![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU.
Leo Nazungumzia mambo machache kuhusu uchumba Kisha Ndoa.
◼️Ni mpango wa MUNGU kabisa Kijana wa kiume apate Mke wake na Maisha Matakatifu ya Ndoa huku wakifanikiwa katika mambo mbalimbali.
Yeremia 29:6 "oeni wake, mkazae wana na binti; kawaozeni wake wana wenu, mkawaoze waume binti zenu, wazae wana na binti; mkaongezeke huko wala msipungue."
◼️Ni mpango wa MUNGU kabisa kwamba Binti au Mwanamke ambaye hajaolewa apate Mume safi anayefunga naye Ndoa takatifu ambaye Binti mwenyewe ndio amempenda Mwanaume huyo na kumchagua.
Hesabu 36:6 "BWANA ameagiza neno hili katika habari ya binti za Selofehadi, akasema, Na waolewe na waume wawapendao; lakini na waolewe katika jamaa ya kabila ya baba zao."
◼️Kitu Pekee ambacho MUNGU wa Mbinguni hataki ni kijana au Binti aliyeokolewa na KRISTO harafu etu akaoana wa wapinga KRISTO ambao ni waabudu miungu.
Nehemia 13:25 "Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa MUNGU, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe."
➡️Binti Usikubali kuolewa na Mtu ambaye hana Wokovu wa KRISTO, ni makosa makubwa yanayoweza kukugharimu milele kama usipopata Neema ya KRISTO.
Lengo kuu la ujumbe wa Leo ni mambo haya hapa chini.
◾Jambo la kwanza.
◼️Usahihi wa mke mwema unayemhitaji hauko katika sura yake, elimu, ukoo anaotoka au kipato chake. Usahihi wa Mke mwema unayemhitaji ni mwanamke huyo kuwa Mteule wa KRISTO anayemcha MUNGU daima.
1 Timotheo 2:10 "bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa MUNGU."
➡️Wanawake waliookoka huambatana na Matendo mema, huko ndiko hupatikana Mke mwema wako Kijana unayetafuta Mke.
◼️Usahihi wa Mume mwema wako unayemhitaji hauko katika pesa zake au kimo chake.
Usahihi wa Mume mwema wako unayemhitaji uko katika Mwanaumue Huyo kuwa Mteule wa KRISTOanayeishi maisha matakatifu.
2 Timotheo 2:22 "Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi."
➡️Mume mwema wako Binti ni yule aliyeokoka na akazikimbia tamaa za ujanani.
◾Jambo la pili
◼️Mke Mwema au Mume mwema hutoka kwa MUNGU hiyo ina maana pia kwamba hutoka katika kundi la wana wa MUNGU waliosafishwa kwa damu ya YESU KRISTO.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
➡️Kama unatafuta Mke mwema au Mume mwema mtafute kutoka katika Kundi la Vijana au Mabinti waliosafishwa na damu ya YESU KRISTO.
Kama hujui ni kwamba Mtu yeyote ambaye hajasafishwa kwa damu ya YESU KRISTO ana mojawapo ya mambo haya;
✓Tabia chafu.
✓Tamaa mbaya.
✓Kufanya Matendo mabaya sana.
✓Anateswa na nguvu za giza au anazitumikia.
✓Ana mapepo.
◼️Hivyo Tafuta mwenzi wa Ndoa Mtu aliyesafishwa kwa damu ya YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
◾Jambo la tatu.
◼️Kupata Mchumba Anayekuzidi Umri Sio Dhambi Kibiblia.
➡️Binti Wa Miaka 20 Kuolewa Na Mwanaume Wa Miaka 50 Wala Sio Makosa.
➡️Kijana Wa Miaka 20 Kumuoa Mama Wa Miaka 50 Wala Sio Makosa.
➡️Kuna Mtu Aliniuliza Kama Ni Dhambi Kuoa Au Kuolewa Na Anayekuzidi Kiumri.
Hesabu 36:6 Inasema Mabinti Waolewe Na Wanaowapenda Bila Kujali Umri Wa Hao Waliowapenda.
◼️Umri Mkubwa Wa Mtu Haumzuii Kuoa Au Kuolewa Na Mtu Mwenye Umri Mdogo Zaidi Yake.
◼️Mtu Na Aolewe Na Ampendaye
Waolewe Na Wawapendao Yaani Hata Wana Umri Mkubwa Au Mdogo.
Labda Nikupe Changamoto Zaidi.
➡️Je Ketura Mke Wa Ibrahimu Alizidiana Miaka Mingapi Na Ibrahimu Mumewe?
Ni mingi sana maana Ibrahimu alimuoa huyo baada ya Sara kufariki na Isaka mwanae alikuwa ameshamuoa Rebeka tayari hivyo wakati huo Ibrahimu alikuwa mzee sana.
Mwanzo 25:1-2 " Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura. Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua."
➡️Kwa hesabu za haraka haraka ni kwamba kama Ibrahimu alimzaa Isaka akiwa na miaka 100 na Isaka akaoa akiwa na miaka 40 basi Ibrahimu alimuoa Ketura akiwa na miaka zaidi ya 140 hivyo Wanandoa hawa walizidiana umri kwa miaka mingi sana.
Hata kwako tambua tofauti ya umri mkubwa kati ya Mwanaume na Mwanamke wanaotaka kuoana sio tatizo sio tatizo kama wanamcha MUNGU na Wanapendana.
➡️Je Boazi Na Ruthu Walizidiana Miaka Mingapi Maana Hao Ndio Waliomzaa Obedi Ambaye Naye Alimzaa Yese Mzazi Wa Mfalme Daudi, Na Katika Daudi Akaja Kutokea Mwokozi.
◼️ 1 Kor 7:2 Inasema Kila Mwanaume Awe Na Mke Wake Mwenyewe Na Kila Mwanamke Awe Na Mume Wake Mwenyewe, Hiyo Ni Kuonyesha Kwamba Mambo Ya Umri Kuzidiana Kati Ya Mume Na Mke Tunayapanga Tu Sisi Wanadamu Ila Sio Agizo La Biblia.
Kuna Mtu Alidhani Ni Dhambi Binti Kuolewa Na Mwanaume Anayemzidi Sana Umri Au Kijana Kuoa Anayemzidi Sana Umri ukweli sio dhambi.
➡️ Ila Kibinadamu tu Tunaweza Kushauriana Umri Wa Anayestahili Ila Hakuna Dhambi Katika Binti Wa Miaka 25 Kuolewa Na Mzee Wa Miaka 70 Kama Huyo Binti Amependa Mwenyewe.
Hakuna Andiko La Biblia Linaloagiza Mwanaume Kumzidi Mwanamke Umri
➡️Rika Kufanana Ni Maamuzi Ya Mhusika Mwenyewe Yaani Muoaji Au Muolewaji Ila Muhimu Ni Kuangalia Na Baadae Itakuwaje. Mfano Kijana Wa Miaka 30 Anamuoa Mama Wa Miaka 60 Huku Huyo Kijana Anataka Uzao, Je Ataupataje Uzao Kwa Mwanamke Aliyekoma Kuzaa.
Changamoto inakuwa baadaye hasa mwanaume akiwa umri mdogo aweza shawishika kwenda nje ya ndoa kwa kutamani sura changa,hili kwa tahadhari ni muhimu sana.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe.

Comments