USHUHUDA WA KUPONA UKIMWI

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu zangu.
Namshukuru MUNGU wa mbinguni maana huyu sasa ni mtu wa tatu aliyenijulisha kupona Ukimwi baada ya kumuombea. Alikuwa na Ukimwi kwa miaka 4 lakini Bwana YESU amemponya sasa, Utukufu wote ni kwa MUNGU Baba juu mbinguni.
Nimeombea wengi na sio wote walipona maana sikujua kwa sababu hawakunijulisha wote ila kwa hawa namshukuru sana MUNGU Baba.
Ilikuwa ni Leo aliponijulisha, ilikuwa hivi.


HUYO NDUGU: Kaka mabula Mungu amenifanyia mimi nimetoka kupima hamna kirusi hata kimoja

PETER MABULA: Namtukuza MUNGU mponyaji, alisema nami kwa Yeremia 10:6 na Zaburi 83:18.
Songa mbele na YESU, wewe ni mshindi na usikubali kurudi dhambi ni tena.
MUNGU amekufanya kuwa ushuhuda na mtolee MUNGU sadaka ya shukrani huku ukiufunga mlango alioutumia adui Mwanzo kuingia kwako.
Ubarikiwe sana sana, Nina furaha mno hata Mimi kwa ajili ya muujiza huo ambao MUNGU alikutendea kupitia ROHO MTAKATIFU na nguvu zake.
Ubarikiwe sana sana


HUYO NDUGU: Ninakosa maneno ya kumshukuru Mungu, nakosa sadaka nzuri yakumtolea Mungu wangu naomba tu Mungu anifanye dhabihu nitumike kuwarudisha vijana waliotekesa kama mimi

PETER MABULA: Amen amen amen sana.
MUNGU alitimize hilo ndani yako.
Hakika Ubarikiwe sana.
MUNGU Baba akupe maisha marefu, akupe utumishi halisi katika injili ya KRISTO.
Kazi yako imzalie MUNGU matunda mema.
Kupitia wewe washinde makumi elfu ya watu.
Kupitia wewe watu wakajue kwamba yuko JEHOVAH aliye hai milele.
Leo Mimi nitakuwa na maombi ya kumshukuru Bwana YESU kwa ajili yako.
Tunza muujiza wako maana muujiza uliopatikana kwa maombi hutunzwa kwa utakatifu, ushuhuda, maombi na unyenyekevu zaidi kwa MUNGU.


HUYO NDUGU:Amen nakuahidi sitarudi tena

PETER MABULA: Shetani anaweza akaandaa mtego wa watu kukuambukiza tena ili usimpe MUNGU utukufu lakini wewe husika na KRISTO,wala adui hatapata nafasi kwako kamwe.
Omba maombi ya kumwekea shetani mipaka na hakikisha malaika wa MUNGU wanakuhudumia sawsawa na Zaburi 34:7 na Waebrania 1:14.
MUNGU akubariki sana.


HUYO NDUGU: Amen mtumishi usiniache kwenye maombi yako pia naamin nitashinda ktk yeye anitiae nguvu

PETER MABULA: Ushuhuda mdogo huu nitauweka mtandaoni kama ulivyo ili uwasaidie watu waliokosa tumaini, wajue kwamba lipo tumaini kwa Bwana YESU kwa kila anayeamini na kuamua kumtii MUNGU maisha yake yote.
Sitataja jina ili usipate usumbufu wowote lakini naamini kuna watu walijichimbia makaburi rohoni sasa watayafukia na kumkimbilia YESU KRISTO awaponye. Nakumbuka siku ya kwanza nakuombea nilitumia Mathayo 9:35, Yeremia 33:6, Luka 1:37, Isaya 43:19 na hayo maandiko ya kwanza.
Yaani namshukuru MUNGU mno


HUYO NDUGU: Oooh sawa haina tatizo mtumishi

PETER MABULA: Amen .

Nb.
YESU KRISTO anaponya kwa walio tayari.
Ukijua kwamba MUNGU anaweza yote basi hudhuria mikutano ya injili na semina za Neno la MUNGU utapona.
Wafuate wachungaji katika eneo lako watakuombea na utapona.
Hudhuria ibada kila Mara katika kanisa la kiroho utaombewa na kupona.
Jiunge na kanisa na utaombewa na kupona.
YESU KRISTO anaokoa, ukiamini Leo hakika unaokoka.
YESU KRISTO anaponya, ukiamini Leo hakika utapona.
Ubarikiwe sana.

By Mwinjilisti Peter Mabula.

Comments