SHUHUDA BAADA YA KUFUNDISHA SOMO LA KUKEMEA UZINZI NA UASHERATI

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Baada ya kufundisha somo la kukemea uzinzi na uasherati nilibata shuhuda kadhaa na hizo nakuletea hapa, naamini kuna kitu utajifunza maana tuko siku za mwisho na baada ya kifo ni hukumu.
 Waebrania 9:27 '' Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; ''
Somo lililotengeneza shuhuda hizi ni hili FUNGUA HAPA

1. USHUHUDA BAADA YA KUFUNDISHA SOMO KUHUSU UZINZI NA UASHERATI.
Mch Mabula Bwana Yesu Asifiwe maana sijapata kuona maonyo Kama hayo maana yangekuwa makanisani ndio mafundisho watu wengi tungekuwa Na mwelekewo wa maisha ya mafunzo mazuri ya Mungu. Kwa sasa wengi wanaenda makanisani kutokana Na Hali ngumu kwa hiyo wanaenda ili wafanikiwe Na si vinginevyo, ndivyo tulivozoeshwa na wachungaji wetu pia maana tunatizama sana yanayoonekana kwa macho Na yaliyo mazuri machoni kwetu. kwa mawazo yangu kwanza nikusifu kueleza ukweli uliyo ndani ya makanisa, kwa hilo tu kwanza umegusa maeneo mengi mno Maana Dunia imetawaliwa uzinzi pamoja Na yote yanayo ambatana Na hilo harafu kinachofuata Fedha Na Mali swala la kuhusu mbinguni mwanadamu ni mpaka akwame au kuumwa au anakaribia kufa kwa kweli nahisi mafundisho ya sasa ni kuhusu tu mafanikio Na wala si swala la safari ya mwisho. Asante sana kwa masomo yako maana hata mimi sasa inabidi nijiulize Niko wapi. ningependa sana unitumie mafundisho zaidi, ni kweli najiona nina Dhambi sana naitaji kutubu upya unenigusa sana sana pia kuna haja ya kuomba kwa ajili ya wengine ubarikiwe sana.



2. USHUHUDA WA JINSI ALIVYOLIPATA SOMO LINALOKEMEA UZINZI NA UASHERATI.
Mchungaji Mabula hii kwangu ni Kama kitu kimenichanganya sana mpaka sasa hata sielewi kabisa maana nilikuwa natoka Arusha nikiwa Na mtoto wangu Na mke wangu nikampatia mama mmoja lifti njia panda ya Moshi.
wakati tukiwa safarini tuliongea mambo mengi sana lakini yalikuwa ni wa Biashara Na wala sio mambo ya Dini Na mwisho tukakubaliana nae kuwa tutajaribu kumletea mzigo trip ya mwisho tukitoka Nairobi. cha kushangaza tukapoteza mawasiliano nae, nayo ilikuwa mwaka juzi. Baadae nikaanza kuona sms katika whatsapp yangu za mambo ya Mungu ni kajua ni za kawaida Na sikutaka kumjua ni Nani aliyenitumia ila kila akituma Na Mimi nasoma na kumjibu namwambia "Amina" ila Leo. ndio katuma ujumbe wa ajabu. Kanitumia somo lako. Ilikuwa hivi Leo nilikuwa Na stress sana nikawa natafari maisha yangu nikajiona sifai mbele ya Mungu kwa mengi sana ghafla ujumbe whatsap ukaingia kwenye simu yangu, yaani nilivyoanza kusoma somo hilo linalonikemea kuhusu uzinzi nikaona Giza ghafla Na mapigo ya moyo yakaenda mbio, nikashindwa kumaliza kusoma somo hilo, ikabidi nivute pumzi kwa muda, Baadae nikaweza kuisoma nikiwa nimetulia Na akili timamu. Mchungaji hauwezi kuamini ilibidi nimpigie simu yule Dada ni muulize wewe ni Nani mwenzangu uliyo nitumia somo hili.
Mchungaji hakunijibu kama ninavyoitaji maana nilikuwa bado sijamjua lakini kwenye hayo maneno ya Mungu aliyonitumia kulikuwa Na namba elekezi za mlengwa aliyeandika somo ambaye ni wewe ndio nikakupata mchungaji. nitashangaa sana Kama watu hawata Respond mafundisho yako hata pia sitashangaa watu waki Respond maana umeongelea ukweli wa ndani sana wa sasa uliopo ndani ya maisha yetu sasa!!!
Inaniuma sana nikijiangalia inawezekana usijijue ukawa ni mfuata mkumbo wa maisha ya sasa, lakini kwa mafundisho haya najiona mtupu kweli kweli hata ipigwe parapanda sitakuwemo kwenye Safari hiyo ya uzima wa milele, ni mengi mabaya kwenye mikono yangu , Akili yangu mawazo yangu Na Nafsi yangu pia najiona Sina chochote kwa Mungu wangu ni kilio cha ndani ya roho yangu. Mimi mwenyewe naitaji kutoka hapa nilipo, miaka mingi ya umri niliyokuwa nayo sasa ningependa kufanya kitu ambacho kingemfurahisha Mungu Na si vinginevyo. naomba nifundishe hata namna ya kulijua neno la Mungu kwa umri niliokuwa nao hata Bible sijui kuisoma nasoma Kama kitabu cha hadithi nikimaliza hapo nasahau kila kitu .
Asante sana kwa kunipiga shoti kichwa changu ili nikae sawa kwa Yesu . namshukuru pia yule Dada niliye mpa lifti ndie amenitumia somo lako WhatsApp na kunifanya nikufahamu
Mimi naishi Arusha Nina mtoto mmoja Na mke wangu yeye ni mama wa Nyumbani ila alipata ajali mbaya Na sasa nimlemavu wa viungo. karibu sana Arusha Mchungaji Mabula. samahani nafikiri ujumbe wangu nimeuandika bila hata kuangalia Makosa ya herufi ila najua utanielewa Na naomba tu iwe hivyo Asante sana na Mungu akubariki Sana.





3. BAADA YA SOMO LA KUKEMEA UZINZI NA UASHERATI NILIENDELEA KUPATA SHUHUDA.
Huu ni ushuhuda mwingine.
"Shalom Mtumishi, Bwana Yesu akubariki sana kwa somo ulilofundisha kwenye Facebook kuhusu kanisa. Kwanza ilikuwa ni mida ya saa tatu kasorobo nilikuwa na binti mmoja tukiwa tunaelekea jikoni kupika chakula, nikaingia fb kitu cha kwanza nimekutana nacho ni hilo somo lako. Niliposoma tu kichwa cha habari nikamwambia yule binti kabla hujachukua sufuria ya kupikia sikia huu ujumbe wa Mungu. Kasema sawa nikasoma kama ilivyoandikwa ,cha ajabu ikawa yeye kila nikitaja kipenge kimoja ananiambia kuwa kanisani kwao hayo yote yanatendeka sana, tukasoma ujumbe mpaka mwisho nikagundua ya kuwa hata kanisani kweli ninapoabudu hayo yote ni kweli yanafanyika tena kwa waziwazi. Yaani kwa kweli Mungu azidi kukulinda na azidi kukutumia kuwafungua wengi kwa neno lake la kweli. Pia ninakuomba kibali cha kukopi kwenye daftari huo ujumbe kama ulivyoandikwa ili nikipewe nafasi ya kusimama madhabahuni kanisani kwetu nichukue hilo somo na kuwafundisha, maana huyo ujumbe umelilenga kanisa letu moja kwa moja. 


Ubarikiwe sana Mtumishi na rafiki yangu Peter M Mabula.

Comments