![]() |
| Na. _Mwl. Nickson Mabena_ (mabenanickson@gmail.com) |
Bwana Yesu Asifiwe, somo hili limetokana na mojawapo ya maswali ninayoyapokea inbox;
Kwa hiyo nilikuwa namjibu mpendwa aliyeniuliza kwa habari ya mambo haya!.
•Ndani yangu nimehisi majibu ya swali lake, yanaweza yakakusaidia n wewe ambaye HUKUNIULIZA!.
•Yeye alitaka kujua sababu za MUNGU KUTOJIBIWA KWA MAOMBI YAKE;
Kwa mtazamo wangu, zifuatazo ni baadhi ya sababu za kutojibiwa kwa maombi yako;-
1. KUOMBA KITU NJE YA MAPENZI YA MUNGU
Biblia inasema
“Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”*
1 Yohana 5:14
-Tunaweza tukafanya MAOMBI MENGI kumuomba Mungu kitu ambacho KIPO NJE KABISA NA MAPENZI YAKE; hivyo Mungu inabidi akae kimya!.
-Kitu unachokiomba kinaweza kikawa ni KITU KIZURI SANA na WALA SIO DHAMBI KUWA NACHO, lakini KINAWEZA KUWA NJE YA MAPENZI YA MUNGU!.
~Mungu hajibu kwa sababu tu umeomba; BALI KWA SABABU UMEOMBA KITU SAWASAWA NA MAPENZI YAKE!.
2. KUOMBA VIBAYA
“Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu *mwaomba vibaya,* ili mvitumie kwa tamaa zenu.”
Yakobo 4:3
-Nia ya KUOMBA kwako inaweza ikamfanya Mungu aseme UNAOMBA VIBAYA!!
•Kumba vibaya sio kule Kuomba BILA MPANGILIO MZURI WA MANENO;
Bali ni KUOMBA ILI UPATE ULICHOKIOMBA kisha UKITUMIE KWA ‘TAMAA ZAKO’
~Nia YAKO ya KUPATA unachokiomba NI IPI?
-Ichunguze nia hiyo!.
3. DHAMBI
•Kikwazo kingine cha MAOMBI ya MTU ni DHAMBI;
“Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;
lakini maovu yenu *yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”*
Isaya 59:2
“Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.”
Yohana 9:31
~Mungu ANAWEZA AKAWA KIMYA kwa Mtu MWENYE DHAMBI!.
4. HALI YA KIROHO YA ARDHI
-Pointi hii Inahitaji maelezo kidogo, nitakuletea hapo chini; lakini tunalipata wazo hili kutokea kwenye
2NYAKATI 7:14-15
-Ardhi inapoponywa kwa MAOMBI YA TOBA YA WATU WA MUNGU, MASIKIO YA MUNGU YANAZIBUKA na KUSIKIA MAOMBI YA WAOMBAJI!.
“ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
*Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa.*”
2 Mambo ya Nyakati 7:14-15
5. KUTOAMBATANISHA MAOMBI NA SADAKA
-Hatununui Baraka ya Mungu kwa PESA YOYOTE!
-Kuna MAOMBI mengi tu Mungu ameyajibu bila SADAKA YA AINA YOYOTE ILE!
Lakini kuna WAKATI ili Mungu akupe JIBU la Ulichomuomba, anahitaji SADAKA!
-Wakati mwingine SADAKA inaweza ikawa njia mojawapo ya Kumfanya Mungu AKUPE MAJIBU YA MASWALI ULIYONAYO!.
•Kwenye Biblia tunayo mifano ya Watu waliopokea miujiza yao baada ya KUPATA MSUKUMO WA KUTOA SADAKA, WALIPOKEA MIUJIZA YAO!.
•Jambo muhimu kwako kuhusu SADAKA hiyo ni UTOE NINI pia UTOE WAPI/KWA NANI!
-Wakumbuke wanawake hawa yule MSHUNAMI na yule WA SEREPTA!
-Mkumbuke Ibrahim aliyeambiwa amtoe ISAKA!
-Mkumbuke yule Eliya alipokuwa anashindana na MANABII WA BAALI alitumia SADAKA kama kigezo cha KUMFANYA MUNGU AJIDHIHIRISHE MAHALI PALE!.
•Kuna wakati MUNGU ANAHITAJI SADAKA!.
6. UWEZO MDOGO WA KUBEBA UNACHOKIOMBA
•Mungu hataki akupoteze, anakupenda na anataka wewe uendelee KUMPENDA!.
-Huwa anajali sana pale anapokupa kitu UWE NA UWEZO WA KUKIBEBA.
•Kwenye Mfano wa Talanta najua unakumbuka jinsi mgawanyo wa zile Talanta ulivyokuwa;
Mmoja alipewa TANO mwingine alipewa MBILI na mwingine alipewa MOJA, unaweza ukafikiri kama vile MGAWAJI anapendelea!
Lakini ukweli ni kwamba mgawaji aliangalia UWEZO wao.
“Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; *kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.”*
Mathayo 25:15
~Kuna vitu ulivyomuomba Mungu hajakupa ni kwa sababu ya UWEZO WA KUVIBEBA HIVYO VITU HUNA;
Chukulia wewe ni MZAZI unayemiliki Magari na Pikipiki pale nyumbani kwako,
Siku moja Mtoto wako wa Shule ya Msingi akaja kwako akakuomba UFUNGUO WA GARI anataka aende kuwapa hai rafiki zake; JE! UTAMPA?
na kama HUTAMPA ni KWANINI?
Je! HUMPENDI MTOTO WAKO?
•Ukweli ni kwamba UNAMPENDA SANA lakini tatizo UMEJUA HANA UWEZO WA KULIMUDU GARI KWA WAKATI HUO!
-Siku akija kuwa na UWEZO bila shaka UTAMPATIA!.
Biblia inasema
“Lakini nasema ya kuwa mrithi, *wakati wote awapo mtoto,* hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote;”
Wagalatia 4:1
-Maombi mengine Mungu hawezi kukujibu anasubiri UKUE NA KUONGEZEKA UWEZO ili AKUPE kwa hiyo SUBIRI!.
•Mungu anajua kuna vitu akikupa sasa hivi; vinaweza kukupoteza kabisa na yeye HATAKI KUKUPOTEZA!.
•UKIKUA ATAKUPATIA!.
7. UPUNGUFU/KUKOSEKANA KWA IMANI.
-Ningeweza kukuwekea somo linalojitegemea kuelezea UHUSIANO ULIOPO KATI YA KUJIBIWA MAOMBI na IMANI;
Lakini hapa Kazi yangu ni ndogo tu, kukuambia kuwa KUKOSEKANA au KUPUNGUA kwa IMANI ni sababu mojawapo ya KUTOJIBIWA kwa maombi!
•Mitume walimshuhudia Yesu akimtoa PEPO wa Kifafa kiulaini tu; wakati wao walihangaika sana kumtoa pepo huyo huyo lakini WALISHINDWA!
-Baada ya HUDUMA ile, wakamfuata Yesu faragha!
“Kisha wale wanafunzi wakamwendea Yesu kwa faragha wakasema *Mbona sisi hatukuweza kumtoa?”*
Mathayo 17:19
Jibu la Yesu ndio linatupa sababu hii;
”Yesu akawaambia, Kwa *sababu ya upungufu wa imani yenu.* Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.”
Mathayo 17:20
Tafsiri zingine zinasema KWA SABABU YA KUTOKUAMINI..
Kwa hiyo, sababu mojawapo ya kutojibiwa maombi yako ni UPUNGUFU WA IMANI au KUKOSEKANA KWA IMANI!.
8. KUTOKUWA NA BIDII YA KUOMBA
~Kwa mwenye haki kuomba bila BIDII inafaa kidogo;
Biblia inasema
“Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. *Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.”*
Yakobo 5:16
-Kwenye mstari unaofuata tunapewa Mfano wa MTU ALIYEOMBA KWA BIDII;
“Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, *akaomba kwa bidii* mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.”
Yakobo 5:17
•Ukitaka kuijua BIDII aliyoionyesha ELIYA unapaswa kurudi kwenye kitabu cha Wafalme!
*(1 FALME 18)*
•Wakati mwingine kushindwa KUOMBA KWA BIDII, kunaweza kukawa KIKWAZO CHA KUPATA MAJIBU YA MAOMBI YETU!.
9. KUISHIA NJIANI
•Kuna MAOMBI mengine yanahitaji muendelezo, yaani siku ya kuacha kuomba ni siku ile ambayo unachokiombea kimefanyika Sawa na maombi yako!
•Nikupe Mfano hapa, unakumbuka Musa alipowachukua Haruni na Huri wakapanda Mlimani ili Wamuombee Yoshua aliyeenda kupigana vita?
Siku ambayo Musa alipaswa ku-stop KUOMBA ni SIKU YA YOSHUA KUMALIZA VITA!
-Kwa Bahati mbaya sana, Musa ALICHOKA KABLA ya VITA KUISHA kwa hiyo MAOMBI yake hayangefanikiwa endapo ANGEISHIA NJIANI!
•Bahati njema kwake alikuwa na ‘SAPOTAZ’, watu waliohakikisha MUSA ANAENDELEA NA MAOMBI HADI VITA IISHE;
•Unawahitaji Hawa watu, WATU WA KUKUINUA MIKONO PALE UNAPOCHOKA KUOMBA!.
•Ukiishia NJIA utashindwa vita, alafu utabaki unajiuliza KWA NINI HUJAPATA MAJIBU YA MAOMBI YAKO!.
10.UJINGA WA MUOMBAJI
•Kuna WAKATI Mungu anakuwa AMEJIBU kwa namna ya KUTOA MAELEKEZO kwa Muombaji, endapo Muombaji huyo HAJUI KWAMBA AMEPEWA MAELEKEZO ya jinsi ya KUPATA MAJIBU YA MAOMBI YAKE basi atabaki kama vile HAKUWAHI KUJIBIWA!.
Tazama hapa
“Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
*Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao.”*
Zaburi 107:19-20
~Hawa watu wameingia kwenye MAOMBI kwa ajili ya Kupeleka mahitaji yao kwa Mungu, Mungu aliyasikia MAOMBI yao HAKULETA WALICHOMUOMBA bali ALILITUMA ‘NENO’ LENYE MAJIBU YA MAJIBU YA MAOMBI YAO!
Mfano, unaweza ukafunga na Kuomba ili Upate KAZI na Mungu anasikia kilio chako; badala ya KUKUPA KAZI yeye ANAKUPA NENO ambalo ndani yake KUNA MAELEKEZO na MAELEKEZO hayo UKIYAFUATA unaipata ILE KAZI ULIYOIOMBA!.
•Yesu alituambia wanafunzi kuwa
“Ninyi mkikaa ndani yangu, na *maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”*
Yohana 15:7
Sababu mojawapo ni kwamba, AKIJIBU KWA NJIA YA KULITUMA NENO LAKE basi TUELEWE KUWA NI YEYE AMESEMA!.
•Changamoto inakuja pale UNASIKIA alafu HUELEWI chochote!
Na usipoelewa ADUI ANAPATA NAFASI YA KUNYAKUA MAJIBU HAYO;
“Kila mtu alisikiapo neno la ufalme *asielewe nalo,* huja yule mwovu, akalinyakua lililopandwa moyoni mwake. Huyo ndiye aliyepandwa karibu na njia.”
Mathayo 13:19
~Vuta picha NAAMANI asingeelewa alivyoambiwa AKAJICHOVYE KWENYE MTO MARA SABA!
~Vuta picha endapo wale Wakoma wangeendelea kukomaa mbele za Yesu wakihitaji UPONYAJI wakati NENO LIMESHATOA MAELEKEZO kwamba WAKAJIONYESHE KWA MAKUHANI!.
•Wengi wetu MAELEKEZO yanapokuja tunashindwa kuhusianisha na TULICHOKIOMBA hivyo tunakuwa kama vile watu ambao HATUJAJIBIWA!.
•Roho Mtakatifu anaweza akakupa MAELEKEZO maalumu,
Mfano; Uombeje, Ufanyeje, Utoe SADAKA, Umpe nani hiyo SADAKA, Umshirikishe Mtumishi gani n.k
~Usipofuata hayo MAELEKEZO unaweza ukadhani HUJAJIBIWA!
•Naamani ALITAKA awekewe mikono lakini MAELEKEZO yaliyotoka anatakiwa kwenda YORDANI.
“Lakini Naamani *akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania,* Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.”
2 Wafalme 5:11
Unaweza UKAFIKIRI UNATAKIWA KUTOA SADAKA kumbe Mungu anakutaka UFUNGE SIKU KADHAA (Sawa na MAELEKEZO)
-Ukienda NJE ya MAELEKEZO basi HUPATI MAJIBU!
•Kwa kukusidia zaidi hapa, ngoja nikupe ushuhuda mmoja!.
•Jamaa mmoja alikuwa ana taaluma ya U-INJINIA (Civil Engineering);
Alikuwa ni Mtaalamu Kwenye MAMBO YA UJENZI,
Pamoja na TAALUMA hiyo lakini HAKUWA NA KAZI na wala hakuwa anapata MADILI!
•Alikuwa anahangaika sana kupata Kazi, akatuma Maombi mengi ya Kazi lakini HAKUPATA KITU!
~Ikabidi aende kwa Mtumishi mmoja ili amuombee, baada ya Maombi ya Mtumishi huyo; Mtumishi AKAPEWA MAELEKEZO NA ROHO MTAKATIFU,
Kwamba watafute mahali ambapo watu WANAJENGA KANISA alafu huyo INJINIA AENDE KUTUMIA *UFUNDI WAKE BILA MALIPO YOYOTE*;
Basi Mtumishi akampa hayo MAELEKEZO yote INJINIA. Bila MASHAKA INJINIA akakubali!
•Wakatafuta hadi wakapata mahali ambapo KUNA UJENZI WA KANISA;
-Wakamtafuta Mchungaji wa mahali hapo, wakajitambulisha na kueleza kilichowapeleka pale!
Mchungaji akaogopa sana, na kuanza kujieleza kwamba wana UPUNGUFU wa fedha hivyo hawataweza kumlipa INJINIA HUYO, lakini yeye akasema wasijali kwani ATAFANYA BURE, BILA MALIPO YOYOTE;
Basi ALIKAMLISHA NA KANISA LIKASIMAMA!.
Baada ya hayo, hakikupita kipindi kirefu AKAPATA KAZI na MADILI KIBAO!.
👆🏻Huyu asingepata haya MAELEKEZO, angezamia mifungo na kuwekewa mikono hadi basi na ASINGEPATA MAJIBU!.
~Niseme na MTU hapa MWENYE UJUZI FLANI NA UNATAFUTA AJIRA, pengine haya ni MAELEKEZO ya ROHO MTAKATIFU kwako, kwanini USITAFUTE SHULE UFUNDISHE HATA BURE IWE SADAKA YAKO KWA BWANA?
•KWA NINI USITAFUTE MAHALI UKAUTUMIE UJUZI WAKO HATA BILA MALIPO?
-KAMA NI WEWE NINAYESEMA NAWE, BASI NENDA KATUMIE KIPAWA, ELIMU, HUDUMA, UJUZI WAKO HATA BURE KAMA SADAKA YAKO KWA BWANA.. NAYE ATAKUFUNGULIA MILANGO YA AJIRA UNAYOITAKA!!.
*NIMEMALIZA*
Mwl. Nick
0712265856
(WhatsApp#)
©Kagera, Nchi ya Maziwa na Asali.

Comments