SHUHUDA ZA MATENDO MAKUU YA MUNGU.

Peter Mabula, , Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU.
YESU wala hajawahi kushindwa kuponya ugonjwa wowote.
Ndugu, huyu ametendewa muujiza mkubwa.

Anasimulia USHUHUDA wake akisema.
Bwana Yesu Asifiwe, kipekee namshukuru Mungu kwa kuniponya ukimwi, ilikuwa 15/5/2017nilipoenda klinik ya ujauzito na kuambiwa mimi ni mwathirika,nilichanganyikiwa,kwa sababu ni kitu ambacho sikutegemea,nilikataa majibu nikawa nasali,niliamini nitapona,manesi walinitaka kumeza dawa nikakataa,niliomba na watumishi mbalimbali akiwemo Crispin Adam, Peter Mabula,Yohana,Shagihiru na Mch Jacob wa Kasulu,baada ya kujifungua Mume wangu alinikimbia,niliendelea kumuomba Mungu pasipo kukata tamaa, huku nikiombewa sana na watumishi hawa,siku ya kwanza baada ya kujifungua nilichukua maji nakuyaombea kisha nikampa mtoto wangu baada ya kujifungua maana niliamini na yeye aneathirika sikuwa na Maziwa kabisa,siku ya NNE baada ya kujifungua nilimpigia Mch Jacob tukaomba na nilipata Maziwa,baada ya hapo aliendelea kunitia moyo juu ya uzima wangu,Aliniambia anaonyeshwa aje tuombe na aniwekee mkono,huku nikiomba na watumishi wengine pia na magroup mbali mbali,alikuja kutoka Kasulu tulifanya huduma na tukapima nikapata majibu mazuri,nilikua na dada mmoja ambaye ni Nesi kutoka Lindi na yeye alikuwa mwathirika, wote tulipata uzima,baada ya siku tatu nilipigiwa simu na Nesi kwamba mtoto ni mzima hana maambukizi,nilimtukuza Mungu, Hata mimi nilipopima hakika nilikuwa mzima. mpaka sasa nashangilia uzima wangu,mpendwa nakusihi usikate tamaa wewe omba na umaanishe Mungu hashindwi jambo,kwa mwenyewe shida asisite kuwatafuta hao watumishi hapo huu,asanteni
By Glory


Huo ndio ushuhuda wa Glory alionitumia huku akiwatumia na watumishi wengine waliohusika kumuombea.
Binafsi Mimi nilimuombea Mara 4 kwa simu na ajabu siku ananipigia simu akinikumbusha hadi maandiko niliyotumia kumuombea.
Namshukuru MUNGU maana amemponya ndugu huyu.
Maandiko hayo niliyotumia Mimi kumuombea ni Yeremia 33:6, Yeremia 30:17, Isaya 53:5 na Mathayo 9:35
Utukufu ni kwa MUNGU juu mbinguni. Nawashukuru sana pia na watumishi wa MUNGU waliomuombea ndugu huyu hadi MUNGU wa miujiza akatenda miujiza.
Katika maisha Yangu mimi Peter huyu sasa ni mtu wa nne kumuombea na Bwana YESU akamponya ukimwi.
Ndugu uliye na tatizo kama hili nakuomba tafuta Kanisa sehemu uliko na mweleze Mchungaji na utaombewa na kupona. Wasumbue watumishi au uwe wazi kwao na hakika MUNGU anaweza kukutendea muujiza.
Lakini lazima ujue ni kwanini MUNGU anakuponya ukimwi.
Nakumbuka siku ya naongea na ndugu huyu kwa Mara ya kwanza kwanza alikuwa mkali hadi kwenye simu na alikuwa na hasira maana mume wake alimkimbia baada ya kugundulika ameathirika.
Ndugu, inawezekana uko hoi na ndugu zako wanasubiria ufe maana wanajua hutapona kutokana na ugonjwa unaokutesa. Mimi nakushauri okoka kisha husika na maombezi na MUNGU anaweza kukupa Neema na ukapona.
Siku moja ROHO MTAKATIFU aliniambia kuna mambo manne yanayoweza kumfanya mgonjwa apone, hata kama ni ugonjwa mbaya sana, baada ya kunisemesha hivyo akanijulisha mambo matatu hapo hapo na jambo la nne ipo siku ataniambia maana siku hiyo alinijulisha mambo matatu.
Mambo hayo matatu ambayo yanaweza kumfanya mtu apone ugonjwa kwa maombi ni;
1. Imani ya muombaji.

2. Imani ya muombewaji.
3. Kwa utukufu wa MUNGU.
Siku moja nitafafanua hayo, hasa utukufu wa MUNGU maana kuna watu hupona kwa sababu ya utukufu wa MUNGU.
MUNGU akubariki sana.
By Peter Mabula


USHUHUDA WA PILI.

