![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Kama unayo nafasi ya kufanya maombi leo basi katika maombi yako unaweza kuombea na haya yafuatayo hapa chini ili ili kuboresha ushindi wako dhidi ya nguvu za giza.
1. Omba katika jina la YESU KRISTO maombi ya toba, ukijitakasa na kutubu ili uwe safi kiroho.
Zaburi 51:1-2 "Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu."
2. Omba katika jina la YESU KRISTO maombi ya kuvunja kila kazi za mawakala wa shetani katika kila eneo linalokuhusu wewe.
Mfano ndoa yako, familia, ukoo, afya, kibali, uzao, kazi, uchumi, mtaa, Kanisa leo, kundi lenu n.k
Haribu kazi hizo za shetani na zifunge ili zisiendelee.
1 Yohana 3:8b " Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."
3. Omba katika jina la YESU KRISTO kwamba maadui zao katika ulimwengu wa roho waabike na kufedheheka.
Nguvu za giza zilizotaka ufedheheke amuru wao ndio wafedheheke.
Wakuu wa giza, majini na kila mawakala wa shetani wanaokuwinda au kuwinda baraka yako au chochote chako, amuru kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO kwamba wao waabike na kufedheheka.
Zaburi 40:14-15 " Waaibike, wafedheheke pamoja, Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize. Warudishwe nyuma, watahayarishwe, Wapendezwao na shari yangu. Wakae hali ya ukiwa, na iwe aibu yao, Wanaoniambia, Ewe! Ewe!"
4. Omba MUNGU akulinde dhidi ya nguvu za giza.
Zaburi 121:7-8 " BWANA atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele."
Omba ndugu maana katika jina la YESU KRISTO kuna ushindi mkuu.
MUNGU akubariki sana.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu aliye hai milele.
+255714252292(Whatsapp, sadaka ya kuipeleka Injili na Maombezi?
Ubarikiwe

Comments