waliookolewa na KRISTO) na kuna wasiohaki(Hawajaokolewa na KRISTO)
Wenye haki wana imani ambayo ni ya YESU KRISTO.
Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea(YESU) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."


Na kuna wasio haki ambao nao wana imani zao lakini hazitokanani na MUNGU na haziwapeleki uzima wa milele.
Ni kweli imani chanzo chake ni kusikia lakini imani ya kweli ni moja tu na hiyo chanzo chake ni kulisikia Neno la YESU KRISTO.
Warumi 10:17 "Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO."


Ndugu, imani zilizo kinyume na YESU KRISTO hazitakiwi kukuchanganya na ziko nyingi sana.
Imani zinazopinga Wokovu wa Bwana YESU hazitakiwi kukuchanganya maana zipo nyingi sana lakini baki katika imani pekee ya kweli ambayo ni Wokovu wa Bwana YESU.

Yuda 1:3-4 "Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu. Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya MUNGU wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu YESU KRISTO."

Ndugu baki katika imani ya Wokovu wa Bwana YESU na ishi maisha matakatifu.
Ukikubali mtu akuondoe kwenye Wokovu wa Bwana YESU maana ukimruhusu mtu huyo ujue amekuondoa wewe kwenye uzima wa milele.
Akikuondoa mtu katika Wokovu wa KRISTO tambua kwamba na jina lako limeondolewa kwenye kitabu cha uzima mbinguni.

Ndugu ishike imani ya Wokovu wa Bwana YESU maisha yako yote.
Ni imani hiyo pekee inayohusika na MUNGU aliye hai.
Ukiingia pia katika imani hii ya pekee ya uzima wa milele basi fuata mashariti ya imani hii.
Mashariti ya imani hii ni kuishi maisha ya Wokovu matakatifu, kuenenda katika ROHO MTAKATIFU na maombi.


Ndugu ni muhimu kujua kwamba Ingawa dunia inatamani sisi tuwe Upande wa Makristo na sio kuwa upande wa KRISTO.
 lakini ashukuriwe MUNGU maana sisi ni wakristo na hatuhusiki na makristo wa uongo.
Mathayo 24:24 ''Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. '
Wakristo kibiblia ni wale wenye KRISTO ndani yao.
Makristo ni wale watenda dhambi hata kama kanisani wanahudhuria kila wiki.
Makristo ni wale ambao ndani yao hakuna YESU KRISTO ila kuna sanamu.
Makristo ni wanaomwabudu Mariamu na wanadamu wengine.
Makristo ni wale manabii wa uongo wanaopotosha watu na kuwadanganya.
Makristo ni wale walioibadili Biblia ili iwasapoti wao.
Makristo ni wale ambao askofu wao feki wanamuita Mungu.
makristo ni wale ambao hudanganya watu kila Leo kwamba hakuna jehanamu ya moto maana MUNGU ni mwenye huruma sana.
Makristo ni wale hujiita wameokoka lakini miili yao haijaokoka, matendo na Tabia zao hazijaokoka.

Makristo Inawezekana kabisa wakawa wengi kuliko wakristo.
Ufunuo Wa Leo ni mgumu kwa baadhi ya watu lakini ndio ufunuo uliotoka mbingu za mbingu aliko Mkombozi YESU KRISTO.
Mwenye sikio la kusikia na asikie Leo.

WOKOVU ni muda huu wala sio kesho kutwa.
Bwana YESU alisema "Wateule ni wachache"
Mathayo 22:14 '' Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.'' 
Ndugu, ng'ang'ania kwenye hao wachache walio na KRISTO na wewe uwemo.
Wachache hao wanaweza kuwa ni zaidi ya watu bilioni 7 lakini Mtu mwingine asiwemo kwenye kundi hilo la wachache Kwa sababu tu amekataa kuokoka.

Nakubariki Kwa jina la YESU KRISTO wewe utakayebadilika Kwa kuanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu Wa KRISTO baada ya kujifunza Neno hili La ufunuo.
 Kuna watu wamefungwa na vitu vingi hata kufunguliwa kwao inakuwa mtihani. Kuna watu wamefunguliwa na vifungo vya dini hivyo inabidi kwanza wafunguliwe vifungo vya dini ndipo wafunguliwe na mengine.
 Ili upone unatakiwa umpe YESU nafasi, usipompa nafasi hutapona.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.''
   Watu wengi wakati wakitenda dhambi huona faida ni nyingi kuliko hasara juu ya uovu huo wanaoutenda. Lakini ukweli hakuna faida katika dhambi yeyote, ila kuna hasara nyingi sana kutokana na dhambi hiyo, na hasara kubwa zaidi ya dhambi hiyo ni jehanamu kama hakutakuwa na muda wa kutubu kwa mtu huyo.
1 Kor 6:9-10 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.''

Leo kuna watu wengi wa ajabu sana.
Kuna watu wako makanisani lakini bado wanazitumikia madhabahu za shetani za pombe.
Walevi wote waliojificha makansisani wamekariri andiko moja tu la 1 Timotheo 5:23 kama silaha yao kwa ajili ya kuhararisha ulevi.
Kiongozi wa kiroho anahararisha ulevi kwa kutumia andiko hilo.
Ngoja nifafanue kuhusu andiko hilo. 1 Timotheo 5:23 '' Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara. ''
-Timotheo anaambiwa kutumia mvinyo tena kidogo sana kwa ajili tu ya ugonjwa wa tumbo uliokuwa unamsumbua mara kwa mara.
Je wanaotumia andiko hilo kunywa pombe wanakuwa wanaumwa tumbo au?.
Ukisikia Mtu  kipofu wa kiroho ndio huyo.
Dawa ya Timotheo iliitwa mvinyo kwa lengo la kutibu tumbo na Paulo hakumaanisha kwamba Timotheo awe mnywa pombe kama walevi wa leo walivyo. Hata ukiamua kuwa mtu wa rohoni tu uatagundua kwamba pombe ni dhambi.
Na Paulo huyo huyo ndiye aliyekataza wateule kunywa mvinyo hivyo asingeweza kujipianga, soma Waefeso 5:18 ambapo Biblia inasema
'' Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe ROHO; ''
Paulo asingeweza kukataza pombe kwa baadhi tu ya watu, hivyo ukijichomeka katika andiko moja tu lenye agizo kwa mtu mmoja tu duniani utakuwa huna akili.

Wengine hudanganyana kwamba Bwana YESU aligeuza maji kuwa pombe kumbe ni maji yaligeuzwa kuwa juice maana hakuna hata mmoja aliyelewa katika harusi ya Kana.
Kama Divai ile nyingi vile ingekuwa Pombe si tungesikia watu wengi wakianza kuombewa ili wapone baada ya kupata majeraha yaliyosababishwa na pombe maana divai ilikuwa nyingi na tena tamu sio chungu kama pombe.

Jambo la muhimu kujua kwa kila mtu ni kwamba hata leo zipo juice nyingi za zinazotokana na zabibu/divai na sio pombe.
Ndizi ni nzuri lakini ndizi hiyo hiyo iliyoiva ukiiacha wiki 2 kisha ukaila utakuta imekuwa tofauti na inaweza ikawa na kazi tofauti na ndizi iliyiovaa kawaida maana kwa muda huu itakuwa imeoza, hata zabibu lazima tujue kwamba sio kila neno divai linamaanisha pombe. Kuna juice ya zabibu na kuna pombe pia, pombe ni dhambi.
Uwe na akili na usitende dhambi.
Kanisa hai la MUNGU halitakiwi kuwa na walevi.
Acha pombe ndugu na usikubali kuwa msindikizaji tu wa waenda mbinguni huku wewe unaenda jehanamu kwa sababu ya dhambi zako za siri.

 MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments