WAZINZI NA WAASHERATI WATAENDA JEHANAMU.


Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.

Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno hili la MUNGU aliye hai.
Huu ni ufunuo kwa wanaofanya uzinzi au uasherati.
Dhambi ya uzinzi na uasherati ni ya kuikimbia tu na sio vinginevyo.
 
1 Kor 6:18 ''Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. ''
 
Nimewahi kuwasiliana na watu wengi wakioniomba niwasaidie jinsi ya wao kuacha kuacha uzinzi au uasherati
Mimi naamini Neno la MUNGU kwamba dhambi hii ni ya kuikimbia tu na sio vinginevyo.
Huwezi binti kusema hutaki kufanya uasherati harafu kila siku unaingia katika vyumba vya wavulana.
Huwezi kijana kusema hupendi uasherati wakati kila siku unawasiliana kimahaba na msichana.
Ndugu zangu, Mtu wa namna hiyo mimi naona anajitoa tu ufahamu maana anajua kabisa kwamba dhambi hiyo inaweza kumpeleka mtu jehanamu.

Kuishinda dhambi hii ni kuikimbia, kuiacha na kujitenga mbali na wanaotaka mwingie nao katika dhambi hiyo chafu sana.
Ndugu, ikimbie dhambi hii ya uzinzi na uasherati.
Jifunze kwa Yusufu ambaye aliikimbia dhambi hii.
 
Mwanzo 39:7-12 '' Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose MUNGU? Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye. Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani; huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje. ''

Wewe ni nani unaendelea kuikumbatia dhambi hii?
Wewe mtu wa Kanisa uliyefyatuka akili kwa sababu unaendelea na uzinzi na uasherati.
Wewe unayewaogopa wanadamu wasikuona kama umefanya uasherati na umepata mimba, hivyo umeamua kuitoa mimba hiyo ili wanadamu wakuone wewe sio mwasherati.
Ndugu, wanadamau hata wote duniani unaweza ukawaficha siri yako lakini MUNGU nakuona na usipotubu na kuacha uchafu huo ujue kuna jehanamu kwa wazinzi na waasherati.
 
Mathayo 13:49-51 ''Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. YESU aliwauliza, Mmeyafahamu hayo yote? Wakamwambia, Naam.'' 
 
Mmeyafahamu hayo yote?
Mmeyafahamu hayo yote?
Mmeyafahamu hayo yote?
Wewe ndugu ambaye kila siku unashiriki uzinzi na uasherati harafu unadanganya watu kwamba unapenda sana kuacha uzinzi na uasherati.
Uzinzi na uasherati ni kamba mbaya sana ambayo ikimfunga mtu asipopata neema anaweza kujikuta jehanamu.
Biblia inapokushauri kuikimbia dhambi hii, ndugu hakika kimbia.
 
Yeremia 23:10 ''Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.''

Wewe unayeisaliti ndoa yako. Wewe kahaba mzoefu na asiye mzoefu, Wewe mwasherati na mzinzi, wewe weweeeeeeeee
Wewe ni nani usiikimbie dhambi ya uzinifu?
Mimi nakushauri ikimbie dhambi hiyo, iache na hakikisha kuanzia leo haikuhusu tena hiyo dhambi, tubu na anza kuishi maisha matakatifu.

Hata kama wewe ni mtumishi wa MUNGU, Kama unafanya uzinzi au uasherati wewe hakika umekufa hata kama unajiona uko hai.
Wewe mzinzi unayehubiri, wewe mwasherati unayeimba kwaya au nyimbo za injili.
Wewe kiongozi Kanisani na bado umejaa uazinzi na uasherati kuanzia kichwani hadi miguuni, wewe umekufa hata kama unajiona uko hai.
 
Ufunuo 3:1 ''........ Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. ''

Ndugu ni kweli kabisa tuko katika wakati wa Neema lakini inawezekana kabisa hii ndio neema yako ya mwisho hivyo itumie kutubu, kumpokea YESU na anza kuishi maisha matakatifu.
Wote waliokufa katika dhambi na wao walikuwa na akili kama zako kwamba wataacha hiyo dhambi baadae, ndugu YESU anasema katika Mathayo 13:49-51 akiizungumzia jehanamu na mwisho akisema na walio hai leo kama wewe kwamba Mmeyafahamu hayo yote?
Mmeyafahamu hayo yote?
Mmeyafahamu hayo yote?
Mmeyafahamu hayo yote?
Ndugu, nakuomba sana sana ikimbie dhambi ya uzinzi na uasherati.
Usiwe mjinga kiroho, mwehu kiroho wala mpumbavu kiroho kwa sababu wewe ni mzinzi au mwasherati.
Nakuomba sana ondoka leo katika kifungo cha uzinzi na uasherati.
Hii ni neema ya MUNGU hata wewe ujifunze Neno la MUNGU hili.
Ujumbe mkali sana lakini ukiisikia sauti ya MUNGU ndani ya Neno hili tubu na acha uzinzi na uasherati.
Jehanamu kutakuwa na watenda dhambi akiwemo na kila mzinzi na mwasherati.
 
1 Kor 6:9 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,''
 
Chanzo kimojawapo kikuu cha mtu kufuatiliwa na roho ya mauti ni mtu huyo kuwa na tabia ya uzinzi au uasherati.

'' Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. -Ufunuo 2:11''

Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
+255786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments

EzzekyForum said…
Barikiwa sana.