![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Ipo miaka ya kukumbukwa na MUNGU.
Zaburi 115:12-13 ''BWANA ametukumbuka, Naye atatubariki sisi. Ataubariki mlango wa Israeli, Ataubariki mlango wa Haruni, Atawabariki wamchao BWANA, Wadogo kwa wakubwa.''
◼️Haijalishi mwaka huu Wewe huoni chochote hadi sana lakini hiyo haifuti kwamba upo mwaka wa Wewe kukumbukwa na MUNGU wa Mbinguni kwa ajili ya Baraka za ki Mbingu.
✓✓Hata ikibaki wiki Moja bado YESU KRISTO anaweza kuitumia kukutendea mambo makubwa na ukawa ndio Mwaka wako wa kukumbukwa na Bwana MUNGU.
✓✓Wakati wa MUNGU kukukumbuka haina maana ya kwamba alikusahau bali ni majira ya MUNGU ili atimize kusudi lake jema kwako.
✓✓Sio miaka yote inaweza kuwa sawa bali ipo miaka ya kukukumbukwa na kutendewa mahitaji yako ambayo katika miaka mingine hayakutendeka.
Ngoja nikupe mifano hai.
◼️Kulikuwa na miaka mingi ya Raheli kuwa katika ndoa yake lakini hakupata mtoto, lakini ulifika mwaka wa kukumbukwa na MUNGU ndipo akampata mtoto Yusufu.
Mwanzo 30:22-23 ''MUNGU akamkumbuka Raheli; MUNGU akamsikia, akamfungua tumbo. Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, MUNGU ameondoa aibu yangu.''
◾Kwanini isiwe miaka mingine iwe ni mwaka huo?
✓✓Kama ni maombi alikuwa anaomba na kama ni kigezo ni kuwa ndani ya Ndoa basi yeye alikuwa ndani ya Ndoa Takatifu, ilikuwaje inafika mwaka MUNGU akamkumbuka?
◼️Ulipita wakati mwingi sana Hannah akiwa ndani ya Ndoa na hakupata Mtoto lakini mwaka mmoja wa kukumbukwa na MUNGU ukafika katika maisha ya Hana.
1 Samweli 1:19 ''Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka.''
✓✓Kama ni Ibada Hannah alikuwa anafanya, kama ni utoaji basi Hana alikuwa zaidi, Kama ni afya Hana alikuwa nayo lakini kwa miaka mingi ilipita bila baraka yake ya uzao, lakini Biblia inasema kwamba ikafika siku moja katika mwaka fulani MUNGU akamkumbuka Hana na kulifungua tumbo la uzao na akapata sio tu bora mtoto bali akapata mtoto bora aitwaye Nabii Samueli.
✓✓Kwanini Biblia sehemu nyingi inasema ''MUNGU akamkumbuka fulani'' wakati anamkumbuka ilikuwa ni mwaka fulani, kwanini mwaka huo?
✓✓Kumbe tunajifunza kwamba ipo miaka ya kukumbukwa na MUNGU.
Mimi Peter Mabula nakuombea Wewe rafiki yangu kwa MUNGU mwaka huu uwe mwaka wako wa kukumbukwa na MUNGU.
✓✓MUNGU akukumbuke katika afya yako na kukuponya magonjwa haijalishi kibinadamu hayo magonjwa hayawezi kupona.
✓✓Akikukumbuka Bwana YESU hakika atakuponya maana Neno lake linasema kwamba anaponya magonjwa yote na madhaifu yote(Mathayo 9:35) hivyo kama anaponya magonjwa yote hata ugonjwa wako uko katika magonjwa hayo anayoyaponya YESU KRISTO.
✓✓MUNGU akukumbuke katika ndoa yako iliyo na migogoro na matatizo na vita kali.
✓✓MUNGU akukumbuke katika zao na uchumi.
✓✓MUNGU akukumbuke katika kazi na kibali.
◼️Huwa kuna wakati wa MUNGU kumkumbuka mtu fulani na kumtendea mema.
✓✓Ulifika wakati wa Nuhu kukumbukwa na MUNGU.
Mwanzo 8:1 ''Na MUNGU akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; MUNGU akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;''
Dada mmoja ambaye ni rafiki yangu na alikuwa ananiuzia vitabu vyangu mkoani maana alikuwa anafanya kazi Stationery alikutana na Muujiza wa ajabu. Kuna mabosi fulani walikuwa wanapita pale na kuchapisha nyaraka wakapenda kazi yake wakamwajiri katika kampuni ya Watalii na ndani ya muda mfupi akawa yeye ni Boss mkubwa pale, hiyo inaitwa kukumbukwa na MUNGU wa Mbinguni.
◼️Ulifika wakati wa Ibrahimu kukumbukwa na MUNGU ili Lutu aliye ndugu wa Ibrahimu aponywe kutoka maangamizo ya moto wa Sodoma na Gomora.
Mwanzo 19:29 '' Ikawa MUNGU alipoiharibu miji ya Bondeni, MUNGU akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.''
◼️Ndugu uliyeokolewa na Bwana YESU nakuomba kwa maombi mwambie MUNGU Baba akukumbuke mwaka huu katika hitaji lako la muda mrefu, kazi yako mkumbushe MUNGU kwa maombi.
Isaya 43:26 '' Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako. ''
◼️MUNGU anaweza akalikumbuka agano uliloingia naye kwa njia ya sadaka na akakuokoa au kuokoa watoto wako.
Kutoka 6:5 '' Na zaidi ya hayo, nimesikia kuugua kwao wana wa Israeli, ambao Wamisri wanawatumikisha, nami nimelikumbuka agano langu. ''
Wakati mwingine mimi huwa nawaza sana juu ya mwaka 2014 nilipofunga Ndoa Takatifu na Mke mwema wangu Jemimah.
