![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
✓✓Najua unafahamu ukisikia Hawara au Mahawara.
Najua pia unafahamu ukisikia Kimada au Vimada.
Na najua ukisikia Neno Nyumba ndogo inamaanisha Nini.
✓✓Wako watu ni mahawara japokuwa wanajiita ni wanandoa.
✓✓Wako watu ni vimada japokuwa wanajiita ni wanandoa.
Wako watu Leo Wana Nyumba ndogo.
◾Hawara ni nini?
✓✓Hawara ni Mwanamke au mwanaume anayeishi na mtu asiyeoana naye.
2 Timotheo 3:6 "Kwa maana katika hao wamo wale wajiingizao katika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi;"
✓✓Ndugu, usionekane mjinga kwa kuishi na Mtu kingono bila Ndoa.
◾Kimada ni nani?
✓✓Kimada ni mwanamke anayeishi na mwanaume ambaye hakumuoa.
Je wewe ni Mke au ni kimada?
✓✓Ndugu, usikubali kuwa kimada bali tubu na hakikisha unafunga ndoa takatifu.
✓✓Vimada na Mahawara ni wale watu wanaishi kama wana Ndoa ila hawajafunga Ndoa.
Kwa kifupi wanazini.
Mithali 6:32-33 " Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika."
◾ Nyumba ndogo ni nini?
✓✓Ukiangalia kamusi ya kiswahili sanifu neno ''Nyumba ndogo'' lina maana ya Mwanamke mwenye uhusiano wa kimapenzi na Mume wa mtu mwingine.''
✓✓Ni dhambi Mwanamke kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mume wa Mtu mwingine.
Mtu huyo anachokifanya ni kuzini na mume wa mtu, yaani ni mzinzi.
Na Biblia iko wazi sana kwamba kwenye uzima wa milele hataingia mzinzi wala mwashwerati hata mmoja.
1 Kor 6:9 ''Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,''
◼️Nimepewa ujumbe huu ili nikuambie utubu leo na kuachana na mume wa mtu na kisha mpokea YESU KRISTO kama Mwokjozi wako kisha anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu.
Katika dunia ya leo wapo watu hata hawaoni aibu kujiita nyumba ndogo, ni hatari sana.
Je na wewe unayesoma ujumbe huu uliye mwanamke, wewe ni nyumba ndogo?
Yaani unaishi na Mume wa mtu au huwa unafanya uzinzi na Mume wa mtu?
◼️Ndugu, kama ni kweli nakuomba sana sana achana na Mume wa Mtu, tubu na anza kuishi maisha matakatifu ya wokovu wa Bwana YESU.
✓✓Mtu Mwingine ana Ndoa yake ila ana uhusiano wa kingono na Mtu Mwingine nje, huyo ni Hawara au Kimada, Biblia hapo juu Iko wazi sana ikisema "Aziniye hana akili?
Namuona kwenye ulimwengu wa roho Mwanamke mmoja mwembamba analia wakati nikiandika ujumbe huu, ngoja niendelee maana huyu ninayemuona muda huu anafunguliwa kifungo Cha uhawara na atakuwa huru kwa Jina la YESU KRISTO.
◼️Je wewe una hawara au una mwenzi wa Ndoa?
✓✓Je umeshindwa nini kutoa mahari kisha kuwa na kibali cha Wazazi na kisha mkafunga ndoa Kanisani?
✓✓Inawezekana ujumbe huu ni changamoto kwa wengi lakini ushauri wangu ndugu hakikisha unafunga Ndoa Takatifu Kanisani.
✓✓Na Kama uko kwenye Ndoa ila una Hawara nje au Kimada achana nae haraka sana.
Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."
✓✓Lakini pia wapo watu wako kwenye Ndoa za kimila au kiserikali hata Ndoa za kimila au za kiserikali ni Ndoa halali, ila kuna watu wanaishi kama Mume na Mke katika mfumo wa uhawara au ukimada, hiyo ni mbaya sana.
Jitenge na uhawara.
◼️Wewe Baba/Mwanaume kama ni hawara hakikisha unaondokana na uhawara.
◼️Wewe Mama/Mwanamke kama ni hawara hakikisha unaondokana na uhawara.
Inawezekana wewe una mke halali ambaye anatambuliwa na wazazi na Kanisa lakini huwa unatoka nje ya ndoa yako ndio maana wewe ni hawara na huko nje ya ndoa huwa unakutana na hawara.
