KUSHAMBULIWA MKONO NDOTONI NA NAMNA YA MAOMBI ILI USHINDE.

Na Mwl Peter Mabula 



Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu. 
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU. 

■Njia mojawapo aliyotupa MUNGU ili tutambue kilichopo kwenye ulimwengu wa roho ni kwa kupitia  ndoto na maono. 

Watu wengi sana wanaomba maombi ya kujinasua na vifungo mbalimbali lakini walipojulishwa kwa ndoto au maono juu ya vifungo hivyo vya giza kwa kupitia kuona mashambulizi katika maeneo  ya miili yao hawakushughulikia kimaombi hivyo tatizo likaendelea kuwapata hata kama walitamani tatizo hilo litoke, ila tu hawakujua wanatakiwa kupambana na nini kwenye maombi.

Ndugu, katika KRISTO YESU  umepewa mamlaka ya kuomba hivyo itumie nafasi hiyo ili ushinde vita vya kiroho. 
 
Yeremia 51:20-21 " Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;"

●Ndugu,  usipohusika na maombi tatizo lako litaaendelea kukutesa. 

Kila tatizo unaloliona kwenye ulimwengu wa roho kwenye eneo fulani la mwili wako,  hakikisha  unajua  namna ya kuomba ili kuondoa tatizo hilo kiroho.

Ngoja nikupe mifano hai michache  kutokana na baadhi ya watu ambao niliwahi kuwasiliana nao kwenye huduma ili unielewe vyema kabla sijaendelea na ujumbe wa leo. 

Ndugu mmoja aliota chura anaingia kwenye unyayo wa mguu wake wa  kulia na kupotelea mwilini, tangu siku hiyo ndugu huyo anaumwa mguu na hata wakati mwingine anashindwa kutembea. 

Mama mmoja siku moja aliota ndoto mkono wake wa kushoto umepakwa kinyesi, tangu siku hiyo watu wakaanza kumdharau na hadi watoto wake wa kuzaa wakaanza kumchukia, hata aliowasaidia sana wakamgeuka.

Mtu mmoja aliota mikono yake imefungwa na kamba, kila akijaribu biashara yeyote hafanikiwi,  anakula hadi mtaji na kufilisika. 

Ngoja nikujulishe kwenye ulimwengu wa roho  mkono unaposhambuliwa inajulisha nini.

Mikono ina maana nyingi kiroho hivyo unaposhambuliwa mikono ndotoni  au unapoota mkono mmoja umedhurika ujue  na kutambua ni nini kimelengwa kwako kuharibiwa na nguvu za giza. 

Mtu mmoja aliota ndoto mkono wake wa kulia unashambuliwa na nyoka  hakujua maana yake hadi alipoingia katika matatizo yaliyosababishwa na hiyo roho ya kuzimu iliyo katika umbo la nyoka. 
 
Ngoja tuangalie maandiko.

Mithali 3:16 "Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto."

■Ukishambuliwa na nguvu za giza kwenye mkono wa kiume ujue nguvu za giza zinawinda uhai wako maana mkono wa kiume kiroho umebeba wingi wa siku,  hivyo ukiona unashambuliwa na chochote kwenye ulimwengu wa roho kwenye mkono wako wa kulia ujue nguvu za giza wanajaribu kuhakikisha hauishi miaka mingi yaani wanakuletea tatizo ambalo litakuletea matatizo yanayolenga usiishi miaka mingi. 

Hata Adamu alifukuzwa Edeni ili asije akatumia mkono wa kulia kuchukua tunda kisha akaishi milele(Mwanzo 3:22)
Kuna uhusiano wa kiroho kati ya mkono wa kulia na kuishi miaka mingi. 

●Mawakala wa shetani hawataki uishi miaka mingi hivyo wanafanya kila mipango ya kipepo kukatisha uhai wako, ndio maana unaota mkono wako wa kulia ukishambuliwa na nguvu za giza. 

Kwa sababu Biblia inasema kuna wingi wa siku za kuishi katika mkono wa kiume, hivyo ukishambuliwa mkono wa kiume tambua ni nini kinawindwa na mawakala wa shetani. 

Ukiwa unaongea na watu mbalimbali ni rahisi tu kusikia mara mtu ameumwa na nyoka mkono wa kulia ndotoni, mara simba, au paka wengine chui au mtu au viumbe hai wengine wameshambulia mkono wake wa kuume , ndugu tambua kinachowindwa na hizo nguvu za giza. 

■Ukiona ni mkono wa kushoto ndio unawindwa na nguvu za giza au unashambuliwa na nguvu za giza,  tambua kwamba adui anawinda uchumi na heshima. 
Mithali 3:16 "........ Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto."

Ukiona mkono wa kushoto ndio unashambuliwa ndotoni ujue adui anafanya kila mbinu kuhakikisha wewe huheshimiwi na maana nyingine pia ni kwamba shambulio la mkono wa kushoto ndotoni ni kwamba adui anakuzuia kufanikiwa kiuchumi. 

Ndugu,  tambua hicho ulichokiona kinashambulia mikono kinawakilisha nini? 

Ukiona kwenye ndoto au maono adui awawinda tu mkono wa kushoto elewa kinawindwa nini na ukiona unalengwa zaidi mkono wa kulia elewa kinalengwa nini ili ujue namna ya kuomba. 

Unaweza kuona nguvu za giza zikiwinda mkono wako wa kuume na kumbe wanawinda uhai wako kwa kutumia watu katika mashambulizi ya kimwili, yaani unaweza kukosana na mtu na anakutumia watu wa kukuuwa.
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda.

Lakini pia unaweza kuona wanyama ndio walishambulia mkono wako elewa ni mnyama gani na amebeba nini na anawinda nini kwako. 
Mfano Ukiona simba ndio awawinda mkono wako Maana yake wakuu wako wa kazi au wakuu wa kiserikali katika eneo lako la kazi ndio una vita nao na pia wanatumia roho za vitisho ili kukuharibia au kukudhuru ili upate madhara yanayohusika na mkono kiroho kama nilivyokueleza hapo juu ya mkono una maana gani kiroho,
pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda. 
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda. 

●Ukiona ng’ombe Ni roho ya kishetani katika ukoo wako au Mizimu ndio inakuwinda, pambana na nguvu hizo za giza na utashinda.  
Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda. 

●Ukiona Mbwa Ni roho ya uzinzi na uasherati, hivyo wanainda uhai wako kupitia wewe ili uanguke kwenye uzinzi au uasherati. 
Hivyo jitenge mbali na dhambi hiyo inaweza kukukatisha uhai wako, hata ukiona tu mbwa analamba mkono wako elewa nini kinalengwa na hiyo roho ya uzinzi na uasherati, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda. 

●Ukiona Nyoka Ni majini, wachawi, waganga wa kienyeji, wakuu wa giza, na kila mwanadamu aliye wakala wa giza, sasa elewa tu nini adui huyo anawinda ili ajue namna ya kuomba, Hivyo haribu roho hizo za nyoka zinazowinda uhai wako,pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda. 

Vivyo hivyo ukiona adui huyo anawinda mkono wa kishoto tambua kwamba nguvu hizo za giza zinalenga kukuondolea kuheshimiwa na zinalenga kukuondolea uchumi wako kwa njia mbalimbali, pambana na nguvu hizo za giza Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO na utashinda. 

Lakini pia kama unaota mikono yako yote ikifungwa hiyo inaweza kuwa na maana tofauti na kufuatiliwa mkono mmoja tu. 

■Kufungwa mikono yote Kwa kamba au chochote hiyo ina maana adui anafunga mkono kiroho ili kukuzuilia kufanikiwa katika lolote mfano  mambo ya kiuchumi. 
Maana yake adui anafunga mafanikio yako. 

Mtu aliyefungwa mikono kiroho hata akipewa milioni 50 afanyie biashara ndani ya muda mfupi atakuwa hana hata lakini na hajui imekuwaje,  adui alishamfunga mikono kiroho ili kumzuilia kufanikiwa, hapo inabidi kuomba maombi ya kufunguliwa mikono kiroho. 

Nini ufanye ukiona kwenye ulimwengu wa roho mkono wako wa kulia/kuume  unawindwa au unashambuliwa ?

1. Omba maombi kuharibu kila kilichoharibu mkono wako wa kuume. 

Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."

2. MUNGU ameahidi atatimiza miaka yako.
Kutoka 23:26 "....... na hesabu ya siku zako nitaitimiza."
Hivyo dai ahadi ya MUNGU kimaombi ili muda wako wa kuishi utimie  na sio mawakala wa shetani kukatisha uhai wako.
 Kumbuka ahadi za MUNGU zilizo katika yeye ni ndio na kweli 
2 Wakorintho 1:20 "Maana ahadi zote za MUNGU zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; MUNGU apate kutukuzwa kwa sisi."

Hivyo timiza wajibu wako wa kuomba mbele za MUNGU na atapewa. 

Mathayo 7:7 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;"

3. Takasa mkono wako kwa damu ya YESU KRISTO. 

Walawi 11:44 "Kwa kuwa mimi ni BWANA, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi."

4. Tumia mamlaka ya jina la YESU KRISTO kukataa kifo cha kabla ya wakati wako  kilichopangwa na nguvu.

Zaburi 118:17 "Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA."

5. Jitenge mbali na dhambi kwa kila mawakala wa shetani ili vitu hivyo visipate nafasi ya kukutumikisha kukatisha uhai wako. 

Mfano hai jitenge mbali na uzinzi na uasherati ili dhambi hiyo isikatishe maisha yako. 

1 Wakorintho 6:18 "Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe."

Ukishambuliwa mkono wa kushoto tu.
Tambua kwamba kinachowindwa ni utajiri na heshima (Mithali 3:16) Unaweza kuwa unafanya biashara, kazi au kilimo na mara kwa mara unaota ukishambuliwa mkono wa kushoto tu au ukifanyiwa jambo baya mkono wa kushoto, ndugu tambua hilo ni shambulio la kisetani linalolenga  kukusababisha usiheshimiwe na watu na usiwe na uchumi mzuri.

Katika mikono si tu lazima  ushambuliwe bali hata kufunikwa kitu au kufungwa kitu n.k 

Muhimu tambua unawindwa uchumi na heshima. 
Wako watu ni wanandoa na wanadharauliwa na wenzi wao kiasi cha ndoa kujaa migogoro na wanapoomba huota ndotoni wanashambuliwa mkono wa kushoto na kumbe heshima yao imeondolewa.

 Unaweza kufanya kazi yako kwa bidii kuliko wenzako hapo kazini kwenu na bado wewe unaongoza kwa kudharauliwa na kumbe lilianzia rohoni na uliona ndotoni. 
Ndugu omba katika jina la YESU KRISTO na utazishinda hizo nguvu za giza zinazoshambulia mkono wako yaani zinashambulia uchumi na heshima yako, omba ndugu. 
Ayubu 16:20 "Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia MUNGU machozi;"

Unapokuwa huwezi kupewa heshima ujue kinachofuata kwako  ni kudharauliwa. 
Kuna matatizo mengi chanzo chake  ni vita ya kiroho kutoka kwa nguvu za giza, wewe unaweza kuona tatizo kwenye mkono wa kushoto na kumbe ni agenda ya kipepo ili usiheshimiwe na mtu yeyote. 
Ayubu 19:18 "Hata watoto wadogo hunidharau; Nikiondoka, huninena."

Nini ufanye juu ya shambulio la kuondoa heshima na utajiri/uchumi? 

Kuhusu HESHIMA.

1. Kwa damu ya YESU KRISTO takasa mikono yako kiroho kwa maombi na kutubu. 

Isaya 1:16 "Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;"

2. Ishi maisha matakatifu na ya  haki katika KRISTO YESU na heshima yako itarudi.

1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"

3. Kwa maombi katika jina la YESU KRISTO futa kila kifungo cha giza cha kukuondolea heshima. 

Yeremia 15:21 "Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha."

Kuhusu UTAJIRI/UCHUMI.
 
1. Tubu kwa ajili ya chanzo cha tatizo. 

Isaya 59:1-3 "Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia. Kwa maana mikono yenu imetiwa unajisi kwa damu, na vidole vyenu vimetiwa unajisi kwa uovu; midomo yenu imenena uongo, ndimi zenu zimenong'ona ubaya."

2. Tembea kwenye kanuni za ki Mungu zinazoleta utajiri na heshima.

 Mithali 3:9-10 "Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya."

3. Fanya kazi kwa juhudi zote.

 Mithali 10:4 "Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha."

Hakikisha tu unafanya kazi njema na halali. 

4. Ombea ufahamu wako. 

Mithali 21:5 "Mawazo ya wenye bidii huuelekea utajiri tu; Bali kila mwenye pupa huuelekea uhitaji."

5. Nyenyekea mbele za MUNGU. 

Mithali 22:4 "Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima."

6. Usitegemee akili zako mwenyewe bali mtegemee MUNGU katika KRISTO YESU 

Mithali 23:4 "Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe."

7. Takasa mikono yako kiroho na shughulikia tatizo hilo kiroho. 

 Walawi 20:7 "Jitakaseni basi, iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu."

8. Hitaji ulinzi wa MUNGU kwenye uchumi wako huku ukifanya kazi. 

Utaupata ulinzi wa MUNGU kwenye mali zako kwa wewe kutoa sadaka na zaka pamoja na dhabihu, yaani uwe mtoaji wa zaka na sadaka ndipo utaruhusu mbingu kulinda uchumi wako. 
 
Malaki 3:10-11 "Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi."

9. Haribu vifungo vya giza vilivofunga utajiri wako. 

Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."

10. Pambana na nguvu za giza zinazoshambulia uchumi wako kiroho huku ukiendelea kufanya kazi. 

Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

NINI UFANYE UNAPOSHAMBULIWA MIKONO AU  KUFUNGWA PINGU MIKONONI KWENYE ULIMWENGU WA ROHO 

Hii ni aina nyingine ya mashambulizi kwenye ulimwengu wa roho na inaweza kuwa na maana nyingine kabisa. 

Ona mfano huu.

Matendo  12:7 ".......... Minyororo yake ikamwanguka mikononi."
Petro alikuwa amefungwa minyororo kwenye mikono lakini ukisoma Biblia matendo 16:24 unawaona kina Paulo wakiwa gerezani wao walifungwa miguu na sio mikono.
Matendo 16:24 ".......... akawafunga miguu kwa mkatale."

Kwenye kipengele cha miguu nitafafanua wakati mwingine, lakini hapa nataka ujue kilichosababisha Petro kufungwa mikono na sio miguu ni kwa sababu alikuwa anawindwa mikono kwa sababu alikuwa na nguvu za kiroho za mikono.

Miguu hujulisha utayari ndio maana Paulo alifungwa miguu na sio mikono(Nitafafanua kwenye somo lingine juu ya kushambuliwa miguu ndotoni) 

Nimesema  miguu hujulisha utayari ndio maana Paulo alifungwa miguu na sio mikono, ukisoma Biblia utaona  Paulo kwa sababu alikuwa na nguvu za miguu alizunguka nchi nyingi akihubiri kuliko Petro hata Biblia yako kwenye ukifungua ramani mwanzoni au mwishoni mwa Biblia utaona ramani inaonyesha safari za Paulo na sio Petro, Paulo alikuwa na utayari zaidi wa miguu na ndio maana alifungwa miguu na Petro alikuwa na utayari zaidi  wa mikono na ndio maana alifungwa mikono, kwa haraka haraka tu ni kwamba Petro ndiye aliyetumia mikono kukamata mtu sikio,  petro alikuwa na utayari wa mikono na ndio maana alifungwa mikono(Yohana 18:10 ) hapo petro alikuwa hajajua matumizi ya mikono kiroho kwa utukufu wa MUNGU. 
Petro ndio aliyekuwa anatumia mikono yake kwa uvuvi wa watu ulipoanza kupitia Petro(Yohana 21:3) hivyo usishangae mahubiri yake yaliwapelekea watu 3,000 kuokoka siku moja tu kwa (matendo 2:14,37,41) hivyo mkono wa kiroho wa uvuvi wa samaki uliokuwa ndani ya Petro ulifanya kazi ya  kuvua watu na kuwafanya wateule wa MUNGU katika KRISTO YESU. 
Ni petro huyu ndiye aliyetumia mkono wake kumwinua kiwete na mda ule ule kiwete akapona(Matendo 3:6-7)

Mikono kiroho inashika hivyo ukifungwa mikono maana yake unazuiliwa kipepo kupata Baraka zote.

Ayubu 36:8 "Nao wakifungwa kwa pingu, Wakitwaliwa kwa kamba za mateso;"

Pingu hufungwa mikono hivyo mikono yako ikifungwa pingu kiroho maana huwezi kupata mafanikio hadi ufunguliwe kwa maombi katika jina la YESU KRISTO Mwokozi.

Kwanini wakufunge mikono kiroho?  
 Wanakufunga mikono kiroho kwa sababu  wamegundua una nguvu za kiroho za mikono.

Kama ulikuwa hujui ni kwamba kila mteule wa MUNGU ana asili ya nguvu zake kiroho kama ambavyo Samsoni nguvu zake zilikuwa katika nywele kiroho. 

Kuna wateule wa MUNGU wenye nguvu za vinywa, miguu, mikono,uso, na wengine wamepewa kiroho kuwa na nguvu zaidi ya moja n.k 
Sasa wakuu wa giza wakigundua mfano kwamba  asili ya nguvu zako ni kufanya kazi ya MUNGU au za kufanya kazi ili ufanikiwe kwa kutumia mikono basi wakipata nafasi usishangae kujikuta unaona kila mara ndotoni ukipata mashambulizi kwenye mikono yako kiroho. 
Ndugu inakupasa kufanya kazi na kuombea kazi ya mikono yako. 
Zaburi 90:17 "Na uzuri wa BWANA, Mungu wetu, uwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe."

Nini ufanye Ukiota umefungwa mikono kiroho au unashambuliwa mikono yote kiroho? 

1. Tubu kwa ajili ya tatizo.

Matendo 3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"

2. Haribu vifungo vya giza vilivyokufunga kwenye mikono yako kiroho na pambana hadi na madhabahu za giza zilizoleta nguvu hizo za giza ili kukufunga. 

Kumbu 12:3 "nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."

3. Achilia mapigo ya jina la YESU kwa wakuu wa giza wote waliokufunga. 

Yeremia 5:14 "Kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika kinywa chako kuwa moto, na watu hawa kuwa kuni, nao moto utawala."

4. Tambua kuwa ni nani aliyekufunga mikono ili upambane nae kiroho ili asipate nafasi tena siku nyingine kukufunga mikono yako. 

Waefeso 6:12 "Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."

Kuna watu wamelogwa mikono yako kiroho kiasi kwamba hata ukipewa mtaji milioni 50 bado unafilisika tu.
 Haribu kila nguvu za giza zilizofunga mikono yako, Tambua kuwa ni nani aliyekufunga mikono ili upambane nae kiroho ili asipate nafasi tena siku nyingine kukufunga mikono yako.

Shinda vita hiyo ya kiroho kwa maombi katika jina juu la YESU KRISTO na ishi maisha matakatifu na wokovu siku zote.

Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri. 
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
By  Peter  Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTOMwokozi.
+255714252292(Ni namba hii  kupiga,  kuandika meseji na pia whatsapp).

Uki-share kwa marafiki zako ujumbe  huu naomba share  kama ulivyo,usibadili jina wala chochote. 
.

Comments