USIMJIBU MPUMBAVU SAWA SAWA NA UPUMBAVU WAKE USIJE UKAFANANA NAYE.

Na Mwl Peter Mabula 
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi wetu 




Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu.

✓✓Wewe kama mteule wa MUNGU katika KRISTO YESU wakati mwingine unatakiwa kuwa makini sana katika usemi wako, majibu yako na maneno yako kutokana na ulichoulizwa na watu au kitu unachotakiwa kuthibitisha mbele za watu.

✓✓Watu wengi wanaihitaji sana kauli ya  kinywa chako hivyo uwe makini daima katika majibu yako, jibu katika mpango wa MUNGU.

✓✓Katika maisha yako wakati mwingine unahitaji Kuwa makini sana na majibu yako kutokana na maswali ya baadhi ya watu hasa wasiokutakia mema, lengo lao uingie katika mitego yako au uingie hatiani.

Mithali 4:14" Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya."

Ndugu, kuna mtu mwingine anaweza kuuliza upumbavu, usimjibu mtu sawasawa na upumbavu wake.

Mithali 26:4" Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye."

Ninachokuomba hakikisha unaishi maisha matakatifu siku zote na uwe makini na maneno ya kinywa chako ili uhakikishe katika kinywa chako halitoki  neno ambalo halikupaswa wewe mteule wa MUNGU kulisema.
Ubarikiwe.
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.

Comments