MAOMBI YA KUFUTA NYONGEZA ZA KISHETANI KATIKA UUMBAJI WA MUNGU KWAKO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU kisha tuombe maombi ya ushindi.
MUNGU ndiye muumbaji wetu.
Na ni MUNGU alikujua wewe kabla ya kukuumba.
Yeremia 1:5 '' Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa .............''

Sasa Biblia iko wazi sana ikisema kwamba MUNGU aliviona kuwa ni vyema sana alivyoviumba ukiwemo na wewe mwanadamu, 
Mwanzo 1:31 ''MUNGU akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.''
kwahiyo unaweza kusema kwa ujasiri kabisa kwamba ''MUNGU aliponiumba aliniona mimi ni safi na mwema''
MUNGU alikuumba kwa kusudi kabisa, na wewe katika siku ya uumbaji wa MUNGU ulikuwa safi kabisa.
 Sasa nisikilize itakusaidia.
Ni kwamba MUNGU alipokuumba wala hakukuumba ukiwa na laana yeyote.
MUNGU alipokuumba hakukuumba ukiwa na mapepo ndani yako.
MUNGU alipokuumba wala hukuwa na roho ya kukataliwa au kuteseka.
MUNGU alipokuumba wala hakukuumba  ili mwili wako ufuatane na mizimu.
MUNGU alipokuumba hakukuumba na magonjwa.
MUNGU alipokuumba alikuumba ukiwa safi, umekamilika na huna kasoro yeyote.
Mwanzo 1:27 '' Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.''

 MUNGU alipokuumba alikuumba kwa kusudi lake jema.
MUNGU hakukuumba ili uwe mvaa hirizi, wala MUNGU hakukuumba ili ushirikiane na shetani kwa namna yeyote.
Shetani na mawakala zake ndio wameleta nyongeza za kipepo kwa watu wengi walioumbwa na MUNGU.
Kuna watu magonjwa yamekuwa sehemu ya maisha yao kiasi kwamba wanadhani MUNGU aliwaumba na magonjwa.
MUNGU hajawahi kumuumba mtu akiwa na magonjwa.
Kuna watu wanaishi na mizimu na hiyo ndio inawaongoza kishetani mwaishani mwao. Mizimu ni mashetani na hiyo haitakiwa mwanadamu yeyote mwenye akili timamu kushirikiana nayo.
Kuna watu wanaishi na mapepo, kuna watu wana maroho ya kuzimu na maroho hayo yanawatesa.
Hivyo vyote ni nyongeza za kishetani  katika maisha yao.
MUNGU hajawahi kukuumba ukiwa na matatizo ya kiroho ulio nayo sasa.
Siku moja mimi P Mabula nikiwa kwenye maombi usiku saa saba kasoro dakika chache ROHO wa MUNGU alinisemesha juu ya somo hili kwamba nifundishe kimaombi kufuta nyongeza za kishetani zote katika maisha ya watu.  Ndio maana leo najua unaenda kushindi katika jina la YESU KRISTO. Ngoja tujifunze kisha tutaomba maombi ya kuurudisha uumbaji wa MUNGU kwako.
Inawezekana ninyi kabila lenu huwa mnakeketwa na kumbe wazee wenu wanajua kufanya hivyo ni kupokea agano la kishetani la kabila.
Mtu mmoja alinipigia simu akiniambia kwamba amezaa mtoto yapata sasa miezi kadhaa lakini amezuiliwa kumnyoa mtoto nywele za kwanza hadi babu yake kizaa baba atakapopata nauli na kutoka kaskazini mwa Tanzania kuja kusini ndipo atamnyoa na kuondoka na nywele hizo, Kitu kama hicho kinaweza kuleta nyongeza nyingi za kishetani kwa mtoto na vifungo hivyo vinakuja kumtesa sana baadae.
Huo ni mfano hao wa jinsi nyongeza za kishetani zimeongozwa kwa watu wengi sana na sasa wanateseka sana.
Mama mmoja alinipigia simu akisema  kwamba ametunza kwa miaka miwili kitovu cha mtoto wake kilichokatwa na alificha kwa sababu ndugu wa mtoto kutoka upande wa baba wa mtoto walikuwa wanakitafuta na wanalazimisha waondoke nacho.
Watu wengi sana waliumbwa na MUNGU vizuri sana lakini shetani ameleta nyongoza nyingi za kipepo tangu wakiwa tumboni au wakizaliwa.
Leo ndugu katika jina la YESU KRISTO kuna kuondoa nyongeza zote za kishetani katika maisha yako kupitia maombi katika jina la YESU KRISTO na kwa damu ya YESU KRISTO ya agano jipya la ushindi wa milele.

 Nyongeza za kishetani zinaweza kuja kwa njia gani?

1. Uongo wa shetani kupitia vizazi.
Hiki ni chanzo kimojawapo cha nyongeza za kishetani nyingi kuwekwa kwa watu wa jamii fulani au familia fulani au ukoo fulani.
Kuna watu katika jamii zao tangu vizazi shetani ameendelea kupofusha fikra zao ili iziwazukie neema ya KRISTO.
2 Kor 4:3-4 ''Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake KRISTO aliye sura yake MUNGU.''
Inawezekana wewe na wazazi wako na babu zako mnajua kwamba kutambika au kuomba wafu au kushirikiana na majini  mliumbiwa hivyo na MUNGU kumbe ni shetani ambaye ni mungu wa dunia hii amepofusha fikra zenu tangu kizazi hata kizazi hiki.  Ndio maana kila anayezaliwa katika familia yenu  anafuata mkondo huo huo wa kishetani.
 Ndugu, leo jitenge na uongo wote wa kishetani ulioleta vifungo kwako kutoka katika taratibu za kijamii au kifamilia au kiukoo ambazo ni za kishetani.
Inawezekana una tabia chafu ambazo umerithi kwa wazazi wako ambao nao walirithi kwa baba zao kwa vizazi vingi.
Inawezekana kwenu akizaliwa mtoto mnafanya sherehe za kipepo.
Inawezekana kwenu akizaliwa tu mtoto wa jinsia fulani kitovu anachukua bibi.
Leo toka kwenye hizo nyongeza za kishetani.

2. Kizazi kisichomcha MUNGU.
Hii ni kiini kabisa cha nyongeza nyingi za kishetani kuwekwa na mawakala wa shetani kwa watu.
Zaburi 78:8 ''Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa MUNGU.''
 Kizazi hiki unaweza kukuta mtoto akizaliwa tu anavalishwa hirizi, au bangili za kichawi, au pete za mizimu n.k.
Ni kizazi ambacho hakitaki wokovu kamwe, kimejaa ushetani tu wa kila namna.
Inawezekana ni wewe ndio unatokea katika kizazi kisichomjua YESU KRISTO kama Mwokozi na hakihusiki na kumwabudu MUNGU Baba, ni hatari sana.
Leo kwa maombi yako hakikisha unafanyika Mwisraeli wa kiroho, yaani uzao wa Ibrahimu wanaomcha MUNGU tu.
Wagalatia 3:27-29 '' Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO.  .................... Na kama ninyi ni wa KRISTO, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.''

3. Kuvamiwa na nguvu za giza.
Isaya 42:22 ''Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha. '' 
Watu waliovamiwa na nguvu za giza hao wako kwenye vifungo vya kipepo, wako kwenye magereza ya giza na watu hao ni mawindo ya nguvu za giza.
Wako watu pia nyongeza zao za kipepo zimetokana na wao kuvamiwa na nguvu za giza kisha na wao kutumia nguvu za giza ili kujaribu kutibu na kumbe ndio wanajimaliza.
Mama mmoja alianza kusumbuliwa na miguu akaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji, waganga wanamnywesha madawa na damu mbichi na baada tu ya kufanya hivyo yule mama akawa kipofu hadi leo, Maombi yangu neema ya Bwana YESU imguse lakini kuvamiwa na nguvu za giza kisha unaziendea nguvu za giza ni kuongeza matatizo na nyongeza nyingi za kishetani.
Nguvu za giza huleta vifungo vya giza.
Kuna watu tangu utotoni mwao wana mapepo au mizimu na hivyo vinawatesa sana na kuwafunga zaidi vifungo vya giza.
Hata inawezekana hata mchawi au mganga wa kienyeji ukimuuliza ilikuwaje akawab hivyo anaweza kukuambia alizaliwa hivyo, hayo ni matokeo ya kuvamiwa na nguvu za giza.
Ndugu, leo ziharibu nguvu za giza, zibomoe na kuziangamiza huku ukifuta nyongeza yote ya kishetani iliyoletwa katika maisha yako na hizo nguvu za giza.

4. Kuishi maisha ya dhambi.
Hosea 7:2- ''Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.''
Dhambi ndio ufunguo mkuu wa shetani na mawakala zake kukuvamia na kululetea nyongeza nyingi za kipepo katika maisha yako.
MUNGU anapokuwa anakukataza kufanya dhambi ni kwa faida yako mwenyewe.
 Zaburi 34:14 '' Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie. ''
Dhambi hufungulia milango ya shetani na mawakala zake kuleta nyongeza nyingi za kishetani katika maisha yako.
Ukiishinda dhambi kwa kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa YESU KRISTO hakika unakuwa umeshinda nguvu za giza kwa sehemu kubwa sana.

5. Kuyaishi makosa ya wazazi wako au mababu zako.
Hii kwa jina lingine inaitwa kuishi maisha ya dhambi ya kurithi kutoka kwa wazazi au mababu zako.
 Maombolezo 5:7 '' Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. ''
 Maisha ya dhambi za kurithi huletwa na madhabahu za giza.
Kuna watu ni walevi au wazinzi  ukoo mzima, yaani hata anayezaliwa katika ukoo huo anarithi na kuendelea na dhambi hizo.
Kumbuka ndugu kwamba shetani alizileta hizo madhabahu za giza ili watu wakose uzima wa milele, ndugu kataa kuzifanya dhambi ulizorithi kwa babau zako na haribu kimaombi madhabahu za giza zinazotesa jamii yako au familia yako au ukoo wako.
Nini ufanye kuhusu madhabahu za giza?
Kazi ni moja tu kimaombi '' Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.-Kumb 7:5''

JINSI YA KUURUDIA UUMBAJI WA MUNGU KWAKO.

1. Mpokee YESU KRISTO ili uzaliwe mara ya pili kiroho na MUNGU mwenywe.
Yohana 1:12-13 ''  Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ''

2. Kwa maombi omba MUNGU akuhamishe kutoka utawala wa giza wa kila namna uliokuwa unautumikia mwanzo, kisha omba MUNGU akuhamishie katika ufalme wa YESU KRISTO mwana wake wa pekee.
 Wakolosai 1:12-14 ''mkimshukuru Baba(MUNGU), aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru.  Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;  ambaye katika yeye(YESU) tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;''

3. Acha tabia mbaya zote.
1 Thesalonike 5:22 '' jitengeni na ubaya wa kila namna.''
Tabia mbaya ni za kishetani.
Mfano mmoja wapo, Unaweza kuwa ni mtu kujipamba sana na vipodozi vingi vya ajabu ajabu na vipodozi hivyo vinakuweka kundi walitakalo majini, maana hapo ndipo utakuwa unaendana nao hivyo baada ya muda utajikuta una nyongeza nyingi za kishetani na kumbe ni wewe ulifungau mlango huo kupitia vipodozi.
Yako mambo mengi sana ambayo ni tabia mbaya ambazo hazitakiwi kuwa kwa watu wa MUNGU.
Kujichua kwa wadada ni ushetani, punyeto kwa wakaka ni dhambi mbaya, uongo, kufanya alama za kishetani n.k ni vitu vya kuviepuka sana.

4. Hakikisha unaurudia uumbaji wa MUNGU kwa kuuishi.
Waefeso 2:10 '' Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.''
 Ishi matendo mema ambayo MUNGU aliyaumba tangu Adamu na Eva hawajakosea.
Hakikisha unalitii Neno la KRISTO.
Hakikisha unaumbwa upya katika KRISTO, mpokee na anza kuliishi neno lake huku ukiongozwa na ROHO MTAKATIFU katika maisha yako yote.

Maombi ya kuomba kuhusu somo hili.

1. Tubu kwa ajili ya kilichosababisha shetani na mawakala zake kuweka nyongeza zao kwako.

2. Haribu madhabahu za giza za ukoo zinazorithisha mabaya katika wote wanaotoka katika ukoo huo.

3. Haribu nyongeza zote za kishetani zilizowekwa na mawakala wa shetani katika  kwako.

4. Ita uumbaji wa MUNGU kwako.

5. Omba ROHO MTAKATIFU amiliki na kutawala roho yako.
Omba Neno la KRISTO lipate kibali ndani yako siku zote za maisha yako.

 Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane na nitakujulisha jinsi ya kukipata na Naamini kitakusaidia sana.
Hapa chini ni
MAOMBI YA KUFUTA NYONGEZA ZA KISHETANI KATIKA UUMBAJI WA MUNGU KWAKO.   
Maombi haya naomba yamsaidie mtu yule ambaye hajui kuomba ili katika kuomba kwa kutumia hayo basi atakumbuka mahitaji yake na kuyataja katika maombi yake. Haya hapa chini ni maombi ya kuanzia tu katika maombi yako ili uendelee zaidi kuomba
Kwa waombaji wazoefu naamini baada tu ya kulisoma somo na kulielewa basi anajua aombee nini maana alikuwa anaandika points za kuombea. Kumbuka pia fundisho ni muhimu kuliko maombi hivyo wewe ambaye huwa unahusika na maombi tu hakikisha unajifunza kwanza somo lote ndipo utapata nguvu za kuomba na kushinda.


 MAOMBI YA KUFUTA NYONGEZA ZA KISHETANI KATIKA UUMBAJI WA MUNGU KWAKO.

JEHOVAH MUNGU wetu  utukuzwe maana hakuna aliye kama wewe.
Ninakushukuru kwa ulinzi wako kwangu na ninakushuru maana ninaishi kwa ulinzi wako BWANA.
Neno lako linasema katika 1 Petro 1:5  kwamba ''Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.''
Niko mahali hapa ninatubu kwa ajili ya kila chanzo cha nyongeza ya kishetani katika maisha yangu.
Ninatubu mbele zako MUNGU wangu kwa ajili ya kila makosa yangu yaliyosababisha shetani na mawakala zake kuweka nyongeza zao kwangu.
Ninaomba msamaha mbele zako MUNGU Baba kwa ajili ya kila jambo nililolifanya katika maisha yangu hata likafungulia milango ya mawakala wa shetani kuweka nyongeza zao za kipepo kwangu.
Katika jina la YESU KRISTO ninaharibu kila madhabahu ya giza ya ukoo au jamii yangu au kabila yangu inayorithisha mabaya katika vizazi kiasi kwamba hata mimi nyongeza nyingi za kishetani ziliongezwa katika maisha yangu.
Ninaharibu kila madhabahu ya giza iliyotumika kuleta nyongeza za kishetani katika maisha yangu.
Kila madhababu ya mganga wa kienyeji au ya mchawi iliyotengeneza nyongeza za giza katika  maisha yangu, hiyo madhababu naiharibu na kuibomoa na kuivunja na kuitowesha kwa moto wa jina la YESU KRISTO aliye hai.
 Kila madhababu ya kuzimu na ya majini au wanadamu wanaotumika kipepo iliyotumika kuleta nyongeza za giza katika maisha yangu,  hiyo madhababu naiharibu na kuibomoa na kuivunja na kuitowesha kwa moyo wa jina la YESU KRISTO. Sasa
nafuta kila nyongeza ya kipepo iliyoletwa na wakuu wa giza katika maisha yangu.
Magonjwa na laana ni nyongeza za kipepo hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO ninaifuta hiyo,  nyongeza ya kishetani katika maisha yangu.
Kila ugonjwa katika mwili wangu(Utaje) ni nyongeza za kishetani, hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO ninaifuta hiyo,  nyongeza ya kishetani katika maisha yangu.
Mikosi, balaa na majanga ni nyongeza za kishetani, hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO ninaifuta hiyo,  nyongeza ya kishetani katika maisha yangu.
roho ya kukataliwa na roho za mauti zote na uharibifu ni nyongeza za kishetani,hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO ninaifuta hiyo,  nyongeza ya kishetani katika maisha yangu.
roho za umasikini, madeni dhambi ni nyongeza za kishetani, hivyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO ninaifuta hiyo nyongeza ya kishetani katika maisha yangu.
Sasa ninafuta kila sumu za kichawi nilizowahi kuchomwa na mawakala wa shetani, nazifuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila mapepo niliyowahi kurushiwa, nafuta nyongeza hizo za giza, nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila mazindiko yaliyowahi kufanyika kunihusu mimi, nafuta nyongeza hizo za giza, nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila nguvu za giza zilizowahi kuvamia maisha yangu, ndoa yangu, familia yangu, uchumba wangu au baraka yangu yeyote,  nafuta nyongeza hizo za giza, nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila nyongeza za kishetani katika  biashara zangu, mtaji wangu na kila baraka yangu yeyote,  nafuta nyongeza hizo za giza, nafuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila nyongeza ya kishetani iliyowahi kuwekwa kwangu na majini au waganga naifuta nyongeza hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila nyongeza iliyowahi kuwekwa kwangu na wachawi au mizimu,naifuta nyongeza hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila nyongeza iliyowahi kuwekwa kwangu na washirikina au waabudu shetani, naifuta nyongeza hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila nyongeza iliyowahi kuwekwa na mawakala wa shetani wa kila namna, naifuta nyongeza hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Kila ntongeza ya kishetani iliyowahi kuwekwa na wazazi au mababu katika maisha yangu,  naifuta nyongeza hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO.
Sasa katika jina la YESU KRISTO najitenga na kila nyongeza ya kichawi iliyowekwa katika maisha yangu ili initese.
Katika jina la YESU KRISTO najitenga na kila nyongeza ya kishetani iliyowekwa kwangu na marafiki wabaya.
Najitenga mbali na kila nyongeza ya kishetani iliyowekwa kwangu na wakuu wa giza, katika jina la YESU KRISTO najitenga na nyongeza hiyo ya giza.
Najitenga na kila nyongeza ya kishetani iliyowekwa kwangu na waganga wa kienyeji, katika jina la YESU KRISTO najitenga na nyongeza hiyo ya giza.
 Najitenga na kila nyongeza ya kipepo iliyoletwa na majeshi yote ya pepo wabaya, katika jina la YESU KRISTO najitenga na nyongeza hiyo ya giza.
Kila nyongeza ya giza katika maisha yangu, haijalishi nyongeza hiyo ililetwa na watu, majini au madawa, naifuta hiyo nyongeza  ya giza, naifuta kwa damu ya YESU KRISTO na katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
Ninakushukuru MUNGU Baba maana ninaamini katika wewe kwamba ni leo kila nyongeza za kishetani katika maisha yangu zimeachia na sasa niko huru kwa jina la YESU KRISTO.
Ninakushuru Bwana YESU maana katika wewe kila nyongeza ya giza imeyaachia maisha yangu, na sasa niko huru.
Asante ROHO MTAKATIFU wa MUNGU maana umenifunulia leo ushindi wangu maana kila nyongeza ya kishetani imeondoka katika maisha yangu.
Kuanzia leo sitateswa tena na roho ya mauti wala roho ya kukataliwa, katika jina la YESU KRISTO imekuwa.
Kuanzia leo sitateswa na roho za kunifilisi wala roho za kuua biashara yangu, katika jina la YESU KRISTO imekuwa.
Kuanzia leo magonjwa na laana sio sehemu ya maisha yangu tena,katika jina la YESU KRISTO imekuwa.
Kuanzia leo kila roho nyemelezi ya kishetani imetoweka na sasa niko huru katika jina la YESU KRISTO.
Ninajua nimeshinda hakika ndio maana ninamtukuza MUNGU Baba wa mbinguni.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na ninashukuru.
  Amen Amen Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen.
Hakika umeshinda. Ukiweza kufunga unaweza kufunga hata siku 1 au 3 au 4 au hata 5 au zile ambazo wewe utaona unaweza ukihusika kila siku na kipengele kuombea na kumbuka baada ya maombi ya kufunga au hata maombi ya bila kufunga fanya tendo la imani kwa MUNGU kwa kutoa sadaka nzuri itakayoambatana na maombi juu ya ukomo wa kuteswa na maadui zako katika ulimwengu wa roho
Nawaonya pia wanaotumia masomo yangu vibaya na kwa manufaa yao waache tabia hiyo.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsap).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.


Comments