Kwa malengo ya tangu zamani ya kwangu nilipanga na kukusudia kufunga ndoa mwaka 2010 lakini mwaka huo haukuwa mwaka wa kukumbukwa na MUNGU juu ya Ndoa, mwaka 2011 ukapita, 2012 ukapita, 2013 ukapita lakini 2014 haukupita maana ndio ulikuwa mwaka wangu wa kukumbukwa na MUNGU wangu wa mbinguni, kuna kuna miaka ya kukumbukwa na MUNGU.
✓✓Akikukumbuka MUNGU shetani anakusahau.
✓✓Akikukumbuka MUNGU matataizo yanakusahau.
✓✓Akikumbuka MUNGU wachawi wanakusahau.
◼️Inawezekana umetafuta kazi kwa miaka mingi sana lakini ukiendelea kuishi maisha matakatifu katika KRISTO na kuomba unaweza kushangaa MUNGU anakuletea mwaka wa yeye kukukumbuka na akakupa double double.
✓✓Kuna Mtu inawezekana unawaza nitaolewa lini? Nitapata Mtoto lini? Ndoa yangu itapata amani lini? nitapata mchumba lini? huduma yangu itakua lini? nitapata kiwanja lini? nitajenga lini? nitaheshimika kwa ndugu zangu wanaonidharau lini? Nitapona ugonjwa huu mbaya lini? nitatoka hospitali lini? biashara yangu itapata faida lini? nitaacha kuteswa na wachawi lini? nitawashinda wakuu wa giza lini? mwenzi wangu atabadilika lini? nitapanda cheo lini? uchumi wangu utakua lini? nitapata kibali lini? haki yangu nitaipata lini? n.k
✓✓Ndugu, kumbuka tu kwamba uko mwaka wa kukumbukwa na MUNGU na utamshangaa MUNGU wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
◼️Kazi yako tu ni kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU na kufanyia kazi kila kitu cha ki MUNGU.
✓✓Bwana YESU na akukumbuke sasa katika unyonge wako.
Zaburi 136:23 '' Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. ''
✓✓Inawezekana wewe ni mnyonge kwa sababu unaumwa na hujiwezi.
✓✓Inawezekana wewe sasa ni mnyonge kwa sababu huna Baba wala Mama.
✓✓Inawezekana wewe sasa ni mnyonge kwa sababu ndugu zako wamekukataa au mchumba amekuacha.
✓✓Inawezekana wewe sasa ni mnyonge kwa sababu umefukuzwa kazi bila kosa au umeshushwa cheo.
✓✓Inawezekana wewe sasa ni mnyonge kwa sababu mtu wako wa muhimu amefariki.
✓✓Inawezekana wewe sasa ni mnyonge kwa sababu umefeli.
◼️Ndugu, yupo MUNGU anayeweza kukukumbuka hata katika unyonge wako na kukuinua juu sana.
◼️Ndugu, kama unaishi maisha ya haki katika KRISTO hakika MUNGU hatakusahau, ndugu endelea kumngoja MUNGU.
✓✓Binafsi mimi nina shuhuda nyingi sana juu ya kukumbukwa na Bwana YESU ndio maana leo nakutia moyo na kukujulisha kwamba ipo miaka ya kukumbukwa na MUNGU.
✓✓Jitahidi tu usitende dhambi maana dhambi ndicho huwa kikwazo kikuuu cha mtu kukumbukwa na MUNGU, dhambi huzuia kusudi la MUNGU la majira kwako, dhambi ndio kikwazo kikubwa cha kuzuia wewe kukumbukwa na MUNGU.
✓✓Nakusihi sana okoka kama hujaokoka na anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu.
✓✓Kama ulikuwa hujui ni kwamba ukitubu leo dhambi zako na kuziacha ujue dhambi hizo hazitakumbukwa tena.
Isaya 43:25 ''Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. ''
✓✓Ngoja nikuambie pia mambo haya muhimu sana ambayo yanaweza kusababisha wewe kukumbukwa na MUNGU.
Nini kinaweza kukufanya ukumbukwe na MUNGU.
1. KUISHI MAISHA YA HAKI KUNAWEZA KUKUFANYA UKAKUMBUKWA NA MUNGU NA KUTENDEWA MEMA.
Isaya 44:21 ''Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.''
2. AGANO ULILOINGIA NA MUNGU LINAWEZA KUKUFANYA UKAKUMBUKWA NA MUNGU NA KUTENDEWA MEMA.
Kutoka 2:24 '' MUNGU akasikia kuugua kwao, MUNGU akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo ''
Walawi 26:42 ''ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Ibrahimu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo. ''
3. ZAKA ZAKO NA SADAKA ZAKO ULIZOMTOLEA MUNGU ZINAWEZA KUKUFANYA UKAKUMBUKWA NA MUNGU NA KUTENDEWA MEMA.
Zaburi 20:3-4 '' Azikumbuke sadaka zako zote, Na kuzitakabali dhabihu zako. Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote. ''
4. NENO ALILOKUAMBIA MUNGU ANAWEZA KULIKUMBUKA NA KUKUTENDEA MEMA.
Zaburi 111:5 ''Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele.''
Zaburi 105:8 ''Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu. ''
5. NADHIRI ZAKO KWA MUNGU ZINAWEZA KUKUFANYA UKAKUMBUKWA NA MUNGU NA KUTENDEWA MEMA.
1 Samweli 1:11 na 19 '' Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe. ........... Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka. ''
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292.
Ubarikiwe sana.

Comments