![]() |
| Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU |
Karibu tujifunze Neno hai la MUNGU aliye hai.
Biblia takatifu iko wazi sana ikisema na moyo wa kila mwanadamu duniani kwamba ni katika YESU KRISTO pekee ndiko MUNGU Mwenyezi amejifunua, amejijulisha na kuelekeza kusudi la uzima wa milele kwa wanadamu.
YESU KRISTO ndio njia pekee ya uzima wa milele kwa agizo la MUNGU mwenyewe.
Ukimpokea YESU umempokea MUNGU.
Ukimuona YESU umemuona MUNGU.
Ukikubali kuokolewa na YESU ni hakika ya milele kwamba umeokolewa na MUNGU.
Yohana 14:6-7 "YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba(MUNGU), ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba(MUNGU); tangu sasa mnamjua, tena mmemwona."
Maana yake kupitia YESU KRISTO ndiko MUNGU amejufunua.
Sasa tena Biblia iko wazi sana ikisema kwamba asiye na ROHO wa KRISTO huyo sio wake KRISTO.
ROHO wa KRISTO ndio ROHO wa MUNGU mwenyewe, kwa jina la kipekee anaitwa ROHO MTAKATIFU.
Warumi 8:9-10 " "Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake.
Na KRISTO akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki."
Niko hapa leo ili kukufanya ujitambue kama unaye ROHO wa KRISTO.
Kama huna ROHO wa KRISTO Biblia inasema wewe sio wake KRISTO na kama wewe sio wake KRISTO basi wewe sio wake MUNGU na kwa jinsi hiyo huwezi kuingia uzima wa milele.
Neema na nafasi ya wewe kumpata ROHO wa KRISTO ipo Leo ndugu.
Kwanini tunajifunza somo hili Leo?
Ili Neno la MUNGU kwa kulitii litufanye tuwe na ROHO wa KRISTO.
Ndugu, hakikisha unahusika na ROHO wa KRISTO ili uhusike kumtii na mwisho iwe uzima wa milele.
Naomba ujikague katika mambo haya saba ya kwanza tu ya muhimu sana.
Haya mambo saba yote kwa pamoja bila kupungua hata moja yanatakiwa kuwa kwako.
Wenye ROHO wa KRISTO ni akina nani?
1. Waliomtii YESU KRISTO na kumpokea kama Mwokozi wao.
Yohana 1:12-13 " Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU."
2. Waliookoka na wanamtumikia MUNGU.
1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."
3. Wanaishi maisha matakatifu katika KRISTO.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
4. Wanaongozwa na ROHO MTAKATIFU ambaye ndiye ROHO wa KRISTO.
Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."
5. Wanaomwabudu MUNGU Baba katika roho na kweli.
Yohana 4:24 "MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."
6. Wanaolipokea Neno la KRISTO na kulifanyia kazi.
Mathayo 7:24 "Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;"
7. Wanaoishi maisha ya wokovu.
Waefeso 4:21-24 " ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika YESU, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya MUNGU katika haki na utakatifu wa kweli."
Ndugu, kufaulu kwako kiroho itategemea umeshibaje Neno la KRISTO.
Neno la MUNGU ni la muhimu sana katika maisha ya wateule wa KRISTO.
"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. -Ufunuo 2:11''
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments