USHUHUDA HUU ULITAKA KUNITOA MACHOZI.

Michael Muema, Nairobi Kenya
Mtumishi Peter Mabula Shalom.
Mimi nilikuwa nimeokoka zamani nikiwa katika shule ya msingi na YESU alinitumia sana sana kuhubiria watoto wengine Wa rika langu neno la Mungu na hata wengine mpaka leo wamesimama na YESU.
Isipokua Mimi baada ya kumaliza shule nilirudi nyuma mbali na KRISTO mpaka mwaka 2014 ndio Siku moja nilipata kabiblia kadogo kakiwa na mtoto wangu HATA sijui alikua amekatoa wapi.
Na nilivutiwa na kukasoma kale kabiblia ka new testament(Agano jipya) nikahisi mvuto WA kunitaka nifungue kitabu cha ufunuo WA yohana na nilipoanza kusoma nilijihisi hatia sana mpaka nililia sana usiku ule nikimuomba YESU anisamehe na anirudishe tena katika upendo wake.
Na anirudishie tena ule ujasiri wa kuhubiri injili niliokuwa nao nyakati hizo za utotoni.
LAKINI SASA NDUGU YANGU SHIDA NI--SIJAWAHI KUJIHISI NA NGUVU ZA ROHO KAMA ZAMANI, NA PIA USOMAJI WA NENO,MAOMBI, HAYO YOTE NIMEKUWA MVIVU SANA.
"SASA NDUGU YANGU, KAMA IKIWEZEKANA NAKUOMBA PLEASE WEWE UNIULIZIE KWA YESU NENO KUNIHUSU MIMI KWA SABABU NINAAMINI KABISA ATAKWAMBIA JAMBO KUNIHUSU.
NA TENA KULINGANA NA VILE NIMEKUWA NIKIFUATILIA JUMBE ZAKO KATIKA MITANDAO YAKO, NIMEHISI KWA SIKU NYINGI KUWA ROHO MTAKATIFU YUKO NDANI YAKO, NA NIKIKUAMBIA SHIDA ZINAZONISONGA, NA UNIULIZIE KWA ROHO MTAKATIFU, BILA SHAKA ATAKWAMBIA JAMBO KUNIHUSU.
>TAFADHALI KAKANGU, MIMI SITAKI NIKIONDOKA HAPA DUNIANI, NIELEKEE KUZIMU NISAIDIE KWA MAOMBI ILI YESU ANIKUMBUKE TENA, NA NINAHAIDI KUTOKA KWA KILINDI CHA MOYO WANGU SITAWAHI TENA KUMSALITI ROHO WA MUNGU TENA MPAKA NIPUMUE PUMZI YANGU YA MWISHO.
na kwa upande WA kukusapoti kwa kazi ya Bwana YESU unayoifanya, nitatumia hiyo number tayari nimeiifadhi kwa simu YANGU.
utapata SMS YANGU ya sadaka yangu anytime asante sana Bwana YESU awe PAMOJA NAWE NDUGU yangu .
Mimi ni mkenya Michael Muema Niko Nairobi
.



Kutoka kwa Mwinjilisti Peter Mabula.
Baada ya kuusoma ujumbe wa ndugu huyu kutoka Kenya nilibaki kwa muda kadhaa nimetulia na kutafakari sana.
Ndugu zangu ushuhuda huu aliponitumia huyu ndugu kutoka Kenya ulinifanya niwe na mzigo wa kumuombea maana ni Neema ya MUNGU ilimgusa.
Sio kila mtu anataka kumkimbilia YESU ili asiende jehanamu, huyu ndugu amethubutu na hakika Bwana YESU atamsamehe na kumsaidia kushinda.
Sio kila mtu aliyerudi nyuma anaweza akawa na ujasiri mzuri kama huu wa kumwitaji tena Mwokozi YESU.
Ukiweza wewe mteule wa MUNGU omba pamoja nami kwa ajili ya ndugu huyu maana amegundua kwamba kwa shetani hakuna usalama ila uzima pekee ni kwa Mfalme YESU KRISTO.
Ukweli ni kwamba bila YESU KRISTO hakuna mwanadamu hata mmoja anaweza kwenda uzima wa milele (Matendo 4:12, Yohana 3:16-21)
Kumkataa YESU ni kuukataa uzima wa milele.
Kumkimbia YESU ni kuukimbia uzima wa milele.
Heri ndugu huyu amegeuka mapema na sasa safari yake ni mbinguni na sio kuzimu.
Ndugu unayesoma ujumbe huu nakuomba rudi kwa YESU kama ulimwacha.
Nakuomba okoka kama hujaokoka.
Nakuomba ishi maisha matakatifu kama kuishi.
Kumbuka baada ya kifo ni hukumu na sio kuokoka.
Kuokoka ni leo na sio kesho.
Nakuomba mpokee Bwana YESU Leo na ishi maisha matakatifu katika wokovu wake.
Hata dini tu haiokoi, dhehebu tu bila Wokovu huwezi kuokoka.
Amua vyema Leo ndugu na utabarikiwa.
1 Yohana 2:15-18 " Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho."

MUNGU akubariki ukiamua vyema.


 Baada ya ushuhuda huo sasa nakuletea shuhuda zingine zikiwahusu watu wengine.
Image may contain: 1 person, selfie and closeup
 Sospeter Antony
 
 Sospeter Antony  aliniandikia ujumbe huu ambao alionyeshwa kwenye maono
 
 MUNGU akubariki sana tena sana wewe ambaye umekuwa ukimtumikia KRISTO kwa njia yoyote ile, iwe kwa mali zako, nguvu zako, au kivyovyote vile,nikutie Moyo kuwa usikate tamaa, maana taji yako ipo, Biblia inasema kuwa, tutavuna tusipokataa tamaa. Ngoja nikushirikishe ujumbe huu ambao Mungu aliniambia, juu ya kanisa na kurudi kwake. Nikiwa kwenye mkutano wa injili, usiku nikiwa nimelala kanisani, katika njozi ya usiku " Ghafla niliona hali ya anga ikibadilika, ndipo nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, waambie watu wangu wajiandae nakuja kuchukua kanisa, nakuja kuchukua mtu aliye mtakatifu, hubirini watu wangu habari za kurudi kwangu, kila mtu ajichunguze mwenyewe moyoni, kama yupo vizuri na Mimi, nakuja kunyakua kanisa.
Hii sauti ilikuwa sauti ya kuogofya, lakini pia yenye upendo wa hali ya juu.
Baada ya hapo nilichukuliwa mpaka angani akanionyesha nchi ya Iran, na mataifa makubwa kama Urusi, China, Korea kaskazini, na mashariki ya kati kwa ujumla, nikaonyeshwa silaha mbali mbali ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya vita, kwenye hizo silaha, ambazo ni kutoka mataifa mbali mbali, ambazo zipo tayari kwa vita.
Mungu akanionyesha silaha ya nyuklia ambayo ipo nchi ya Iran, ambayo aliniambia ni silaha mbaya sana, na ina madhara makubwa, na pia ina uwezo wa kwenda masafa marefu. Ndipo sauti ilisikika toka mbinguni ikisema "
Hizo silaha hazitatumika kanisa langu likiwa duniani, nimezizuia, waambie watu wangu wajiandae nakuja upesi kuchukua kanisa langu, hubirini toba na utakatifu, muda umeisha, watu wangu hawatashuhudia hivyo vita.
Baada ya hapo nilishushwa chini, nikaambiwa, sehemu yeyote ulipo hubirini habari ya ufalme wa Mungu, atakaye nionea haya mbele za watu na Mimi nitamuonea haya huyo mtu mbele ya za Baba yangu"
Ni ujumbe ambao aliniambia hivyo ndugu yangu, nikutie nguvu kuwa Yesu yu karibu sana, wala usikate tamaa, dunia isikupotezee muda, Mungu anapoleta ujumbe wake, maanake ni kutuonya, pia kututia moyo, lengo ni mimi na wewe tujiandae kwa ujio wa masihi. Ukisoma Yoel 2:28, utanielewa.
By Sospeter Antony.

Watumie ushuhuda huu watumishi wa MUNGU wote unaowafahamu.
Ubarikiwe.



 Ushuhuda wa pili unanihusu mimi Peter Mabula.
DIRECTOR. PETER MICHAEL MABULA
Peter Mabula.
Siku moja  jumapili Nilienda kuhudumu Kigamboni Soweto Kanisa la P A G chini ya Mchungaji Eliza Kihwili, na ROHO wa MUNGU alinipa ujumbe usemao NJIA SABA(7) ZA KWANZA ZA USHINDI KATIKA VITA YA KIROHO.
Baada ya ujumbe huo kuna ndugu walihitaji kitabu changu cha MAOMBI YA KINA nikawapa.
Jambo la ajabu sana na ambalo lilinifanya nimtukuze MUNGU ni pale ambapo ndugu mmoja ambaye ni kipofu wa macho jina Enock aliponiambia kwamba anakihitaji sana hicho kitabu. Nilimtajia bei na akanunua. Baada ya kununua aliniambia nimsomee angalau kwa uchache kilichomo ndani ya kitabu changu, nilimsomea na akashangilia.
Moyoni mwangu niliwaza je atakisomaje kitabu wakati yeye haoni na hutembea kwa kusaidiwa na mtu?
Nikiwa bado nawaza hivyo ghafla Enock aliniambia kwamba hakika kitabu hicho kitamfaa sana maana atakuwa anasomewa na mtu kile kilichomo ndani ya kitabu.
Nilimshangaa MUNGU kwa imani ya ndugu huyo kisha nikamuombea na kuondoka kurudi nyumbani.
Kama kuna mtu amenitia moyo katika kitabu ni pamoja na huyo ndugu Enock.
Hakika kuna watu wana njaa na kiu ya haki.

Mathayo 5:6 '' Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.'

Comments