USIMPE NAFASI SHETANI KATIKA MAISHA YAKO.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi 



Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.

◼️Katika Maisha Yako yote usimpe nafasi shetani kwa lolote.

➡️Njia ya shetani ni njia ya jehanamu na mipango yake yote anayoipanga kuhusu wewe ni ili uende jehanamu kwa sababu yeye anajua kwamba anasubiri tu hiyo  jehanamu.

Ufunuo 20:10 "Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele."

 ◼️Kwa kulijua hilo Biblia inakutaka ufanye jambo hili kuhusu shetani kwamba usimpe nafasi kamwe katika maisha yako.

Waefeso 4:27 " wala msimpe Ibilisi nafasi."

➖Ukimpa nafasi shetani katika maisha yako ujue anataka uende na wewe jehanamu.

➖Shetani ni wa jehanamu hivyo usikubali kufanya naye kazi yeyote ile.

Kwa Njia gani watu humpa shetani nafasi?

1. Kwa Mtu kuamua kumkataa YESU KRISTO kuwa Mwokozi wake yaani kukataa kuokoka 

Yohana 3:16-18 " Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye(YESU) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU.

◼️Shetani alishahukumiwa tayari, anasubiri tu kuanza adhabu yake isiyobadikika, hivyo na watu wanaomkataa YESU KRISTO kama Mwokozi wao Biblia hapo juu inasema wamekwisha hukumiwa kwa tendo hilo hivyo kwa sababu ya Neema inawapasa Sasa waokoke ili kufuta hiyo hukumu ya MUNGU juu yao.
Ndugu, unamhitaji YESU KRISTO ili upone dhidi ya jehanamu.

2. Kwa Mtu kuabudu miungu.

Kumbu 13:6-8 " Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako; katika miungu ya mataifa yaliyo kando-kando yenu karibu nawe au mbali nawe, tokea ncha moja ya dunia hata ncha ya pili ya dunia; usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;"

◼️ Ndugu, Usikubali Mtu yeyote Duniani akushawishi kuabudu miungu, hata kama ni mzazi wako au ni Mtu wa thamani sana kwako.

◼️◼️Wa kumwabudu ni MUNGU Baba wa Mbinguni aliyejifunua kwetu kwa njia ya YESU KRISTO na anaabudiwa katika ROHO MTAKATIFU.

Yohana 4:24 "MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."

3. Mtu kuingia maagano na wanaomkataa YESU KRISTO kama Mwokozi wao.

Kutoka 34:12-16 " Ujihadhari nafsi yako, usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea, lisiwe mtego katikati yako. Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.  Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni MUNGU mwenye wivu. Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao."

4. Kwa kumkataa au kumwacha  MUNGU wa kweli aliyejifunua Pekee katika KRISTO YESU.

2 Nyakati 15:2 "naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi."

◼️ Biblia inasema MUNGU atakuwa pamoja na Wewe kama ukiamua kuwa pamoja na yeye, ukiamua kumwacha na yeye anakuacha, akikuacha MUNGU ni hatari sana, aliowaacha hawawezi kuwa katika uzima wake hadi warejee kwenye Wokovu wake.

5. Kwa kufanya dhambi, maovu na makosa.

1 Wakorintho 6:9-10 " Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi."

6. Kwa Mtu kupenda kufanya mambo ya Duniani yaliyo machukizo kwa MUNGU.

1 Yohana 2:15-17 " Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda BABA hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na BABA, bali vyatokana na dunia.
 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele."

7. Kwa Mtu kukataa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU.

Warumi 8:9 "Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake."

◼️Kukataa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU ni hatari sana.

Ndugu, Usikubali kuongozwa na shetani kamwe, amua kuongozwa na ROHO MTAKATIFU baada ya Wewe kuokoka.

◼️ Kumbuka shetani  hana nafasi hata moja katika ufalme wa MUNGU, hivyo usimpe nafasi kisha na wewe ukose nafasi katika ufalme wa MUNGU.

➡️Biblia inasema kwamba shetani ndiye adui wetu hivyo hatutakiwi kumpa faida Wala nafasi hata moja shetani.

◼️Shetani anajua kwamba katika KRISTO YESU Mimi na wewe tuliookoka tutaenda Mbinguni kule ambako yeye alifukuzwa.

✔️✔️Ndugu jitahidi sana ishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.

◼️Usimpe shetani nafasi wala mawakala zake usiwape nafasi hata moja katika maisha yako.

1 Petro 5:8-9 "Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi,  pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments