JE, HIVI MUNGU WA BIBLIA AMEKAA KIMYA JUU YA DOME OF THE ROCK YA WAISLAMU ILIYOJENGWA ISRAELI?



JERUSALEM

Na Jimmy John

Duniani kuna imani nyingi sana. Lakini imani PEKEE inayotangaza wazi kwamba Biblia ni uongo, Yesu ni mwongo, Mungu wa Israeli ni mwongo, na wafuasi wake ni waongo NI UISLAMU.

Tena dini hii haina shida na sana na uhindu, ubudha, nk. Nguvu yake KUBWA ni kupinga Wayahudi, Wakristo na Biblia.

Hivi kweli Mungu wa Biblia atakaa kimya kabisa asiseme chochote kwenye Neno lake juu ya Uislamu?

Hekalu la Mungu la kwanza lilitengenezwa na Musa jangwani. Kwa sababu walikuwa wako safarini, lilikuwa na kuhamisha. Lilitengenezwa kwa mapazia yaliyofungwa kwenye nguzo.
Hekalu hilo lilikuwa na sehemu kuu tatu:
- Ua wa nje (Kut 27:9)
- Patakatifu (Ebr 9:2) na
- Patakatifi pa patakatifu (Ebr 9:3)


Sulemani alipokuja kujenga hekalu Yerusalemu lilifuata mfano uleule wa hekalu la Musa jangwani.


Lakini hekalu hili la Sulemani lilikuja kubomolewa na Nebukadreza kutokana na dhambi za Wayahudi.

Baadaye lilijengwa jingine ambalo nalo lilikuja kubomolewa na Warumi.

Baadaye zaidi Waislamu walikuja kujenga jengo lao eneo lilelile ambako lilikuwapo hekalu la Sulemani. Lakini hawakujenga kwenye patakatifu au kwenye patakatifu pa patakatifu.
Walijenga kwenye UA WA NJE.
Mojawapo ya majengo yao ni Dome of the Rock.

Katika karne ya 1, Bwana akasema na Mtume Yohana. Na hiki ndicho anachotufunulia Yohana.
Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. (Ufunuo 11:1-4)


Hapa tunaona kwamba:
1. Alipima hekalu (la Sulemani)
2. Behewa ya nje (ua wa nje) akaambiwa asipime

Kwa nini aliambiwa asipime ua wa nje?
Bwana anasema ni kwa sababu: MATAIFA WAMEPEWA HIYO, NAO WATAUKANYAGA MJI MTAKATIFU MIEZI AROBAINI NA MIWILI.

Mataifa kuukanyaga mji hapa maana yake kupanajisi mahali pa Mungu wa Israeli.

Kuanzia mwaka 688 BK maneno ya Mungu wa Israeli yakatimia. Waislamu chini ya Khalifa Abd al-Malik ibn Marwan wa Ummayad, walianza KUJENGA Dome of the Rock (au Qubbatus Saqqara) kwenye ua wa nje.


 Najua unabii wa Biblia huwa unatimia hata zaidi ya mara moja wakati ukingoja utimilifu wake wa MWISHO KABISA.
Ndio maana, kwa mfano, mwaka 168 KK Antiochus Epiphanes aliingia Yerusalemu akamwua kuhani mkuu na kuweka sanamu ya Zeus kwenye hekalu la Yerusalemu, na wengine wanadai kuwa alitoa hata sadaka ya nguruwe kwenye madhabahu. Huyu alitimiza unabii wa Danieli unaohusu Chukizo la Uharibifu. Lakini huo haukuwa utimilifu wa mwisho. Tunajua kuwa kabla tu ya kurudi kwa Yesu, utimilifu wa MWISHO KABISA utatokea kutoka kwa Mpinga Kristo mwenyewe halisi.

Kwa hiyo, hata haya ninayokuonyesha hapa, sisemi ndio mwisho kabisa wa kila kitu na sisemi kuwa ndio tafsiri pekee. Lakini tutafakari pamoja. Je, hii ni coincidence tu?

Tuliona kuwa Mungu anamwambia Yohana:
Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili. Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia. Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi. (Ufunuo 11:1-4)

Hawa mataifa (waislamu) walijenga Dome of the Rock kwenye behewa la nje kuanzia 688 BK.
Mungu anasema: nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi 42.
Pia anasema, kuhusu mashahidi wake: nao watatoa unabii siku 1260.

Sasa ona jambo hili:
Israeli walitawanywa duniani kwa miaka mingi.
Hawakuwapo kwenye nchi yao kwa muda mrefu sana.
Kwa kipindi chote hicho, mataifa waliendelea KUKANYAGA (KUNAJISI) behewa la nje.

Mwaka 1948, Israeli KAMA TAIFA walirudi kwao na kukomboa RASMI mji wao mkuu, Yerusalemu.
Miezi 42 ukizidisha kwa siku 30 kwa mwezi, unapata siku 1260
Na mashahidi nao wanatabiri siku 1260.
Kimsingi, kinabii hii ni miaka 1260.
1948 toa 688 ni sawa na 1260.

Kwa hiyo, waislamu walikanyaga behewa la nje kama sehemu yao RASMI kuanzia 688 BK hadi 1948 BK.
Je, hii ni coincidence tu isiyo na maana yoyote?

Najua kutaibuka maswali juu ya mashahidi wawili, lakini hao tunaweza kuwajadili kama part ya discussion. Ila unaweza kuanza kuwasoma kwenye kitabu cha nabii Zekaria sura ya 4.

Hakika Mungu wetu hawezi kuwa hajasema kitu kuhusu allah wa kaabah;
Maana huyo ndio mpinzani wake wa moja kwa moja.
Usimwache Yesu.
Utaangamia!

By Mchungaji Jimmy John

Comments