EWE ROHO UNAYEISHI KATIKA MWILI NISIKILIZE KWA MAKINI SANA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Mwanadamu Ni roho Anayeishi Katika MwilI.
 Mwili Ni Chombo Tu Kilichombeba Mwanadamu Ambaye Ni roho. Mwili Utabaki Hapo Ila Mwanadamu Ambaye Ni roho Ataondoka Na Kuvaa Mwili Mwingine Tayari Kwa Kwenda Uzimani Kama Alishi Maisha Matakatifu Katika KRISTO, Au Kwenda Ziwa La Moto Kama Alimkataa KRISTO Na Utakatifu. 
 Biblia Iko Wazi Katika Ezekieli 18:20 Ikisema roho Itendayo Dhambi Ndio Itakayokufa Yaani Ndio Itakayoenda Jehanamu. Biblia Haijasema Mwili Utendao Dhambi Ndio Utakaokufa Bali roho Itendayo Dhambi. 
 Ezekieli 18:20-24 '' Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa. Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi. Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi? Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa.''

Roho itendayo dhambi ndio itaenda jehanamu, lakini MUNGU ameileta neema yake leo. Neema ya MUNGU ni watu wampokee YESU KRISTO kama Mwokozi, Kisha kutubu na kuacha uovu hakika hao watasamehewe na wala dhambi zao Hazitakumbukwa  tena.
Ndugu unahitjai kujua mwisho wa watenda dhambi kuwa ni jehanamu.
Ndugu unahitaji kujua kwamba wateule wa KRISTO watakatifu wataurithi ufalme wa MUNGU.
Ewe roho unayeishi katika mwili hakikisha unamcha MUNGU.
Zaburi 34:14 ''Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.'' 

Ndugu, umetenda dhambi sana na hukufaidika na lolote hata moja, nakusihi sasa mpokee Bwana YESU na anza kuishi  maisha matakatifu katika yeye Mwokozi wa pekee.
Wewe ni roho anayeishi katika mwili hivyo jua kwamba mwili wako huu  uatenda kaburini na kuoza na kufutika lakini wewe ambaye ni roho utavaa mwili mpya na kwenda sehemu uliyoichagua.
Sehemu ambazo mwanadamu anaweza kuchagua kwenda baada ya kufa ni mbili tu yaani Uzima wa milele au jehanamu.
Kumbuka Biblia inasema hivi ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;-Waebrania 9:27 '
Mtenda dhambi yeyote akiondoka duniani leo anaelekea kuzimu akisubiri siku ya mwisho ili aingie jehanamu.
MUNGU Baba anasema ''Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa MUNGU wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.-Ufunuo 21:6-8''

Kama umeokoka sasa na unaishi maisha matakatifu hakika ukiondoka duniani hata leo hii unaenda Paradiso ya mbinguni ukisubiria tu uzima wa milele usiokoma wala kuisha.
Ndugu yangu, wewe ni roho anayeishi katika mwili hivyo usitii matendo ya mwili ambayo ni machukizo kwa MUNGU.
1 Kor 6:9-10 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.'
Ndugu, ni heri kufanyika mtakatifu kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako, kutubu na kuacha dhambi zote.
Usidhani kwamba wewe utaingia kaburini, hapana, mwili wako tu ndio utaingia kaburini na wakati huo wewe utakuwa ama mbinguni au kuzimu, unahitaji kuwa makini sana.
Watakatifu wote wako mbinguni leo, wale waliookoka na kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU. 
Ndio Maana Watakatifu kama Akina Yohana Mbatizaji Waliokatwa Vichwa Leo Wako Mbinguni Wakiwa Na Miili Mipya Isiyo Na Makovu Wala Alama Za Panga, Akina Stephano Waliopigwa Mawe Na Kupata Majeraha Na Manundu Leo Wako Mbinguni Wakiwa Hawana Kovu Hata Moja. Ndugu Okoka Leo Maana Kwa Njia Hiyo Utaiponya roho Yako.
Bwana YESU alikuja duniani maalumu kabisa kwa ajili yako ili tu uokoke na kuishi maisha matakatifu.
Bwana YESU alikuja kukutafuta ndugu ''Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.-Luka 19:10 ''
 Kuokoka Ni Kuuchagua Uzima Wa Milele. 
Kuishi Maisha Matakatifu Ndani Ya KRISTO Ni Kama Kutanguliza Mali Zako Zote  Uzima Wa Milele. Kuishi Maisha Matakatifu Ni Kama Kujitanguliza Mwenyewe Uzima Wa Milele, Imebaki Huku Roho Yako Tu, Siku Ukiondoka Huku Roho Yako Itaenda Uzima Wa Milele.
Bwana YESU anasema ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.-Mathayo 11:28 ''

 Ndugu unahitaji kufanyika mteule wa MUNGU halisi na asiye na mawaa.
Unahitaji kuwa mtu wa maombi na unahitaji kumtumikia MUNGU katika injili ya Wokovu wa KRISTO YESU Mwokozi.
Kuna Watu Huweka Bajeti Za Magonjwa Kila Wakipata Mishahara Au Vipato. shetani Kwa Njia Hiyo Hiyo Huwaongezea Magonjwa Ili Bajeti Zao Kwa Magonjwa Ziongezeke. Na Ajabu Bajeti Za Ugonjwa Hazijawahi Kuwatosheleza Watu Hawa. Ndugu Zangu, Magonjwa Ni Mali Ya shetani Lakini Tukimwita Bwana  YESU Atazihamisha Mali Za shetani Zote Ili Zitoke Ndani Yako. Nakushauri Wewe Unayeweka Bajeti Kwa Magonjwa Hamishia Bajeti Hiyo Kwenye Injili Ya KRISTO Maana Magonjwa Yote Yataondoka Ndani Yako. Sapoti Kazi Ya MUNGU Na Sio Kusapoti Magonjwa. Kama Hujaokoka Nakusihi Sana Uokoke Leo Maana Kuokoka Ni Kuuchagua Uzima Wa Milele.
Ndio maana Bwana YESU anasema ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.-Mathayo 11:28 ''
 Shetani Anawabebesha Watu Mizigo Mingi. 
Kuna Watu Wamebebeshwa Magonjwa, Wengine Wamebebeshwa Mizimu, Wengine Wamebebeshwa Mapepo, Wengine Wamebebeshwa Kiburi, Wengine Utasa, Wengine Dhambi N.k. Habari Njema Ni Kwamba Bwana YESU Ana Uwezo Wa Kuwatua Wanadamu Wote Hiyo Mizigo Inayowatesa kama Neno lake linavyosema katika Mathayo 11:28
Ndugu Yangu, Ukimpokea YESU Leo Mizigo Yako Itaondolewa Kwako Na Kupelekwa Golgotha, Huku Wewe Ukibaki Huru.
Ndugu unahitaji nini zaidi?
Nakuomba hakikisha wewe roho unayeishi katika mwili, hakikisha unamcha MUNGU na kutembea kwenye kusudi lake la uzima wa milele katika KRISTO YESU.
 
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments