![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
✓✓Ninaongea na wewe usiye na YESU KRISTO.
✓✓Naongea na wewe uliye na jina la kuwa hai lakini umekufa kiroho.
Ufunuo 3:1 ".......... Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za MUNGU, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa."
✓✓Naongea na wewe uliye Kanisani lakini ni mwigizaji tu maana wewe u mzinzi, mwasherati, mchawi, mwongo, fisadi, mwizi, tapeli n.k
✓✓Naongea na wewe unayetenda dhambi.
✓✓Naongea na wewe ambaye hauishi maisha matakatifu ya Wokovu wa Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
✓✓Naongea na wewe ambaye huna muda na ibada Kanisani kwa sababu unaipenda dunia kuliko kumpenda MUNGU.
1 Yohana 2:15 " Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake."
Ndugu nisikilize kwa makini sana.
1. Usipopenda kwenda mbinguni moja kwa moja utakuwa unapenda kwenda jehanamu.
Ufunuo 20:15 "Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto."
2. Usipomhitaji YESU KRISTO Mwokozi moja kwa moja utakuwa unamhitaji shetani.
Yohana 10:10-11 "Mwivi(Shetani) haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi(YESU) nalikuja ili(Watu wanaomtii) wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Mimi(YESU) ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo."
3. Usipouhitaji Wokovu wa KRISTO YESU moja kwa moja utakuwa unauhitaji uharibifu wa mwili wako, nafsi yako na roho yako.
1 Wathesalonike 5:9-10 "Kwa kuwa MUNGU hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu YESU KRISTO; ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala."
◼️Ndugu yangu, inakupasa kupenda kwenda mbinguni, na kupenda kwenda mbinguni ni kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako kisha unaanza kuishi maisha matakatifu ya wokovu wake.
1 Petro 1:14-15 " Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"
◼️Ndugu, inakupasa kupenda kuishi maisha matakatifu na hakikisha kuanzia sasa unaanza kuyaishi maisha matakatifu, jitenge mbali na dhambi, vunja uhusiano na mtu anayekuangusha dhambini futa hata namba yake ya simu ondoa ukaribu naye ili tu asikunase dhambini ukaenda jehanamu, kuanzia sasa ambatana na neno la MUNGU kwa kulifuata na kuliishi katika KRISTO YESU Mwokozi.
Zaburi 1:1-3 " Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa."
✓✓Ndugu, mhitaji YESU KRISTO na hakikisha unampokea kama Mwokozi wako leo.
◼️YESU KRISTO anazungumza na wewe kupitia somo hili nakuomba zingatia sauti yake ambayo ndio neno lake, hivyo mpokee kama Mwokozi wako leo.
Waebrania 4:7 ".......... Leo,kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu."
Ndugu usiufanye moyo wako kuwa mgumu katika kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Ndugu kumbuka kwamba kila neno la MUNGU huwa limebeba kusudi la MUNGU juu ya anayelisikia hivyo usidharau kamwe neno la MUNGU.
Mtu mmoja walinipigia simu watu wake wa karibu ili nimuombee apone maana alikuwa amelazwa hospitalini anaumwa.
Wakati namuombea rohoni mwangu nilisukumwa kumuongoza sala ya toba ili ampokee YESU KRISTO kama Mwokozi wake.
Nilipoanza kumuongoza sala ya toba akakubali lakini katikati ya sala ya toba akakataa. Akaniambia nimuombee tu uponyaji Niachane na masuala ya kuokoka, Nikamuombea uponyaji huku nikisikitika sana. Neema ya MUNGU ni kwamba baada ya maombi akajisikia nafuu kubwa mno, wakanipigia hadi simu wakisema amepona maana amenyanyuka kitandani na kutembea maana mwanzo hakuweza, lakini rohoni mwangu nilisikia sauti ikisema "Huyu hatarudi" hivyo nikajua mtu huyo ni wakati wake wa mwisho wa kuishi duniani. Sikuwaambia ndugu zake juu ya sauti ya rohoni niliyoisikia ila nilitaka kumuongoza sala ya toba tena akakataa, nikamwambia ampe simu binti yake niongee naye, nikaongea na binti yake na kumsisitiza sana kwamba jirani na hapo awatafute wachungaji wa madhehebu ya kiroho ili wakamuongoze sala ya toba. Binti yule alifanya haraka kumfuata Mchungaji huku na mimi nikiomba mtu huyo apate neema ya wokovu. Mchungaji alipofika tu akamuombea na kumuongoza sala ya toba, mtu yule akakubali kuokoka na akafurahi kuokolewa na YESU KRISTO lakini muda mfupi baadae yule mtu akafariki dunia.
Ndugu yangu, kuna neno la MUNGU linaweza kubeba kusudi la MUNGU kabisa hivyo usiliache lipite bali fanyia kazi.
Nakuomba mhitaji YESU KRISTO na mpokee kama Mwokozi wako leo, ishi maisha matakatifu huku ukitimiza katika kumcha MUNGU.
Na hili ndilo neno la BWANA kwako leo.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU Mwenyezi.
+255714252292(whatsapp).
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.
Na hili ndilo neno la BWANA kwako leo.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la MUNGU Mwenyezi.
+255714252292(whatsapp).
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments