MTU ANAYEISALITI NDOA YAKE AACHE KUFANYA HIVYO KUANZIA LEO

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 





Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.

Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."

◼️Ndoa inatakiwa kuheshimiwa na walio ndani ya Ndoa hiyo na hadi walio nje ya Ndoa hiyo.
Heshima kuu ya kuiheshimu Ndoa ni kutokumsaliti mwenzi wako wa Ndoa.

◾Mtu anayeisaliti Ndoa yake anatakiwa kujua mambo haya muhimu sana kwake.

1. Wazinzi na waasherati wataenda jehanamu.

1 Wakorintho 6:9 "Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,"

◼️Tubu na acha dhambi hiyo Mara moja.

2. Mtu anayezini hana akili kabisa na anafanya kosa litakalomwangamiza yeye mwenyewe.

◼️Ndivyo Biblia inavyosema.
Mithali 6:32 "Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake."

3. Uzinzi na uasherati huunajisi/huuchafua mwili wote kiroho.

◼️Ndio Biblia inavyosema
1 Wakorintho 6:18 " Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."

4. Kufanya ngono na mtu asiye mwenzi wako wa ndoa ni kukaribisha roho ya mauti.

 Walawi 20:10 " Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa."

5. Utakaribisha mapigo ya MUNGU kwako.

2 Samweli 12:9 -10 "Kwa nini umelidharau neno la BWANA, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni. Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako."

➡️Ndugu, kama wewe ni msaliti wa Ndoa yako tubu na kuacha dhambi hiyo.

➡️Kama wewe ni mwasherati tubu na acha dhambi hizo.

"Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo ROHO ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. -Ufunuo 2:11''
Asante kwa kujifunza Neno la  siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments