![]() |
| Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe sana ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Je umeshampokea YESU KRISTO kuwa Mwokozi wako?
Je unajua kwamba YESU KRISTO alikuja ili akuhamishe wewe kutoka kwa shetani na sasa uwe kwa MUNGU?
Je umeshahamishwa kweli?
Ngoja niseme haya yafuatayo ili unielewe nazungumzia nini; Mtu anayehamishwa hakai katika eneo la awali tena.
Ukihamishwa nina hakika utaenda kule ulikohamishiwa.
Mfano
Ikiwa uko Comoro kisha ukapata uhamisho uhamisho wa kwenda Canada hakika utaenda kuishi Canada. Haiwezekani wewe uko China uhamishiwe Chile kisha uwe unakaa China lakini kisha asubuhi unachukua usafiri kwenda Chile Kazini, haiwezekan.
Mtu anapohamishiwa eneo jingine haitakiwi tena kuendelea kuishi katika eneo la kwanza.
Mtu anapohamishwa huhama hakika.
Sasa tunapompokea YESU kama Mwokozi hapo tunakuwa tumetoka ufalme wa Giza na kupelekwa ufalme wa MUNGU.
MUNGU ndiye anayetuhamisha kutoka kutawaliwa na shetani na sasa tunaanza kutawaliwa na YESU KRISTO.
Ndugu ukiokoka hakikisha umehama kweli kweli kutoka ufalme wa giza na sasa kaa katika ufalme wa nuru yaani ufalme wa YESU KRISTO.
Wakolosai 1:13 " Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;"
Mtu aliyehamishwa kutoka uzinzi au uasherati haimpasi tena kubaki katika uzinzi na uasherati.
Mtu aliyehamishwa kutoka dhambini hakai dhambini tena.
Ndugu hakikisha umehamishwa na MUNGU kutoka kwa shetani na sasa uwe katika YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
Ikiwa sasa uko katika YESU KRISTO hakikisha unatembea katika nguvu za MUNGU.
Waefeso 6:10 " Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake."
Ni muhimu sana kutembea katika nguvu za MUNGU.
Ukishahamishwa kutoka kwenye dhambi haikupasi tena kuendelea na dhambi.
Ulikuwa kahaba, unapookoka unahamishwa kutoka ukahaba hivyo usiendelee na dhambi hiyo tena.
Ulikuwa mwizi, muongo, tapeli, mlevi au mchawi lakini ukapata Neema ya Wokovu wa Bwana YESU hivyo haukupasi sasa kuendelea na dhambi.
Biblia inasema ukihamishwa na YESU KRISTO hakikisha unaishi maisha matakatifu kama yeye Bwana YESU alivyo mtakatifu milele.
1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
Hakikisha tu umehamishwa na anza sasa kutembea katika nguvu za MUNGU.
Kwanini tuwe na nguvu za MUNGU?
1. Tunapata nguvu za MUNGU kwa sababu tumeumbwa kwa mfano wa MUNGU ili pia tumiliki na kutawala.
Mwanzo 1: 26 '' MUNGU akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. ''
2. Tunashiriki utawala wa MUNGU, tu sehemu ya ufalme wa MUNGU.
Matendo 1:8 '' Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu ROHO MTAKATIFU; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi. ''
3. Tunalindwa na nguvu za MUNGU.
1 Petro 1:5 '' Nanyi mnalindwa na nguvu za MUNGU kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho. ''
Ndugu hakikisha umehama mazima kutoka kwa shetani na sasa ukiwa katika KRISTO YESU hakikisha unatembea katika nguvu za MUNGU na hakikisha unajua jinsi ya kupigana vita ya kiroho maana unao maadui katika ulimwengu wa roho wanaojaribu kukudhuru au kukuharibia.
Waefeso 6:12 '' Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. ''

Katika kupigana vita ya kiroho ukiwa katika wokovu inakupasa sana pia kuwa na bidii katika MUNGU.
Bidii yako kwa YESU itakufikisha kwenye ushindi mkubwa.
Bidii yako katika utakatifu katika KRISTO itakufikisha uzima wa milele.
Juhudi yako katika kazi ya MUNGU itakufunguliwa milango mingi ya ushindi maishani mwako.
Warumi 12:11-13 " kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia BWANA; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi."
Wewe unatembea katika nguvu gani?
Mimi nakushauri tembea katika nguvu za MUNGU, ngoja nikujulishe aina ya nguvu anazoweza kuwa nazo mtu.
Aina 4 za nguvu anazoweza kuwa nazo mwanadamu.
1. Nguvu za MUNGU.
1 Mambo ya " Nyakati 16:11 " Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote."
2. Nguvu za madaraka anayopewa mtu.
Walawi 25:43 " Usitawale juu yake kwa nguvu; ila umche MUNGU wako."
2. Nguvu za mwili.
Kumb 34:7 "Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka."
4. Nguvu za shetani.
Ufunuo 13:4 " Wakamsujudu yule joka(shetani) kwa sababu alimpa huyo mnyama(utawala wa kishetani) uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?''
Nimekujulisha hayo ili nikushauri ndugu yangu.
Ushauri wangu ni huu tafuta nguvu za MUNGU kwenye maisha yako yote.
Usipoteze muda kutafuta nguvu za mwili au za madaraka au nguvu za kishetani Bali tafuta nguvu za MUNGU, kama kweli unatakiwa kuwa mshindi siku zote dhidi ya nguvu za giza.
Nguvu za MUNGU zina ROHO MTAKATIFU katika KRISTO YESU Mwokozi.
Bwana YESU mwenye nguvu na mamlaka yote anathibitishwa na Biblia .
Mathayo 28:18-20 " YESU akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari."
Ndugu tafuta nguvu za MUNGU.
Nguvu za MUNGU zinapatikana kwa wewe kukaa katika kusudi la MUNGU, wewe kuishi maisha matakatifu ya Wokovu, wewe kuwa muombaj na mtoaji, wewe kutembea kwenye Neno la MUNGU na wewe kumtii ROHO MTAKATIFU.
Wakati mwingine inakubidi ubadilike katika kufikiri, ndipo ulielekee kusudi la MUNGU.
Katika vita ya kiroho kuna mambo husababisha muombaji kushindwa katika vita ya kiroho anayopigana.
Mambo mawili kati ya mengi ambayo huwa kizuizi cha kushinda vita ya kiroho ni haya;
1. Katika vita ya kiroho watu wengi hushindwa kumjua hasa adui halisi unayepigana nao, ndio maana hawashindi vita ya kiroho.
Ni vigumu sana kushinda vita kama humpigi adui yako kiroho.
2. Hofu.
Hofu huleta woga, kuchanganyikiwa.
Hofu huondoa kukua kwako kiroho.
Usikubali uoga ukashika maisha yako.
Uoga ni moja ya silaha kubwa zaidi za mawakala wa shetani wanaotumia ili kukushinda kiroho.
Hakikisha unakuwa mtu wa imani maana imani huondoa uoga wote.
Isaya 54:14 " Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia."
Unapojifunza na kutii mambo ya ufalme wa MUNGU wakati mwingine unaweza usione matokeo kwa wakati huo, lakini ukizingatia utapata matokeo mazuri sana baadae. Mimi nakushauri kwamba endelea kumngoja MUNGU kwa maombi na utakatifu.
Zaburi 27:14 " Umngoje BWANA, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA."
Endelea mbele na Wokovu, mtii Bwana YESU na Neno lake, enenda katika ROHO MTAKATIFU na siku moja utamuona MUNGU akibadilisha historia ya maisha yako.
Zaburi 37:3-6 " Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu. Nawe utajifurahisha kwa BWANA, Naye atakupa haja za moyo wako. Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya. Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama adhuhuri."
Endelea mbele kwa maombi na utakatifu katika KRISTO.
Vumilia katika YESU KRISTO hata mwisho maana utukufu ujao ni mkuu sana.
Zaburi 37:34 " Wewe umngoje BWANA, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona."
Sasa ili kujua jinsi ya kupigana viya ya kiroho, inakupasa kuzingatia mambo haya;
1. Hakikisha una Neno la MUNGU ndani yako ili Neno hilo alitumie ROHO MTAKATIFU kukujulisha nini cha kufanya kinachotokana na Neno la MUNGU ili ushinde vita ya kiroho.
Wakolosai 3:16 '' Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. ''
2. Enenda kwa ROHO MTAKATIFU.
1 Kor 2:10 '' Lakini MUNGU ametufunulia sisi kwa ROHO. Maana ROHO huchunguza yote, hata mafumbo ya MUNGU. ''
3. Uwe mtu wa maombi mara kwa mara ili hali hiyo ikufanye uwe na uzoefu wa kudumu wa kuomba, na kwa jinsi hiyo utakuwa na ufunuo mwingi wa maombi utakaokufanya uwe muombaji unayeshinda.
1 Thesalonike 5:17 '' ombeni bila kukoma; ''
4. Uwe thabiti katika Imani huku ukimpinga shetani na mawakala zake.
1 Petro 5:9 ''Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. ''
5. Uwe mtoaji ambaye matoleo yako yanaambatana na maombi.
Mithali 11:24 '' Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. ''
Andiko hili katika tafasiri ya BHN Biblia inasema hivi ''
Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika; lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini.'' Hivyo hapo utakuwa umeelewa maana ya Mithali 11:24 Kwenye Biblia yako ina maana gani.
Ukitimia katika hayo matano itakuwa rahisi kwako kupigana vita ya kiroho na kushinda.
Unatakiwa uwe unaomba maombi ya ufunuo kama ROHO wa MUNGU anavyokufunulia ndipo utashinda vita ya kiroho kirahisi sana.Siku moja mimi nilikuwa kwenye gari nikisafiri lakini nilijikuta katika nguvu za MUNGU na kuomba maombi yafuatayo, baada ya kuona vita kali ya kiroho inanikabili.
Niliomba maombi haya huku nikitamka moyoni hivi huku nikiandika kila ninachoomba;
"Eee MUNGU Baba wa mbinguni naomba kwa Neema yako kwamba Malaika wako wawawekee alama wachawi wote wanaotaka kuja kwangu, wakuu wa Giza wote wanaotaka kufanya chochote kwenye baraka zangu au maisha yangu, majeshi ya pepo wabaya wote wanapanga lolote kuhusu Mimi. Eee MUNGU Muumbaji wangu ninaomba Malaika zako wawawekee alama maadui zangu hawa. Na kisha Eee JEHOVAH MUNGU wangu, kwa sababu wapo pia Malaika zako wengi kwangu, ambao kazi zao ni kunihudumia kama Waebrania 1:14 inavyosema, kazi yao nyingine Malaika zako kwangu ni kunilinda na kuniokoa kama Zaburi 91:11 inavyosema, tena Malaika zako hufanya kituo cha kudumu kwangu kama Zaburi 34:7 inavyosema, basi Eee MUNGU Muumbaji wangu ninaomba maadui ambao wameshawekewa alama tayari basi kila wakikaribia kwangu, Malaika zako wanaziona zile alama na kuwakatilia mbali na kuwaangamiza. Najua Malaika zako hufanya kazi ya kuwaangamiza maadui za wateule wako kama Zaburi 35:1-8, basi maadui zangu wenye alama Malaika zako Bwana YESU wawashambulie maadui zangu hao maana wana alama tayari.
Biblia inasema utakusudia jambo jema mteule nalo litakuwa(Ayubu 22:28) basi sina wasiwasi maana maajenti wa kuzimu sasa wameshawekewa alama na Malaika za MUNGU Baba na wakisogea tu kwangu au kwa familia yangu au kwa baraka zangu hakika watawakuta Malaika wa MUNGU wa kuwapiga. Najua kabisa MUNGU Baba ni ahadi yako kuwaua nyoka mwepesi, nyoka wa kuzonga zonga, nyoka aina ya lewiathani na yule joka kama Neno lako linavyosema katika Isaya 27:1, Eee MUNGU wangu naomba uwaue Leo katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai"
Nini kilinisaidia kuomba maombi hayo na kushinda vita ile ya kiroho?
Ni rahisi tu kwamba Nilikuwa na Neno la MUNGU moyoni mwangu, nilikuwa na ROHO MTAKATIFU, Nilikuwa na imani n.k
Hata wewe ni muhimu ukazingatia ujumbe wa leo katika kushinda kwako vita ya kiroho.
Kuna maandiko ndani ya maombi yangu na hiyo ilitokana na kusoma sana Biblia na kutumia maandiko kwenye maombi yangu, njia kama hiyo inaweza kukusaidia katika vita ya kiroho unayopitia.
Inawezekana maombi yangu yatakupa mbinu za ki maombi, au labda ujumbe huu utakutia moyo n.k
Labda ujumbe utakupa hasira za kiroho ili maombi yako ya Leo yapeleke uangamivu mkubwa sana kwa mawakala wa shetani waliokutesa muda mrefu.
Kuna watu wakipata hasira za kiroho wanaweza kuomba hadi kilugha chao lakini katika jina la YESU KRISTO na maadui zao wanaipatapata.
Kwa lugha yako hiyo hiyo unaweza kumuomba MUNGU katika jina la YESU KRISTO na akakutendea muujiza .
Mama mmoja katika maombi alikuwa anaomba kwa kiswahili lakini hasira ya kiroho ilipoongezeka ndani yake alianza kuomba kwa kutumia lugha ya kabila lake lakini katika jina la YESU KRISTO.
Ndugu sijui ujumbe huu utakuongezea nini katika maombi yako dhidi ya wakuu wa Giza, katika jina la YESU KRISTO hakika ushindi upo, haijalishi maadui zako ni wengi kuliko nywele za kichwa chako.
Zaburi 69:4 ''Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. ''
Pigana vita ya kiroho kimaombi na hakikisha unashinda.
Natamani niseme mengi mno lakini naamini mwenye kuelewa ameelewa.
MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
+255714252292(Hadi whatsapp).
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments