NINAMSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA 2017.


Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU KRISTO atukuzwe.
Heri ya mwaka mpya .
Ni MWAKA ambao MUNGU ameuvika taji ya wema kwako.
Zaburi 65:11" Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono."
MUNGU akubariki sana na utauona wema wa MUNGU katika nchi ya walio hai.
Zaburi 27:13 "Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai."


Kipekee sana Napenda kumshukuru sana MUNGU Baba wa mbinguni kwa neema, rehema, kibali, kusudi lake na uzima wake kwangu kwa Mwaka 2017.
Kipekee sana Namshukuru Bwana YESU kwa kuniokoa na kunijulisha mpango wake kwa wanadamu.
Kipekee sana Namshukuru ROHO MTAKATIFU kwa kunipa neema, kuniongoza, kunifundisha na kunikumbusha.
Nnachoweza kusema ni kwamba ‘’Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yake yote ya ajabu. Nitafurahi na kukushangilia wewe; Nitaliimba jina lako wewe uliye juu- Zaburi 9:1-2”


Kipekee Namshukuru Mke wangu Scholar Mabula kwa kunitia moyo, kuniombea, kunishauri na kunisaidia katika huduma yangu.
Kipekee Namshukuru kila ndugu katika KRISTO aliyepaza sauti yake kuniombea au kuombea huduma yangu.
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya ndugu zangu wote katika ukoo, waliniombea, walinishauri na walinitia moyo ili nisonge mbele na kazi ya MUNGU. Ni wengi sana lakini kwa niaba tu namtaja Mzee wangu Moses Mabula na kaka yangu Samwel Mabula, MUNGU ambaye mbingu ni zake awabariki sana ndugu zangu wote.
Neno la MUNGU linasema kwamba ipo siku ya furaha JEHOVAH ataileta.
Isaya 12:4-5 ''Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka. Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote. ''

 
Napenda kuwashukuru rafiki zangu wote ambao walinifuatilia kupitia masomo yangu, hao mimi hupenda kuwaita ''Ndugu zangu.''. Namshukuru kila mmoja kwa kusoma masomo yangu.
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya kila rafiki zangu wachache walionisapot kwa sadaka ya hiari 2017 ili niweze kufundisha Neno la MUNGU kwa gharama zao, MUNGU ninayemtumikia awubariki sana na kuzidi sana.
MUNGU awajibu na awe Wokovu KWENU.
Zaburi 118:21 '' Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.''

 
Namshukuru MUNGU kwa ajili rafiki zangu walioniunga mkono kwa kununua kitabu changu cha MAOMBI YA KINA 2017, JEHOVAH aliye hai milele awakumbuke katika maisha yenu yote na katika ufalme wake kwa tendo hilo jema kwangu. Namshukuru MUNGU kwa marafiki ambao walikuwa wapokeaji wa vitabu vyangu kwa ajili ya kuvisambaza. MUNGU alinipa neema maana kitabu changu kimefika mikoa 13 Tanzania na nje ya Tanzania vitabu vyangu vimefika Kenya na Marekani, kwangu hiyo ni neema ya KRISTO na MUNGU wa mbinguni awabariki sana wote waliohusika na vitabu vyangu.
''siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,-Waefeso 1:16'' 

 
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya watu niliowaombea na baadhi yao walinipa ushuhuda wa matendo makuu ya MUNGU, Utukufu ni kwa MUNGU mwenyewe.
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya watumishi wa MUNGU kutoka kila mahali Tanzania na nje ya Tanzania ambao walinishauri, kunitia moyo, kuniombea na kunipa mialiko katika maeneo yao, sikwenda kwa sababu muda wa MUNGU wa mimi kutembea maeneo mbalimbali kuhubiri haujafika rasmi, ila muda huo utafika na maono yangu kila wilaya ya Tanzania nitafika kufundisha Neno la MUNGU, Na hata nje nitafika kama ROHO wa YESU KRISTO akinipa kibali na ruhusu ya MUNGU Baba.
Namshukuru MUNGU kwa kila mtu niliyeongea naye kwa simu iwe kwa kutaka huduma, ushauri, maono, mawazo au chochote. Hakuna Mwaka nimeongea na watu wengi kama mwaka huu.
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya Taifa langu la Tanzania, amani iliyopo Tanzania imefanya hata kazi ya MUNGU ifanyike vyema.
Mwaka 2017 nilijiwekea ratiba ya kuandika masomo 204 nikiwa na maana ya kuandika masomo 17 marefu kila mwezi. Niliweka hivyo kwa sababu nimekuwa na mambo mengi sana na nachoka sana, hivyo hata kama nimechoka lakini ROHO wa MUNGU alinitia nguvu ili nikamilishe kusudi lake, na kwa Neema ya MUNGU mwaka huu 2017 nimeandika masomo 219 na ni masomo 783 tangu nimeanza huduma hii ya kuhubiri Mtandaoni mwaka 2012.
Mimi binafsi na wote tuliojifunza masomo hayo naomba tu tufanye haya ''Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni MUNGU wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni BWANA wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. -Zaburi 136:1-4


Namshukuru MUNGU kwa ajili washirika wenzangu wa wa Kawe Pentecostal Church, Mchungaji wangu Elly Boto, na vingozi wangu wote Kanisani.
Namshukuru MUNGU kwa ajili ya kila rafiki yangu, kila mtumishi mwenzangu.
Kila anayesoma ujumbe huu nakushukuru sana maana MUNGU amekulinda hada kufika leo hii.
Naweza nikasema mengi sana lakini kwaa Neema ya MUNGU mimi nakuombea rafiki yangu na naomba MUNGU akupe 2018 yako iliyovikwa taji ya wema na yeye MUNGU kama Neno la MUNGU linavyosema katika Zaburi 65:11 Kwamba ''Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono.''
Mwaka 2017 sio kwamba maudhi hayakuwepo bali yalikuwepo tena mengi, vitisho na hila zilikuwepo lakini bado YAHWEH alibaki kuwa MUNGU wangu na kanuni ya Biblia ni nzuri sana maana siku zote inanifundishwa kwamba ''Heri ninyi watakaowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu- Mathayo 5:11-12’’ 

 
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza kitu muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
0714252292(Hadi whatsapp).
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments