![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◾Uzinzi ni nini?
✓✓Uzinzi ni kitendo cha Mtu aliye kwenye Ndoa kufanya mapenzi na mtu yeyote nje na mwenzi wake wa ndoa.
Yakobo 4:4 "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU."
✓✓Wazinzi Ni Wanandoa Wanaotoka kingono nje Ya Ndoa Zao.
◾Uasherati ni nini?
✓✓Uasherati ni kitendo cha kuzini anachokifanya mtu ambaye hajaingia katika ndoa.
Waefeso 5:3 "Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;"
✓✓Waasherati Ni Wale Ambao Hawajafunga Ndoa Wakifanya Ngono Wao Kwa Wao Au Wakifanya Ngono Na Wale Walio Kwenye Ndoa.
◾Kuzini ni nini?
✓✓Kuzini ni kukutana mwili na Mtu yeyote ambaye sio mwenzi wako wa Ndoa.
✓✓Kama kuna mtu yuko katika ndoa anapozini na mtu ambaye hayuko katika ndoa maana yake mzinzi na mwasherati wanakutana kuzini.
✓✓Aliye kwenye ndoa anapotoka nje ya ndoa yake kingono ni mzinzi na mtu ambaye hajaingia kwenye ndoa anapozini huyo ni mwasherati.
✓✓Kitendo wanachokifanya wazinzi au waasherati kinaitwa uzinifu au zinaa.
◼️Biblia iko wazi sana kwamba uzinzi na uasherati ni dhambi na dhambi hiyo mtu asipoitubia na kuacha anaweza kuishi jehanamu milele.
1 Kor 6:9-11 '' Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa MUNGU? Msidanganyike; WAASHERATI hawataurithi ufalme wa MUNGU, wala waabudu sanamu, wala WAZINZI, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana YESU KRISTO, na katika ROHO wa MUNGU wetu.''
Naamini nimejibu swali lako ambalo huwa unajiuliza mara kwa mara Kwa yule ambaye alikuwa hajui.
✓✓Wazinzi ni walio ndani ya ndoa wanapotoka nje ya ndoa zao.
✓✓Waasherati ni wale ambao hawajaingia ndani ya Ndoa wakifanya uzinifu.
Akikutana kimapenzi mtu aliye ndani ya ndoa na mtu asiye ndani ya ndoa maana yake hapo wamekutana mzinzi na mwasherati ili wafanya uzinifu, ni dhambi mbaya sana.
Waliofyatuka akili tu ndio hufanya uzinzi na uasherati.
Na uzinifu wao huwafanya wawe rafiki wa dunia na kuwa adui wa MUNGU.
Yakobo 4:4 "Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa MUNGU."
Je wewe ni adui wa MUNGU kwa sababu ya uzinzi na uasherati?
◼️Geuka Leo kwa Jina la YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai.
◼️Kwa ambao wanataka kuingia katika ndoa nasukumwa kuwapa ushauri huu.
✓✓Kama unataka kuingia katika ndoa epuka sana uasherati.
✓✓Jitenge mbali sana na uasherati kama kweli unataka kuingia katika Ndoa Takatifu.
Kwanini ujitenge mbali na uasherati?
Ni kwa sababu hizi.
1. Uasherati utakufanya MUNGU akuache.
✓✓Akikuacha MUNGU ujue mapepo yatachukua nafasi na hivyo kuvuruga uwezekano wa wewe kufunga ndoa.
2. Uasherati huondoa heshima yako.
3. Uasherati huifuta hadhi yako, unakuwa mtu usiye na hadhi.
4. Uasherati ndio njia kuu ya kuwafanya vijana na mabinti wasiingie katika ndoa.
✓✓Ndugu, usikubali kuwa na mazoea yasiyo na mipaka yanayoweza kukufanya uachwe na mchumba au usipate wa kufunga ndoa na wewe.
✓✓Uasherati ni silaha kuu ya shetani kukufanya usifunge ndoa.
1 Wakorintho 6:18 "Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."
Je wewe ni rafiki wa dunia kwa sababu u mzinzi au mwasherati?
Biblia inasema kwamba kuna hukumu ya MUNGU kwa wazinzi na waasherati.
Waebrania 13:4 " Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."
◼️Ni uamuzi wako Leo kuikimbia hukumu ya MUNGU, kwa kutubu na kuacha uzinifu, au uendelee na kukumbatia uzinzi na uasherati kisha hukumu ya MUNGU iendelee kukusubiri kwa ajili ya jehanamu.
Mwenye sikio la kusikia akipenda leo kusikia na asikie na kuacha uzinzi na uasherati.
Zingatia na MUNGU atakubariki sana.
Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Kama pia unatumia Facebook ni follow maana itafika kipindi nitakuwa napost tu katika page yangu na profile yangu.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By Mwl Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292(Ushauri, Sadaka ya kuipeleka Injili, Maombezi, Whatsapp n.k)
Share ujumbe huu kwenye magroup ya Whatsapp uliyopo.
Ubarikiwe

Comments