MWOKOZI YESU TUSAIDIE ILI TUWE WAAMINIFU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU
Mwokozi YESU nisaidie, ili niwe mwaminifu siku zote, ili siku ile ukija nami niingie uzima wa milele.
Bwana YESU ulisema
"Duniani mnayo dhiki lakini jipeni moyo, Mimi nimeushinda ulimwengu- Yohana 16:33"


Ni kweli wakati mwingine tunakutana na magumu, wakati mwingine tunakutana na dhiki lakini magumu na dhiki hayatakiwi kutufanya tuwe mbali na wewe Mwokozi.
Eee Bwana YESU tusaidie.
Wako wamama wanapigwa Sana na kuonewa na waume zao kwa sababu tu wameamua kukupokea wewe YESU kama Mwokozi, Ee Bwana YESU umesema wajipe moyo.
Wapo ndugu wametengwa na familia na ukoo kwa sababu tu wameokolewa na wewe, Ee mfalme wa uzima watie nguvu.
Wapo watu wanatishwa sana na maadui, lakini MUNGU Baba wewe bado uko nao maana wametii mpango wako wa Wokovu.
Wewe JEHOVAH uliyeumba mbingu na dunia unasema

" usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni MUNGU wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia. Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.
Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.-Isaya 41:10-13


Asante Ee MUNGU wetu wetu maana katika wewe tunashinda na zaidi ya kushinda.
Ee MUNGU wetu, wapo watu wamedharauliwa na dunia kwa sababu tu wameokoka.
Wako watu wanaonekana ni vituko lakini kwa sababu tu wameokoka.
Wewe Bwana YESU unasema
" Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwafisha.
 Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.-Mathayo 10:21-22


Ee BWANA tusaidia tumalize mwendo salama.
Tusaidie uchungu usitumeze, kutokusamehe kusitumeze, dhambi isitupate kamwe.
Madeni yasitukamate, dunia na anasa za kidunia zisitukamate.
Tusaidie MUNGU wetu maana katika wewe tu tunashinda.
Tunambua kwamba "Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.-Isaya 35:8

 
Eee MUNGU wetu wa uzima wetu tusaidie.
Najua kama vile Siku ile tunaokoka kwa kukupokea Wewe YESU KRISTO kama Mwokozi, Malaika mbinguni walishangilia sana, Eee MUNGU Baba tunaomba hata siku tunaondoka duniani Malaika washangilie maana sisi tu wa KRISTO YESU Mwokozi wetu milele, na huko tuendako ni uzima wa milele.
MUNGU Baba nakushukuru sana tena kipekee sana kwa kutupa ROHO wako MTAKATIFU ili atuongoze.
Eee ROHO wa kweli naomba unisaidie kushinda dhambi, uovu na makosa. Nisaidie kushinda ya dunia yote.
Wewe ni wa thamani sana na Neno la MUNGU linathibitisha hivyo, Na Mwokozi YESU anathibitisha akisema
" Nami nitamwomba BABA, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai.
Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya BABA yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na BABA yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.-Yohana 14:16-21.


Asante Bwana YESU kwa wema wako, kwa kuja kutuokoa sisi tunaokutii.
Tunajua kabisa hakuna uzima wa milele nje na wewe hivyo tunakaza Mwendo ili tufike mbinguni.
Tunakushuru MUNGU Baba kwa upendo wako kwetu.
Tunakushuru MUNGU Mwana kwa Neema yako ya ajabu kwetu.
Tunakushuru MUNGU ROHO MTAKATIFU kwa ushirika wako kwetu.
Tuna furaha katika yote maana YESU ndio Mwokozi wetu na tunaelekea uzima wa milele.
Tumekataa dhambi na machukizo yote ya dunia, Wewe Bwana YESU KRISTO unasema "Naja Upesi -Ufunuo 22:20 ,na ndio maana na sisi wateule wako tunasema " Amina; na uje, Bwana YESU.-Ufunuo 22:20


By Peter Mabula
0786719090
0714252292

Mabula1986@gmail.com
Ndugu ambaye hujampokea YESU KRISTO kama Mwokozi, wala hujachelewa, itumie Leo yako kuokoka.
Wewe uliyerudi nyuma,amka Leo kutoka katika usingizi wa dhambi, tubu maana ufalme wa MUNGU umekaribia.
Wewe ambaye hujui kwa usahihi kwamba YESU KRISTO ni nani,Napenda kukujulisha kwamba YESU KRISTO ndiye pekee anayetakiwa kuwa Mwokozi wako. Kama kweli unautaka uzima wa milele hakika huo unapatikana ndani ya YESU KRISTO pekee, huo ndio mpango wa MUNGU Baba na sio vinginevyo.
Wewe uliyeokoka nakuomba songa mbele na Wokovu, haijalishi nani na wa wapi anasema nini kumbuka 2 Petro 3:13-14 " Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake."

Naamini mwenye kuelewa ameelewa.
Amen Amen Kwa YESU KRISTO

Comments