UNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YAKO YA WOKOVU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Hili ndio somo langu la 700 tangu nimeanza kufundisha mtandaoni mwishoni mwaka mwaka 2012.

ROHO MTAKATIFU ni ahadi ya MUNGU kwa wote waliookolewa na Bwana YESU.

Matendo 5:32 "Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na ROHO MTAKATIFU ambaye MUNGU amewapa wote wamtiio."


Ahadi hii ya kipekee sana kutoka kwa MUNGU inampasa kila mteule awe nayo.
Kanisa la MUNGU ni lazima sana lienende katika ROHO MTAKATIFU
Ndipo litampendeza MUNGU.
Kanisa ni Mimi na wewe tuliokolewa na Bwana YESU.
ROHO MTAKATIFU ndiye anayelishikilia Kanisa la MUNGU.
Kanisa bila ROHO MTAKATIFU sio kanisa tena.
Kazi za Huduma zote ili zifanye kazi zinamhitaji ROHO MTAKATIFU.
Maisha ya kumpendeza MUNGU yako pekee katika ROHO MTAKATIFU.
Kanisa ni watu na sio jengo hivyo wewe kanisa inakupasa sana kumshikiria ROHO MTAKATIFU.
ROHO MTAKATIFU kwa kupitia Neno la MUNGU ndiye anayeweza kuufanya utu wako wa ndani kumpendeza MUNGU.
Ni hatari sana kuishi bila ROHO MTAKATIFU.
Ukiishi bila ROHO MTAKATIFU mtakatifu au ukiishi na ROHO MTAKATIFU lakini usikubali kumtii wala kuongozwa naye hakika kuna mambo utafanya na usijue kama ni machukizo kwa MUNGU.
Ni lazima sana kanisa la MUNGU limshikilie sana ROHO MTAKATIFU.
ROHO MTAKATIFU ni ahadi ya MUNGU kwa wateule wote waliotakaswa kwa damu ya thamani sana ya YESU KRISTO Mwokozi.


Matendo 2:38-28 'Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana MUNGU wetu wamjie."


Kila aliye kanisa la MUNGU inampasa kumhitaji sana ROHO MTAKATIFU katika maisha yake yote.
Bila ROHO MTAKATIFU huwezi kushinda dunia na mambo yake.
Ndugu hakikisha una ROHO MTAKATIFU na mshikilie huyo daima.


Wagalatia 5:25 " Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO."


ROHO MTAKATIFU ni zawadi ya MUNGU kwetu.
Zawadi hutunzwa na kuthaminiwa.
Zawadi ni kitu atunukiwacho MUNGU kwa sababu ya upendo wa mtoaji wa hiyo zawadi.
MUNGU kwa hakika anatupenda upeo.
MUNGU ana upendo wa agape kwetu.
Kwanza MUNGU alitupenda na akachagua kutuletea Mwokozi wa roho zetu YESU KRISTO.


Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee(YESU), ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."
 
Ni upendo wa ajabu sana wa MUNGU kwetu, kazi yetu ni kumpokea tu Mwana wa MUNGU kama Bwana na Mwokozi wetu kisha tunamtii na kuliishi Neno lake.
Upendo wa MUNGU haukuishia hapo tu Bali kwa waliomchagua YESU KRISTO kama Mwokozi MUNGU ametuongezea na ROHO MTAKATIFU kwa upendo wa kipekee mno mno.
Bwana YESU alithibitisha hayo katika andiko hili.


Yohana 14:26 "Lakini huyo Msaidizi, huyo ROHO MTAKATIFU, ambaye Baba(MUNGU) atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia."


ROHO MTAKATIFU ni lazima apewe nafasi kuu sana katika kanisa la MUNGU.
Ndugu kama uko dhehebu au Kanisa wanaofundisha mafundisho ya kumtaa ROHO MTAKATIFU hakika hilo dhehebu au kanisa halitokani na MUNGU.
Ushauri wangu kama uko katika dhehebu la jinsi hiyo hama haraka sana maana dhehebu hilo halitokani na MUNGU.
Nafasi ya ROHO MTAKATIFU katika kanisa ni muhimu Sana Sana na ya thamani sana.
Ndugu Yangu uliyeokoka nisikilize itakusaidia.
Kama ilivyokuwa rahisi kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako basi hakikisha inakuwa rahisi pia kumpokea ROHO MTAKATIFU ili akuongoze katika kweli ya KRISTO na MUNGU.
Ni lazima uhakikishe ROHO MTAKATIFU anakaa katika maisha yako yote baada ya wewe kuokoka.
Bwana YESU anasema "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.-Yohana 14:14-17


ROHO MTAKATIFU ni wa muhimu sana katika maisha yako.
Mpe nafasi ya kwanza ROHO MTAKATIFU baada ya wewe kumpokea Bwana YESU.
Kumbuka ROHO MTAKATIFU hajilazimishi kuwa kwa mtu yeyote Bali anaingia ndani ya wenye kitu ya kumpokea.
ROHO MTAKATIFU anawahitaji wenye kiu ya haki.
Hata MUNGU halazimishi watu kumwabudu katika Roho na kweli ila wenye kiu ya haki kumwabudu katika Roho na kweli.
ROHO MTAKATIFU hutusaidia kumwabudu MUNGU katika kweli yake yote.


Yohana 7:37-39 "Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, YESU akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Na neno hilo alilisema katika habari ya ROHO, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana ROHO alikuwa hajaja, kwa sababu YESU alikuwa hajatukuzwa."
Ndugu unamhitaji sana sana ROHO MTAKATIFU maana bila yeye huwezi kushinda mambo ya dunia.
Kumbuka Neno la MUNGU linavyosema,
Warumi 8:9-14 " Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake. Na KRISTO akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa ROHO yake yeye aliyemfufua YESU katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua KRISTO YESU katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa ROHO wake anayekaa ndani yenu. Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa ROHO, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."


MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments