MASWALI NA MAJIBU NA MTUMISHI PETER MABULA.

Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU
Bwana YESU atukuzwe.
Niliulizwa maswali na watu mbalimbali na baadhi yab maswali hayo na majibu yangu ni haya.

Swali la kwanza.

Je ni sawa kwav Mwanamke kuwa Mchungaji au Askofu?

Majibu yangu ni haya.

Sio dhambi wala sio kosa Mwanamke kuwa askofu au mchungaji tena ni vizuri kabisa mwanamke akawa askofu mkuu maana MUNGU haangalii watu ila anangalia moyo ulio tayari kumtumikia. Wagalatia 2:6 ''Lakini wale wenye sifa ya kuwa wana cheo; (walivyokuwa vyo vyote ni mamoja kwangu; Mungu hapokei uso wa mwanadamu); nasema, hao wenye sifa hawakuniongezea kitu; ''
MUNGU hapokei uso wa mwanadamu bali anapokea aliye tayari kumtii yeye na kumtumikia tu
 Akiwa tu askofu maana yake atahubiri na atakufundisha pia
 Kila andiko katika Biblia huwa linathibitishwa na maandiko mengine, huo ndio umoja wa Biblia ndio maana binafsi nasema hivi kuacha kichwa wazi kanisani kwa wanawake ni sahihi kabisa maana jambo hilo halimuathiri mtu yeyote. na andiko hilo lilitamkwa kukataza watu wa kanisa fulani katika Biblia hivyo tukiiga hivyo ni sawa tu na tusipoiga pia ni sawa. Hivyo kufunika nywele ibadani kwa wanawake ni sahihi kabisa lakini pia na kutokufunika nywele ni sahihi pia maana haimathiri yeyote


 Swali linaendelea 
 1 TIM. 2:11-12
Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.

Je tafsiri halisi ya neno hili ni ipi maana imekua ikinichanganya


Majibu yangu.
 
 Hii ilikuwa Inawahusu wanawake wa kikoritho, walikuwa na desturi wakipata mali au wadhifa, wanakuwa juu ya waume zao. Na kujisahau kuwa wao ni wanawake wanapaswa kuwa chini ya waume zao. Hivyo andiko hili linamsisitiza mwanamke hata kama atakuwa na mali au wadhifa kuliko mume wake, anapaswa kuendelea kumtii mume wake.

 Swali la pili.
Umekuwa Ukitupa Mafunzo Mengi Sana Vijana, Juu Ya Ndoa!, Maswali yangu ni haya.
 1.Nani Alimfungisha Ndoa Yakobo, Alipoenda Kuoa Kwa Mjomba Yake Laban ? 
2.Ipi Ni Ndoa Halali Kibiblia,? 
3.Kwanin Mtu Awe Na Mke Mmoja, Ikiwa Ibrahimu Alizaa Na Wake Wawili, Yakobo Wake Wa 4 Wawili Wa Kuoa Wawili Masulia.

 Majibu yangu.
 Tamaduni za kipindi cha akina Labani zilikuwa ili umchukue mkeo ni lazima utoe mahari, ndio maana Yakobo akamtumikia Labani miaka 7 ili kupata mke. Kwa hiyo ukimpenda binti na akakukubalia unatakiwa kuchukua wazazi wako ili wakakubaliane na wazazi wa binti kisha unatoa mahari na kupewa mke wako. Lakini leo yote tunayotakiwa kuyafanya watu wa MUNGU ni lazima yote yawe katika BWANA.  
Wakolosai 3:17 '' Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.  ''

Majibu ya Swali la pili.
 Ndoa halali kibiblia ni ya mke mmoja kwa mume mmoja tu Mwanzo 2:18,24 '' Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. ''


 Sawa, Umenijibu Vyema Swali La Pili, Lakini Bado Nina Walakini Sana Juu Yakobo (israel) Ambaye Ni Kizazi Pili Cha Ibrahimu, Vipi Kwa Yeye Kuwa Na Wake Wawili Tena Ndugu Wa Baba Mmoja Nae Hakulijua, Hili? Vipi Leo Wazazi Wangu Na Wazazi Wa Binti Wakarithia Nitoe Mahari Na Wakanipa Binti Yao, Bado Haihesabiki Kama Ndoa?

 Swali la tatu umesema kwamba kwanini mwanaume aone mke mmoja tu? 
majibu yangu ni haya ni kwasababu 'Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.-Mathayo 7:12'' 
 Kumbe mwanaume anatakiwa amtendee mwanamke yale anayopenda yeye kutendewa. ukiona ni sawa kuoa wake 4 basi mruhusu na mkeo kuolewa na wanaume wanne lakini ukiona haiwezekani mkeo kuolewa na wanaume 4 basi na wewe usikubali kuona wanawake 4 bali baki na huyo mmoja maana unayopenda wewe utendewe basi watendee na wengine hivyo

 Majibu ya swali la kuoa wake wengi linaendelea hapa.
Akina suleiman walioa wake wengi kwa sababu ambayo ilikua kujibiwa na BWANA YESU. Mathayo 19:7-9 '' Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini. ''.
 Ugumu wa mioyo ulisababisha musa kuwaruhusu waisraeli kuoa wake wengi na kuwapa talaka lakini hiyo haikuwa katika mpango wa MUNGU. Jambo muhimu kujua ni kuhusu wakati uliopo leo wewe, ukitaka kumuiga Daudi kwa yote unaweza kuikosa mbingu, ndio maana leo hujaletewa Goliathi ili umpige mawe uwe kama Daudi hata uweze kumuiga


Swali lingine.
Najua Tumeambiwa Tutii Sheria Na Mamlaka, Zilizopo Juu Yetu, Je, Yatupasa Kutii Hata Sheria Za Kishetani?

 Hatupaswi kutii sheria za shetani maana shetani amewekwa chini ya nyayo zetu. kama tukiomba hakika utawala wa shetani utaondoka tu(Warumi 16:20)

 MUNGU akubariki.
By Mtumishi Peter Mabula.

Comments