Bwana YESU atukuzwe.
Tuko mwisho wa mwaka na napenda kukupa ushuhuda huu ambao rafiki mmoja ambaye nilimuombea aliniandikia.

USHUHUDA.
Mtumishi Wa MUNGU katika Bwana Peter M Mabula Shalom . Nakusalimia Katika Jina La Bwana wetu YESU KRISTO nikisema Neemaya Bwana Wetu Yesu Kristo Napendo La MUNGU na ushirika wa ROHO MTAKATIFU VIWE NANYI. kwanza nitangulize shukrani zangu za dhati kwa MUNGU WETU WAMBINGUNI ambaye YEYE anaendelea kukilimia mema sisi wenye dhambi bila kujali tuamuudhi kiasi gani kwakukulinda Wewe Unaetupatia matunda yakiroho Eee MUNGU WETU poke Sifa na HESHIMA Na UTUKUFU NA SIFA ZOTE NA ADHAMA ZOTE Kwani Ukiitwa Unaitikia Kama Unavyosema Katika NENO LAKO katika yeremia 33:3 ASANTE MUNGU KWA KUTUWAZIA MEMA . Mtumishi Peter M Mabula, naomba unikubalie, nikushukuru, sana, sana, sana, kwa Msaada Wa maombi Yako Mtumishi Nilikuwa nimefugwa Sana Tena Sana Kwakila Kitu Kipato Kilipotea Nilikuwa na Mpango Wakuoa Uchumba Ukavunjika Yani Kila Kitu Ila Saivi Naona Wema Wa MUNGU Nakuomba usichoke kuniombea nataka mpaka nipate kitabu cha maombi. ubalikiwe sana"
Majibu yangu mimi Peter yalikuwa haya.
Amen na Ubarikiwe sana.
tuko pamoja na nitazidi kukuombea.
Ubarikiwe pia kwa kuhitaji kitabu changu.
MUNGU akubariki na kukufungulia milango ya baraka na ushindi.
Amen



USHUHUDA WA TATU.

Ushuhuda baada ya kufundisha kuhusu ufanyeje ili uweze kuomba muda mrefu?
Bwana asifiwe wapendwa katika Bwana, mimi nipo mbele yako nikimshukuru MUNGU kwa miujiza alionitendea siku ya jana nilikuwa napenda Sana kuomba lakini nilikuwa siwezi, Roho wa Mungu akanishuhudia Kuwa niingie katika mtandao nikakutana na blog ya Mtumish wa Mungu Peter mabula, nikajifunza kwa kina namna ya kuomba lakini tatizo lilikuwa siwezi kuomba kwa Muda mrefu Roho wa Mungu akanishuhudia Kuwa bado Ninatakiwa kuomba Sana nikajiuliza nifanyeje? nikaongozwa nimuulize mtumwa Peter mabula nifanyeje ili niombe Muda mrefu ndio mtumishi wa Mungu akanielekeza jana kwa undani zaidi. namshukuru Mungu Muda huo huo nikafnya kama alivonielekeza aiseee namshukuru Mungu nilifanikiwa kuomba masaa matatu mfululizo kwa mara ya kwanza.
Namshukuru Mungu sana na utukufu kwa Mungu.
By Mary.
Iringa



USHUHUDA WA NNE
 
Bwana Yesu asifiwe saaana
Nawiwa kusema haya jamani na kama nisipo mshukuru Mungu ktk hili nitakuwa mnafiki

Namshukuru Mungu ktk maombi niliyokuwa nikimuomba watu ambao anikutanishe nao ktk safari yangu ya wokovu na Mungu amefanya ktk hili na bado ameahid kufanya
Thanks God kwa ajili ya kunikutanisha PETER MABULA amefanyika baraka saana kwangu
Thanks God kwa ajili ya ISAYA KAKUSA umefanyika saana baraka kwangu
Thanks God kwa ajili ya Carlos Kirimbai.
Amekuwa baraka saana kwangu

Thanks God kwa ajili ya mchungaji Shagihilu amefanyika saana Baraka kwangu
Hiz ni shukran za kipekee sanaa japo wapo wengiiii mmekuwa sehemu ya kunisogeza kiroho
Mungu akawape upako mpya wa 2018
Mbarkiwe saaaana
Nimetembea kwa ushindi 2017 kwa mafundisho yenu na ushahuri wenu Mungu awabariki one day Mungu akinipa kibari nitakuja kuwaona Mbarikiwe saaaaana

Niwatakie heri ya mwaka mpya.
by Vicky Steven, mtumwa wa Bwana
Ameen

Comments