![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni kuhusu Ubatizo.
Wagalatia 3:27 "Maana ninyi nyote mliobatizwa katika KRISTO mmemvaa KRISTO."
◼️Kwanza ni Muhimu Mtu kumkiri YESU KRISTO kama Mwokozi kabla hata ya ubatizo.
◼️Mkristo yeyote ni lazima amkiri YESU kwa wazi.
Warumi 10:9-11 " Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika."
➡️Kubatizwa kwa maji ni njia mojawapo ya kumkiri YESU KRISTO kwa wazi.
◼️Matendo yetu yakiwa matakatifu huko ndiko kumkiri Mwokozi wetu YESU KRISTO.
◾Kuna ubatizo Wa aina mbili, ubatizo huo umebebwa na Maelekezo ya Bwana YESU KRISTO mwenyewe.
Mathayo 28:19 "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na ROHO MTAKATIFU;"
1. Ubatizo Wa maji mengi.
Warumi 6:3-5 " Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika KRISTO YESU tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama KRISTO alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa BABA, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;"
Ubatizo huu wa maji mengi una maana zifuatazo;
◼️Ni ishara ya kufa na kufufuka na YESU KRISTO.
◼️Tena ubatizo huo maana yake ni ishara ya nje ya ondoleo la dhambi.
◼️Tena ubatizo huo ni ishara ya kuachana na dunia ili uambatane na BWANA YESU.
2. Ubatizo Wa Pili ni ubatizo Wa ROHO MTAKATIFU.
Marko 1:8 "Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa ROHO MTAKATIFU."
Ubatizo wa ROHO MTAKATIFU una maana hizi;
◼️Ni ishara ya kukamilishwa Kwa mteule wa KRISTO.
◼️Ni kuingia ROHO MTAKATIFU ndani yako na kuanza kukuongoza.
◼️Ni ni nguvu za MUNGU kuingia ndani yako Kwa kiwango cha juu sana.
✔️✔️Ni Muhimu sana Kila Mkristo kuwa Mkristo aliyeokoka na amebatizwa batizo hizi mbili.
➡️Waisraeli walibatizwa katika bahari ya shamu ili wawe wa Musa, Sisi tuliookoka tumebatizwa na Bwana YESU kwa ROHO MTAKATIFU ili tuwe wa MUNGU.
➡️Ubatizo wa waisraeli ili wawe wa Musa imeandikwa hapa
1 Wakorintho 10:1-2 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;"
◼️Yohana Mbatizaji aliijulisha dunia nzima juu ya Bwana YESU kutubatiza kwa ROHO MTAKATIFU ili tuwe wa MUNGU maana ROHO MTAKATIFU ni Roho wa MUNGU.
Mathayo 3:16 ''Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa ROHO MTAKATIFU na kwa moto.''
◼️Ndugu hakikisha unabatizwa ili uwe wa MUNGU.
➡️Kubatizwa ili uwe wa MUNGU inakupasa ubatizwe kwa ROHO MTAKATIFU, na huko ndiko kuzaliwa Mara ya Pili.
Yohana 3:5-6 "YESU akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa ROHO, hawezi kuuingia ufalme wa MUNGU.
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa ROHO ni roho."
Ndugu hakikisha unazaliwa Mara ya Pili kwa kubatizwa na Bwana YESU Ubatizo wa ROHO MTAKATIFU.
◾Wako baadhi ya Makanisa hubatiza ubatizo wa maji machache au maji ya kikombe au bakuli, jambo hili kwa Wakristo ni la kulikataa daima, kwanza halifai na sio la ki MUNGU, hivyo ni Muhimu sana kubatizwa ubatizo wa maji mengi.
Nimesema hapo kwamba Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya kiroho ya kuzikwa pamoja na KRISTO na kufufuka pamoja naye, hakuna anayezikwa nusu.
Warumi 6:4 "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama KRISTO alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa BABA, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima."
◼️Sisi ni kama mbegu ni lazima mbegu hiyo uizike yote ili iote, hata Ubatizo ni kuzikwa pamoja na KRISTO ili ufufuke naye, huwezi kuzikwa kichwa tu yaani kubatizwa kichwa tu Bali ki MUNGU ni mwili mzima uzame kwenye maji.
◾Labda kwa ufupi ngoja nikuambie chanzo Cha Ubatizo fake ambao ni Ubatizo wa maji ya bakuli au kikombe.
➡️Ubatizo wa maji machache.
Huo ulianza mwaka 300 B.K na ulianzishwa na mtawala Wa Roman Empire aitwae Constantine, huyu aliwaua sana Wakristo lakini baadae alipata maadui wengine wakakaribia kumshinda ndipo siku moja usiku akaona alama ya msalaba kwenye mwezi akatambua kwamba msaada wake utakuwa Kwa KRISTO hivyo akaacha kuwaua Kanisa, lakini Kwa sababu hakuwa ameokoka akaleta sheria nyingi za nje ya Biblia katika Kanisa na viongozi wakamuogopa. Kwa kuanza tu Mama yake Constantine alipotaka kubatizwa alikataa kwenda mtoni na viongozi Wa Kanisa wa wakati ule kwa uoga wakambatiza ubatizo Wa bakuli. Mfalme alipoona kumbe inawezekana kupatizwa bila kwenda mtoni basi akapitisha sheria ya kubatizwa Kwa maji ya bakuli hadi Leo Kwa baadhi ya madhehebu lakini hiyo sio kibiblia na hiyo inaondoa maana halisi ya ubatizo wa maji.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments
Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.
Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
Nitaendelea kushukuru milele.
Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
. Usaidizi wa kurejesha ndoa
. Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
. Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
. Mwongozo na ulinzi wa kiroho
Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com