UFUNUO WA ROHO MTAKATIFU NI WA MUHIMU SANA ILI USHINDE VITA YA KIROHO.

Peter na Jemimah Mabula 
Watenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki yangu.

Sitasahau siku moja usiku walinipigia simu marafiki zangu wawili wanawake waliokuwa wajawazito ili niwaombee, muda wa kujifungua umefika lakini hakuna uchungu, madaktari wamejaribu dawa za kuleta uchungu lakini haikuwezekana.

Wamama hawa wawili walikuwa maeneo tofauti tofauti na hawajuani hata kidogo ila nilishangaa walivyonijulisha kuwaombea kwa wakati mmoja wakiwa hospitali tofauti.

Nilijikuta Naomba huku natafakari na nikawa na mzigo mkubwa sana wa kuwaombea.

Ghafla nilipata ufunuo huu ambao niliuandika katika simu yangu ila Leo nimeuona kama nilivyouandika siku hiyo ambapo sasa ni zaidi ya miaka 5 tangu tukio hilo.

Wamama hao wawili wote walijifungua Salama na mmoja alijifungua mapacha. 
Yaani walipishana muda mfupi kujifungua.

◼️Nimeuona ufunuo huo nikatamani nikushirikishe na wewe ili uombe kwa MUNGU ukitumia ufunuo huo na maelekezo hayo na maandiko hayo ili kumuombea ndugu yako au rafiki yako aliye mjamzito ili MUNGU ampe kujifungua Salama.

 ◼️Au kama ni wewe mwenyewe basi muombe MUNGU katika jina la YESU KRISTO utajifungua Salama.

Ufunuo huu nilipomaliza kuuandika niliwatumia wahusika na huku na Mimi nikiendelea kuutumia kuwaombea huku nikimtaja kila mmoja kwenye Maombi yangu.

◼️Namshukuru MUNGU Sana maana aliwapa kujifungua Salama na hata sasa wanaendelea vyema.

UFUNUO HUO WA KIMAOMBI ULIKUWA NI HUU.

Nilielekezwa rohoni mwangu kwa Sauti nami nikawa natamka ile Sauti ya rohoni, ilikuwa hivi.


"Tunasimama upande wa MUNGU Wa Yasiyowezekana Kwa Mwanadamu(Yeremia 32:27).

 Rohoni Mwangu Nasukumwa Kwamba Tumwambie MUNGU Akupe Nguvu Kama Za Sarah, Rebeka, Mariam, Zipora Na Hana Za Kujifungua Salama. 
Biblia haisemi popote kwamba hao walifanyiwa operation bali Biblia inathibitisha kwamba walijifungua Salama na watoto walio hai.

Tunaita Uchungu Wa Uzazi Uliokua Umepokonywa kipepo, Uje Sasa Na Ujifungue Salama Kabla Ya Mipango Ya Kibinadamu Ya Operation. 

Tusimame Na Mathayo 7:7 Kisha MUNGU Wetu Atatukuzwa(Zaburi 50:15)

MUNGU akubariki Sana na najua Bwana YESU atakupa kujifungua Salama."

◼️MUNGU akubariki uliyepata points za kimaombi ili kumuombea mjamzito yeyote anayekuhusu.
MUNGU akubariki na kukulinda.
Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments