KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIA?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze ujumbe huu muhimu sana wa Neno la MUNGU.
Kwanini YESU KRISTO alikuja duniani?

Biblia ina majibu sahihi sana juu ya kwanini Bwana YESU alikuja duniani.
 
1. Luka 19:10 '' Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.''
 Wanadamu wote ili waokoke wanamhitaji  Bwana YESU tu.
Yeye alikuja kwa ajili ya wenye dhambi ili sasa kupitia yeye waokolewe na kuanza kuishi maisha matakatifu yanayoagizwa na Neno la MUNGU.
Kila asiye na YESU amepotea na anatakiwa kumpokea Bwana YESU mwenye uwezo pekee wa kuwaokoa waliokuwa wamepotea.
Ukikubali kuokolewa na Bwana YESU hakika wewe umeufuata mpango wa MUNGU wa uzima.

2. 1 Yohana 38B '' Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi ''
 Kazi za shetani zinaweza kuvunjwa na jina la YESU KRISTO tu pamoja na damu yake.
Kuna kazi nyingi za shetani zinatesa wanadamu alio wengi.
Njia ya kupona ni kumfuata Bwana YESU maana yeye alikuja ili kuzivunja kazi zote za shetani.
Chochote kile cha kipepo ambacho kinamtesa mtu yeyote hakika mtu huyo akimkimbilia Bwana YESU hakika atafunguliwa na kuwa huru mbali na mateso hayo ya wachawi, wakuu wa giza, washirikina, majini na kila mawakala wa shetani.

3. Yohana 10:10B ''mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. ''
 Bwana YESU alikuja ili tuwe na uzima wa milele.
Kumpokea YESU kama Mwokozi, kutubu  na kisha kuanza kuishi maisha matakatifu katika yeye hakika  ni kujihakikishia uzima wa milele.

Kwa maandiko hayo basi tunajifunza kwamba;
1. YESU alikuja kumuokoa mwanadamu.
2. YESU alikuja ili ili kuharibu kazi zote za shetani kwa wanadamu
3. Alikuja ili atupe uzima sasa na uzima wa milele.

Kazi yetu ni kumpokea tu na kumtii ili atimize yote hayo.
Yohana 3:16-18 ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee(YESU), ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.''
Jitahidi Kujituma Katika Chochote Kinacholeta Baraka Kwa Kanisa La KRISTO.
MUNGU ni mwenye haki na ni mtakatifu.
Tukitaka tumpendeze MUNGU ni lazima tuipende haki na tuuishi utakatifu katika Wokovu.
.
Wengine hmpokea YES lakini baada ya muda huiacha njia pekee ya uzima wa milele kwa ajili ya mambo ya kidunia.

Bakushauri Ndugu kwamba  Usimwache YESU Kwa Ajili Ya Mwanaume Au Mwanamke.
Kaka Usimwache YESU Kwa Ajili Ya Binti.
Dada Usimwache YESU Kwa Ajili Ya Mwanaume. Kumbuka Uhusiano Wako Na Mwanaume/Mwanamke Huyo Utaishia Duniani Tu, Lakini Ukimtii KRISTO Na Neno Lake Uhusiano Wako Na KRISTO Utakuwa Wa Milele. Usione Kubadili Dini Kwa Kumwacha YESU Kuwa Ni Jambo Jema Bali Ni Kwa Kujiangamiza Mwenyewe. Kumbuka Nje Na YESU Hakuna Uzima Wa Milele, Chunga Usikose Uzima Wa Milele.
Nakuomba ufikiri nilisemalo maana sijalisema kwa akili zangu tu Bali nimeambiwa nikuambie ili kwa neema ya MUNGU usimwache YESU.
Kumbuka ulipompokea YESU kama Mwokozi wako ndio siku pia makazi yako yalianza kuandaliwa mbinguni.
Kumbuka Neno hili la Bwana YESU "Yohana 14:2-3 " Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo."

Sasa unapomwacha Bwana YESU unakuwa pia umeyaacha makazi yako ya mbinguni, na ukijitenga na makazi yako ya mbinguni unakuwa umejichagulia jehanamu.
Ndugu nakuomba sana usikubali kumwacha YESU KRISTO kwa vyovyote.
Usimwache YESU ili upate ndoa na baada ya ndoa hiyo uende jehanamu.
Ndugu usimwache YESU kwa ajili ya mwanamke au mwanaume.
Wanakuambia dini ni dini tu wanakudanganya ili uende motoni.
Ni heri usipate mume/mke ila uende Uzima wa milele na KRISTO kuliko kupata make/mume lakini kisha uende jehanamu.
Wanaojitenga na Wokovu wa KRISTO hakika wanajitenga pia na mbingu.
Wanaomkataa YESU hakika wanamkataa MUNGU.
Wanaomkataa YESU hakika wanaukataa uzima wa milele.
Ndugu nakusihi sana sana usimwache YESU kwa ajili ya mwanamke au mwanaume.
Yohana 3:17-19 " Maana MUNGU hakumtuma Mwana(YESU) ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu."

Ndugu nakuonya.
Wewe unayehusika nakuomba tengeneza maisha yako na Bwana YESU.
Kama ulimwasi Bwana YESU ili upate mume au mke nakuomba tubu na rejea kwa YESU Leo maana neema bado ipo.
Wewe unayetaka kumwacha YESU ili upate mke au mume nakuomba acha mpango huo hatari na wa kukuangamiza.

Matendo 4:12 '' Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ''

Alama ya Mteule wa MUNGU ni utakatifu.
Alama hiyo unatakiwa kuitunza sana.

Ndugu itunze alama yako.
Kama mteule wa MUNGU uliyeokolewa na Bwana YESU hakikisha unaitunza alama yako.
Alama ya wateule wa MUNGU wote ni utakatifu.
Ndugu mteule itunze alama yako.
Itunze kwa kulitii neno la MUNGU.
Itunze alama yako kwa kudumu katika fundisho ya Neno la KRISTO.
Itunze alama yako kwa kuenda kwa ROHO MTAKATIFU.
Ndugu mteule wa KRISTO hakikisha unaitunza alama yako ambayo ni utakatifu.
1 Petro 1:15-16 "bali kama yeye(YESU) aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi(MUNGU) ni mtakatifu."

Kwa kuongezea ni kwamba hapa chini ni alama za mteule wa MUNGU lakini kiini ni utakatifu katika KRISTO.
Alama za mteule wa MUNGU.
1. Kuishi maisha matakatifu.
2. Kumtii MUNGU katika yote.
3. Kuenenda katika ROHO MTAKATIFU.
4. Kulitumia kwa haki Neno la MUNGU.
5. Kuwa na upendo wa MUNGU.


Vipo vitu tunaweza sisi wenyewe lakini vipo vingine vinamhitaji MUNGU ndiye atushindie.
Kuna vitu haviwezekani mpaka umwite Bwana YESU akushindie.

Maombi ni ya muhimu sana ili ushinde.

Parapanda Italia siku ya mwisho.
Wateule Watakua Wamenyakuliwa Kwenda Kumlaki Bwana YESU Mawinguni, Chini Watabaki Walevi, Wazinzi, Waasherati, Majambazi, Waongo, Waabudu Sanamu, Wachawi, Waganga Wa Kienyeji, Mashoga, Freemason, Matapeli, Wanaomkataa YESU Leo Na Watenda Dhambi zingine zote na Wote ambao hawakutubu na kuacha dhambi zao.

Ndugu Yangu Hata Kama Umefanya Dhambi Zote Nilizotaja Hapo Juu na hata zingine zozote Ukimpokea Bwana YESU Leo Atakusamehe Na Utajumuika Na Wateule Kama Ukidumu Katika Utakatifu.
YESU Anakuhitaji Sana Kuliko Wanavyokuhitaji Wanadamu Wote, Amua Tu Leo Kumpokea Ili Awe BWANA Na MWOKOZI Wa Maisha Yako,
 1 Petro 1:14-17 ''
Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba, yeye(MUNGU) ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. '

MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments