HAKIKISHA YESU KRISTO NDIYE MWOKOZI WAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu!
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Kuna wanafunzi wa YESU na kuna wapinga Kristo.
Wapinga Kristo wako nje ya KRISTO lakini pia wapo wapinga Kristo ambao hujaribu kuwa kotekote yaani nusu kwa MUNGU na nusu kwa shetani.
Sizungumzii  dini ya mtu wala dhehebu la mtu bali nazungumzia  mtu mwenyewe Binafsi, Nazungumza na mtu na mtu husika Binafsi.
Tangu zamani shetani ametamani kuabudiwa, na kwa kupitia watu wachache wasio na KRISTO YESU ndani yao aliteka wengi.
Leo kuna akina mungu Baali wengi tu ambao wote ni watumishi wa shetani wanaoabudiwa na wanadamu.
Kibiblia Baali mwanzo lilikuwa jina la mtu mwabudu shetani ambaye chimbuko lake lilikuwa mji wa Edomu huko uarabuni.
Mwanzo 36:38 " Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake."

Edomu ulikuwa ni mji wa ushirikina, uganga, uchafu, uabudu shetani na vinyago vya kishetani vilikaa.
Mhubiri wa kwanza wa shetani alikuwa Baal na huyo ndiyo alikuwa kuhani wa kwanza wa shetani.
Kadri miaka ilivyoendelea kuna kundi la watu walianza kumwabudu Baal ambaye chimbuko lake ni roho ya kuzimu.
Hata leo kuna dini nyingi wanamwabudu mungu Baal na sio MUNGU wa mbinguni.
Wengi hawamtaki Bwana YESU awaokoe kwa sababu tu mungu Baal amewateka na kuwapofusha macho.
Wengi ukiwaambia wampokee YESU kama Mwokozi watakuambia wao wanaye Baal (hata kana hawamtaji kwa jina la Baal)
Wengi hawamhitaji Bwana YESU kwa kigezo kwamba mungu wao ni mmoja (Baal)

Siku akija Bwana YESU ndipo kila mtu atamjua na ndio siku hiyo kila goti litapigwa mbele zake maana atakuja katika nguvu, mamlaka na utukufu.
Wafilipi 2:9-11" Kwa hiyo tena MUNGU alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la YESU kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa MUNGU Baba."

Ewe ndugu unayeukataa wokovu wa Bwana YESU hakika uko kwa mungu baal na hata kama Baal kakufundisha sheria nyingi za dini yake ya kishetani lakini mwisho ni jehanamu na sio mbinguni.
Hata kama Baal anakuambia kwamba anakuandalia pepo, naomba nikuambie kwamba anakuandalia mapepo tu na sio pepo.

Ni rahisi tu kuhama kutoka kwa Baal ukiamua.
Biblia inakushauri kwa upole kabisa ili usiende jehanamu ambako Baal anawadanganya sasa kwamba ni pepo.

Ndugu mpokee YESU kama Mwokozi wako na anza kuishi maisha matakatifu katika yeye hakika hutajuta milele.
Yohana 3:16-18 "Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU."


Ndugu usikubali Baal akudanganye hata usimwamini Bwana YESU na kumpokea ili upate uzima wa milele .
Ndugu usikubali Baal na wahubiri wake wakutoe kwa YESU kwenye uzima wa milele.

Kumbuka Wokovu sio wa kundi Bali wokovu ni wa mtu mmoja binafsi.
Ukitaka wokovu uwe wa kundi basi baadhi ya wana kundi wakirudi nyuma basi na wewe utarudi nyuma.
Lakini ukijitambua kwamba wokovu ni kwa ajili yako binafsi basi utaendelea na YESU KRISTO hata kama ulionao wamekengeuka.
Utaendelea na utakatifu hata kama jamii yako iko mbali na MUNGU.
Wokovu sio wa familia kiasi kwamba baba au mama akiacha kwenda Kanisani na wewe unaacha.
Wokovu sio wa ukoo kiasi kwamba mkuu wa ukoo wetu akisema "Inatosha kumwabudu MUNGU wa kweli, basi tuigeukie mizimu" wewe mteule usikubali kufuata miungu hiyo hata kama ukoo mzima wameigeukia.
Kumbuka wokovu wa KRISTO ni kwa ajili ya mtu mmoja binafsi anayejitambua.
Hakikisha unang'ang'ania taji yako ya uzima ulioipata baada ya kumpokea Bwana YESU.

 Warumi 6:23 ''Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU Bwana wetu. ''

Twende wapi wakati YESU ana maneno ya uzima?
Mtume Petro alipouliza na Bwana YESU kama na yeye anataka kumwacha YESU kwa sababu dunia alisema neno hapo juu.
Hata sisi wateule leo tunasema hatuna pa kwenda ila kwa YESU mwenye uzima wetu wa milele.

Yohana 6:67-68  ''Basi YESU akawaambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.'' 
 
Kuna vyanzo vingi vya watu kuwa kwenye vifungo.
Baadhi ya vifungo hivyo ni; .
1. Watu wengi wahataki kuishi maisha matakatifu ndio maana wanateswa na vifungo vya giza vingi maana dhambi zao zinafungua mlango wa shetani kuwashambulia. 2. Sababu ya pili ni kwamba Leo watu wengi wanaabudu sanamu na kwa sababu hiyo vifungo vya giza vinawatesa.
 Unaweza ukasumbuliwa na mapepo kwa sababu tu ya vitu vya kipepo ulivyowahi kuvaa au kuvalishwa, kupakwa au kujipaka, kulishwa au kula mwenyewe lakini ashukuriwe MUNGU maana damu ya YESU na jina la YESU vinaweza kukuondolea mapepo yote. 
Husika tu na maombezi kanisani au kwa watumishi.

Leo kuna wapinga Kristo wa kisirisiri.
Japokuwa Ibrahimu Ni Baba Wa Imani Lakini Hiyo Haina Maana Kwamba Sara Ni Mama Wa Imani. 
 Mambo Ya Kiroho Huwa Tofauti Na Mambo Ya Kibinadamu. Tukiruhusu Kanisa Liifuate Dunia Basi Ipo Siku Tutasikia Kwamba Stephano Au Ayubu Ni Babu Wa Imani. Dunia Leo Imeingia Kanisani Ndio Maana Kuna Mawakala Wa shetani Hujipachika Katika Baadhi Ya Maandiko Na Kudai Maandiko Hayo Yaliwatabiri Wao.
 Kuna Watu Hudai Wao Ni Eliya Amerudi Duniani, Kuna Watu Hujiita Kristo, Kuna Watu Hujiita Henoko Aliyerudi Duniani, Wengine Hudhani Kuna Mtu Anaitwa Mama Wa Mungu. Kuna Watu Hujiita Mungu Muumbaji Aliyekuja Kuishi Na Wanadamu Na Kuna Waongo Original Hudai Biblia Iliondolewa Zamani Na Kuja Kitabu Kingine. 
Hao wote wanafanyia kazi fundisho la mpinga Kristo.
Kanuni Ya Biblia Iko Tofauti Sana Na Kanuni Za Kibinadamu Au Kanuni Za Kimwili. 
Ukitaka Biblia Ikufuate Utaishia Pabaya. 
Wewe Mwanadamu Ndio Unatakiwa Uifuate Biblia. Biblia Haiwezi Kubadilishwa Na Mazingira Wala Haiwezi Kubadilishwa Na Wanadamu. 
Kataa Kuokoka Harafu Utarajie Mbingu. 
Mkatae YESU Ukidhani Utafika Mbinguni.
Unahitaji kuwa makini sana.
Usikubali mawakala wa shetani wakuondoe kwa Bwana YESU.
Bwana YESU anasema na moyo wako leo kwamba  ''Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.-Ufunuo 3:20''

Dhambi ambayo mtu ameshindwa kuikataa, kuikemea na kuiacha ni kwamba dhambi hiyo itamea, itamuathiri na itamwangamiza asipopata kutubu na kuacha.
Dhambi huwa haipakwi rangi Bali dawa ya dhambi ni kutubu na kuiacha.

Mambo matatu ambayo shetani hana ni.
1. Ufunuo.
2. Ufahamu
3. Maono.

Wanaomfuata shetani hukosa ufunuo wa MUNGU na kwa jinsi hiyo watu hao huangamia.
Wanaomfuata shetani hukosa ufahamu ndio maana mtu anaweza akajiunga katika mikataba ya kishetani huku akijua baada ya muda shetani huyo huyo atamuua mtu huyo.
Wanaomfuata shetani hawana maono ya MUNGU ndio maana wanafanya dhambi huko wakijifariji japokuwa wanajua kabisa kwamba mwisho wa wenye dhambi ni jehanamu.

Ndugu mkimbie shetani Leo.
Mpokee Bwana YESU mwenye uzima wa milele.

Kumb 18:10-11 " Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu."

Usiishi jana kwa sababu leo ipo inakusubiri.
Jambo muhimu sana kwako ni Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana, huo tu ndio utadumu iwe ni juzi, jana, leo, kesho na kesho kutwa yako. Kama Aliyeuleta Wokovu anavyodumu basi na wokovu huo hudumu.
 Kadri unavyozembea kwa MUNGU, ndivyo MUNGU anazidi kukuacha! Ndugu usikubali MUNGU akuache.
Hakikisha YESU KRISTO Ndiye Mwokozi wako. 
Yohana 3:36 ''Amwaminiye Mwana(YESU) yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana(YESU) hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.''


 MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments