MAOMBI YA KUFUTA MAZUIO YA KIPEPO YOTE DHIDI YAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe milele ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU kisha tuombe maombi ya ushindi.
Neno zuio linatokana na neno zuia ambalo tunaweza kusema   kuzuiliwa au kuzuilika.
Neno zuia lina maana ya kuzuiliwa kuendelea mbele.
Neno zuia lina maana ya kusimamisha jambo fulani lililokuwa linaendelea na sasa lisiendelee.
Neno zuia lina maana na kukomeshwa jambo ambalo lilikuwa linaendelea na sasa kwa sababu ya nguvu fulani jambo hilo linakoma.
Neno zuia lina maana ya kupinga jambo fulani lisiendelee.
Neno zuia lina maana ya kukataza kitu fulani kisifanyike au kisiendelee.
Zuio la kipepo ni mambo yote mazuri kwako ambayo yamezuiliwa kichawi ili usiyapate hata kama ni haki yako.
Mara nyingine mawakala wa shetani huweka zuia mapema kabisa kwa mtu wa MUNGU.
Walio wengi tunaokoka tukiwa wakubwa  na hadi tunaokoka unakuta shetani alishaweka mazuio ya kipepo mengi kutuhusu.
Baada ya maana hiyo ya zuia au zuio nakuomba sana ujue maana hizo za zuia ili pale mawakala wa shetani wamekuzuia basi uombe maombi ya kushinda hata kama walikuzuia.
Wapo Watu wamezuiliwa kipepo kupata baraka fulani katika maisha yao.
Wapo watu wamesimamishwa kipepo ili wasiendelee katika baraka zao mbalimbali au hali zao.
Kuna vitu vinaweza kukomeshwa kwako kipepo kabisa na hujui ufanyeje.
Unaweza ukapingwa kipepo kufanya kitu fulani chema kabisa na hujui ufanyeje.
 Unaweza ukakatazwa kipepo kufanikiwa katika jambo fulani maishani mwako.
Shetani huwa anaondolewa kwa nguvu na sio kubembelezwa.
Maombi ya vita kwa kutumia mamlaka ya jina la YESU KRISTO kama ya leo ni muhimu sana ili usizuilike tena.
Unaweza ukazuiwa kipepo hata kwa jambo lolote tu jema na wala usilaumu bali mwite MUNGU aliye hai mbinguni ili akushindie.
Hebu ona mfano huu ambao Nabii Danieli aliundiwa zengwe na wanaotumika kipepo ili tu asimuombe MUNGU wa mbinguni na ili tu ajumuike na wao katika kuabudu sanamu, lakini kwa Danieli muombaji na anayejua nguvu za maombi hakika alishinda.

Danieli 6:4-24 '' Basi wale mawaziri na maamiri wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia hivi, Mfalme Dario, uishi milele.  Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu ye yote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.  Sasa, Ee mfalme, piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyoweza kubadilika. Basi mfalme Dario akayatia sahihi maandiko yale, na ile marufuku. Hata Danielii, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za MUNGU wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Basi watu hao wakakusanyika pamoja, wakamwona Danielii akiomba dua, na kusihi mbele za MUNGU wake. Ndipo wakakaribia, wakasema mbele ya mfalme katika habari ya ile marufuku ya mfalme; Je! Hukuitia sahihi ile marufuku, ya kwamba kila mtu atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, akasema, Neno hili ni kweli, kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika. Basi wakajibu, wakasema mbele ya mfalme, Yule Danielii, aliye mmoja wa wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoitia sahihi, bali aomba dua mara tatu kila siku. Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danielii; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa. Ndipo watu wale wakakusanyika pamoja mbele ya mfalme, wakamwambia mfalme, Ee mfalme, ujue ya kuwa ni sheria ya Wamedi na Waajemi, lisibadilike neno lo lote lililo marufuku, wala amri yo yote iliyowekwa na mfalme. Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danielii, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danielii, MUNGU wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya. Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danielii. Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa. Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba. Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa MUNGU aliye hai, je! MUNGU wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa? Ndipo Danielii akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele. MUNGU wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danielii katika lile tundu. Ndipo Danielii akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini MUNGU wake. Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danielii, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.''

 Habari hizi za danieli ni mfano hai kwetu kwamba mawakala wa shetani hupanga mipango ya kutuzuia katika vitu vyetu vyema.
Kwa Danieli tunaona walifanya hila na kupitisha sheria ya dharula katika taifa ili tu kumnasa mtu mmoja Danieli. Katika maandiko hayo tunajifunza kwamba Danieli alizuiliwa katika mambo yafuatayo.

1. Alizuiliwa kumwomba na kumwabudu MUNGU, Je wewe unazuiliwa katika nini?

2. Danieli alizuiliwa kuishi, ndio maana wakamtupa katika shimo lenye simba ili simba wamuue, Je wewe mawakala wa shetani wamekuletea ugonjwa gani ili ufe?
Kwa jina la YESU KRISTO leo unaweza kuzuia kifo hicho kilichopangwa kipepo.
Kuondoka duniani tutaondoka tu lakini kwa mpango wa MUNGU na sio kwa mpango wa wachawi au mawakala wengine wa shetani, ndugu kataa kuteswa na wakuu wa giza.

3. Danieli alizuiliwa kufanya kazi zake, ndio maaana alikamatwa na kuwekwa kifungoni yaani kutupwa ndani ya shimo. Wewe je ni nani amekuzuia kipepo ili usipate kazi? Ni nani amefanya miundombinu ya kipepo ili ufukuzwe kazi au usimamishwe kazi?
Ni nani ambaye amefanya hila zake ili japokuwa una kazi lakini usipate faida hata moja kutoka katika kazi hiyo?
Ndugu unahitjai kumcha MUNGU na kufuata kanuni zake zote na hakikisha unafunguliwa.

4. Danieli alizuiliwa kuipata furaha ya familia yake, ndio maana alikamatwa na kutengwa mbali na familia yake.
Wewe je ni nani amekuzuia kuipata furaha ya familia yako au ndoa yako?
Leo kuna ushindi katika jina la YESU KRISTO kwa maombi ya imani katika yeye.

5. Danieli alizuiliwa kupata chakula ndio maana aliwekwa kifungoni.
Je wewe ni nani amekuzuia kupata kipato kizuri kinachokufanya uwe na maisha mazuri?
Leo ndugu nakuomba uombe.
Zuio la kipepo ni la kulivunja kwa maombi katika jina la YESU KRISTO.
Wapo watu shetani amewawekea zuio la kupata baraka zao tangu wako tumboni mwa mama zao.
Wako watu wamefungwa kipepo tangu wakiwa watoto wachanga.
Ndugu, wewe ndio unajua ni katika baraka yako ipi kuna zuio la shetani ili usiipate baraka hiyo.
Leo futa mazuio yote ya kipepo na wewe hao waliokuzuia wawekee kizuizi cha damu ya YESU KRISTO ili wasikuzuie tena milele.
Elisha aliomba maombi kwamba madui zake wapigwe upofu, wewe hao wanaokuzuia unaombaje kuwahusu?

2 Wafalme 6:18 '' Na walipomtelemkia Elisha akamwomba BWANA, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.''

 Na wewe ndugu wapige upofu wote waliokuzuia kichawi kupata kazi, kupandishwa cheo,Kufunga ndoa,kufaulu mitihani au kupata biashara nzuri n.k
Kama waliweka zuio la kukuzuia leo futa hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO aliye hai.
Na kisha wawekee wao kizuizi cha kutokuigusa baraka yako.
Usikubali mtu akuendee kwa mganga ili kukuzuia usiipate baraka yako uitakayo.
Jambo lingine naomba ufahamu ni kwamba wakati mwingine zuio linalokutesa linaweza lisitokane tu na mawakala wa shetani bali likatokana na wewe.
Kuna mazuio mengine umeyasababisha wewe kwa kutenda dhambi.
Dhambi inaweza kuwa chanzo cha zuio lako. Kuwa mbali na ibada na kuwa mbali na Wokovu wa Bwana YESU kunaweza kutengeneza zuio kwako.
Kudharau mambo ya MUNGU na kutokuishi maisha matakatifu kunaweza kutengeneza mazuio kwako, unahitaji kuwa makini sana sana.
Yeremia 5:25 ''Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.''

 Maovu yako yanaweza kukuzuiliwa Mema aliyotaka kukupa MUNGU Muumba wako.
Kama ni wewe umejizuia kwa kufanya maovu basi hakikisha unatubu na kumrudia Bwana YESU kwa usahihi na toba yako ya kweli itayafuta mazuio yote yaliyotokana na dhambi zako.
Baada ya hapo anza sasa kupambana na mawakala wa shetani waliokuzuia kipepo, zingatia hayo itakusaidia sana.

Utajuaje kama kuna zuio la kipepo katika maeneo fulani ya maisha yako?

1. Unafanikiwa katika mambo mengine tu lakini hilo ulilozuiliwa kipepo kila ukijaribu  hufanikiwi.

2. Kila ukijaribu kuipata baraka hiyo inakukimbia au kuipata ni hadi utumie nguvu kupita kiasi na hata ikipatikana ni kwa muda mfupi sana inatoweka.

3. Kupata vita kali sana kila ukijaribu kuipata baraka hiyo.
Vita hiyo inatoka kwa watu wa karibu yako au ndugu na au vita kutoka nguvu za giza.

4. Kujulishwa na ROHO MTAKATIFU kwamba kuna zuio.
ROHO wa MUNGU anaweza kukujulisha kwa ndoto, maono, Neno au ufunuo.

5. Ufahamu wako kuhamishwa  kila ukipanga mipango ya kuipata baraka hiyo.
Unaweza ukapanga mipango yako kwa mwaka mpya ulioingia lakini baada ya mwezi unasahau na hadi mwaka unaisha hujatekeleza hata jambo moja katika mipango hiyo.

Leo ondoa mazuio yote ya kipepo katika baraka zote zinazokuhusu. Kumbuka Bwana YESU alikuja ili akushindie dhidi ya nguvu za giza zote, hakikisha tu uko upande wake Mwokozi wa milele.
1 Yohana 3:8b ''Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.''
Omba leo ndugu na kuna ushindi mkuu kupitia jina la YESUKRISTO.
Yohana 14:13 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba(MUNGU) atukuzwe ndani ya Mwana(YESU). ''

 Leo kuna ushindi ndugu kama ukiomba katika jina la YESU KRISTO.
''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake(MUNGU), ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.-1 Yohana 5:14-15''

 Jitahidi tu kujua ni katika eneo gani maadui wamekuzuia kiroho ili usifanikiwe.
Futa zuio la kipepo kwenye ardhi, futa zuio la kipepo kwenye ukoo, kabila, mji uliopo au familia.
Jitenge na kila mpango wa shetani wa kukuzuia kupata baraka zako halali kutoka kwa MUNGU.
Kataa dhambi ili isiwe kikwazo kwako.
Kuna mambo mengi tu kwako huu ni wakati wake lakini shetani amekuzuia kuyapokea na wewe unajipa moyo tu kwa baraka hizo bado muda wake, kumbe muda wake ulishafika siku nyingi.
Shetani anaweza akafunga ufahamu wako hata ukawa unadhani kwamba hizo baraka zako sio kwa wakati huu.
Leo omba maombi yafuatayo;
1. Futa mazuio yote ya kipepo yaliyowekwa kwenye ulimwengu wa roho kukuzuia.
2. Baada kufuta mazuio ya kipepo weka wewe zuio la MUNGU ili maadui zako washindwe kugusa baraka zako.

MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu na  kama ukipenda kunisapoti katika huduma yangu kwa sadaka ya hiari ya kiwango chochote utakachopenda karibu na MUNGU akubariki sana, pia kitabu cha MAOMBI YA KINA kipo na wasiliana nami utakipata na ukifanyia kazi itakusaidia sana.
Hapa chini ni maombi ya kufuta mazuio ya  kipepo na kisha wewe kuweka kizuizi cha MUNGU.
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake.
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini.


 MAOMBI YA KUFUTA ZUIO LA KIPEPO.

JEHOVAH MUNGU uliye hai ninakuabudu na kukutukuza MUNGU muumbaji wangu.
Nalibariki jina lako BWANA maana wewe u mwema kwangu.
Nalitukuza jina lako maana wewe u mwema kwangu.
Naomba unisamehe na kunitakasa dhambi zangu zote. Nifanye sasa niishi maisha safi ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi wangu.
Ninakuja mbele zako MUNGU wa uzima nikiomba mazuio ya kipepo yote yaliyonizuia katika maisha yangu yafutike leo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Kila adui aliyenizuia kupata kazi, nafuta zuio hilo na sasa kwa jina la YESU KRISTO naenda kupata kazi nzuri.
Kila wakala wa shetani aliyenizuia kipepo ili nisipate Mchumba na ili nisifunge ndoa, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kichawi katika biashara, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mchawi anayenizuia kupona magonjwa sasa napona kwa jina la YESU KRISTO na zuio la kichawi la kunizuia kupona linafutika muda huu katika jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kipepo katika kupata uzao, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kipepo katika kupanda cheo, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kipepo ili nisimwabudu MUNGU BABA kwa uhuru,ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kichwawi ili nisipendwe katika ndoa yangu, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kishetani ili nisipate haki zangu, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kipepo ili nisiendelee, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Aliyenizuia kichawi ili biashara yangu isikue na kunipa faida, ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Kila aliyenizuia kipepo katika jambo lolote katika maisha yangu,
ninafuta hilo zuio kwa damu ya YESU KRISTO na sasa naenda kufanikiwa kwa jina la YESU KRISTO.
Kuanzia leo mimi sitazuiliwa na mganga wala mchawi katika jambo lolote.
Kila aliyenipinga kipepo na kila aliyenikataza kupata baraka yangu, leo nafuta mazuio yake kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Bwana YESU nishindie Mwokozi wangu.
Neno la MUNGU linasema katika Mithali 3:26 kwamba '' Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.'' 
Kuanzia sasa sitanaswa tena na zuio la kipepo.
Kuanzia sasa mtu akiniendea mimi kwa mganga wa kienyeji ili kunifunga kipepo au kunizuia atazuiliwa yeye katika hayo aliyokusudia maana mimi nimemtegemea MUNGU Baba katika jina la YESU KRISTO.
Neno la MUNGU linasema katika Zaburi 91:10 kwamba ''Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.''
Hivyo kuanzia leo katika jina la YESU KRISTO neno hilo litimie na mabaya yote yaliyokusudiwa sasa hayatanipata kamwe, katika jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ee BABA wa mbinguni ninaomba sasa kwa neema yako ''Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.'' Kama Neno lako MUNGU linavyosema katika Zaburi 71:13.
Naweka kizuizi katika ulimwengu wa roho kwa jina la YESU KRISTO hakuna adui yeyote atanizuia.
Ninawazuia maadui wote kuigusa fursa yangu wala baraka yangu kutoka kwa MUNGU.
Wanaoiwazia mabaya ndoa yangu au biashara yangu sasa hawataiweza kwa jina la YESU KRISTO.
Asante MUNGU uliyeniumba maana umeuleta ushindi wangu katika jina la YESU KRISTO.
Ninakushukuru na kukutukuza Mfalme wa mbinguni.
Katika jina la YESU KRISTO Nimeomba na kupokea ushindi mkuu.
Amen Amen Ameeeeen.

 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.

0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.


Comments