◼️Ndugu heri ufunge Ndoa bila hata sherehe na bila hata kutumia gharama lakini iwe ni Ndoa Takatifu yenye baraka za MUNGU na kibali cha MUNGU na cha Kanisa na wazazi, sio kuendekeza uhawara.
◼️MUNGU anataka Ndoa Takatifu na sio uhawara wala ukimada.
✓✓Maana nje ya Ndoa Takatifu kuna uzinzi na uasherati, ndio maana Biblia inataka wewe uwe na Mke/Mume wako mwenyewe mmoja tu na hakikisha unaiheshimu Ndoa yako maana hiyo inatambuliwa na Wazazi, Kanisa na inatambuliwa mbinguni.
Waebrania 13:4 '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu.''
✓✓Unapozini maana yake umeingia patano la kikahaba. Kinachofanyika hapo ni kwamba mapepo ya ukahaba kutoka kwa huyo unayezini naye yanakuja kwako, yanakuwa na uhalali kwako, maana umefungua mlango kwa uzinzi au uasherati.
✓✓Mapepo yanakuja ndani yako kutoka kwa huyo unayezini naye maana mlango mmoja wapo wa mapepo ni pale yanapopata uhalali, na kuzini huleta uhalali wa mapepo kuingia ndani ya mtu yakitokea kwa yule anayezini naye wakati huo.
1 Kor 6:16 '' Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.''
✓✓Kuna mtu anaweza sana kukutaka mfanye mapenzi kumbe huo ni mpango wa shetani kuhamisha nguvu za giza zilizo na uhalali kwa mtu huyo ziwe na uhalali na kwako pia, yaani mtu anaweza kukushawishi mzini na kumbe ni mpango wa shetani ili mapepo yaliyo ndani ya mtu huyo yawe pia ndani yako yaani yataingia kwako kutoka kwa mtu huyo kwa sababu umefungua mlango kwa dhambi ya uzinzi au uasherati.
◼️Kama kuna kitu kina madhara sana kimwili na kiroho basi ni uzinzi au uasherati.
1 Kor 6:18 '' Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.''
✓✓Uzinzi na uasherati ni moja ya vitu vinavyowaharibia maisha watu wengi kimwili na kiroho.
✓✓Kama tu ulikuwa hujui ni kwamba uzinzi au uasherati ni moja ya ibada za sanamu.
Wakolosai 3:5 '' Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; ''
Kumbe ukifanya mapenzi na mtu asiye mke wako wa ndoa au mume wako wa ndoa umefanya dhambi nyingi zikiwemo.
1. Kuunajisi mwili kiroho.
2. Ni dhambi ya uzinzi na uasherati.
3 Ibada ya sanamu.
Na Biblia inasema
1 Kor 10:4 ''4 Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.''
✓✓Ndugu, inawezekana nguvu za giza zinazokutesa sana sasa ni matokeo ya uzinzi au uasherati.
Kama ni kweli tubu na acha kufanya dhambi hiyo mbaya.
✓✓Kama uko katika ndoa rizika na Mke wako mmoja tu uliyepewa au Mume wako mmoja tu uliyepewa.
✓✓Kama hujaoa au kuolewa usikubali kufanya ngono na mtu yeyote, awe ndani ya ndoa au hajaingia katika ndoa.
✓✓Jichunge sana ili usije ukaanza baadae kuteswa na nguvu za giza kwa sababu ya uzinzi au uasherati wa sasa.
◼️Ndugu hakikisha unampokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na anza kuishi maisha matakatifu ya Wokovu kuanzia sasa.
◼️Kwa wewe uliyeteswa na dhambi hii basi kama kuna kitu muhimu unakihitaji sasa ni maombi ya toba katika KRISTO YESU.
◼️Kama kweli umeamua kuachana na dhambi za uzinzi na uasherati basi mwambie MUNGU akusamehe na kukuosha uovu huo kwa damu ya YESU KRISTO na kisha omba Bwana YESU akutakase kwa damu yake ya agano jipya iliyo ya thamani sana.
Zaburi 51:1-4 ''Ee MUNGU, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. ''
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Sadaka ya kuipeleka Injili, Maombezi, Whatsapp n.k)
Ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Sadaka ya kuipeleka Injili, Maombezi, Whatsapp n.k)
Ubarikiwe sana.

Comments